Ijumaa, 5 Desemba 2014


Taasisi ya wazalendo Mkoa wa Kilimanjaro wakutana kuwapongeza wanachama wake kwa kuhitimu masomo yao. Baadhi ya wahitimu hao ni Ndg. Rashid A. Rashid shahada yake ya uzamivu na Ndg. Rusmah Ndossi shahada yake ya kwanza wote ni wahitimu wa chuo cha ushirika moshi Mkoani Kilimanjaro.

Picha ya pamoja wa kwanza kulia ni Ndg. Jerry Nzowa, Ndg. Rashid A. Rashid, Ndg. Adam Mapusa, Ndg. Daud Mrindoko, Ndg. Rusmah Ndossi, Ndg. Hassan Husein na Ndg. Juma Raibu
Kwa mujibu wa Katibu wazalendo Mkoa wa Kilimanjaro Ndg. Jerry Nzowa amesema.." Taasisi imeamua kuandaa hafla fupi ili kuwapongeza wanachama wenzetu kwa kuweza kuhitimu masomo yao. Hii ni moja ya jukumu la taasisi hii ya wazalendo kuhakikisha tunajenga umoja na udugu bila ya kujali itikadi zetu za aina yoyote iwe za kisiasa au za kidini. Kama Taasisi tunajukumu la kusaidiana katika shida na raha..."

Katibu wa wazalendo Mkoa wa Kilimanjaro Ndg. Jerry Nzowa akisema jambo

Tafrija hiyo imefanyika nyumbani kwa Mwenyekiti wa wazalendo Baraza la wazee Taifa Ndg. Adam Mapusa maeneo ya Moshi mjini. Pia, wametumia fursa hiyo kukumbushana kutanguliza uzalendo wa Taifa letu kwa kupinga na kuchukia rushwa kwa vitendo. 


Pia, wametumia fursa hiyo kuweka mikakati ya kuweza kuwasaidia vijana.Taasisi ya wazalendo imedhamiria kupambana na tatizo hilo ajira kwa kuweza kuanzisha miradi mbali mbali ili kuweza kuwasaidia vijana wazalendo wa Taifa hili.

Related Posts:

0 maoni:

Chapisha Maoni

Kumbukumbu la Blogu

Inaendeshwa na Blogger.

Machapisho Maarufu

Machapisho ya Karibuni

Recent Posts Widget