Katibu Hamasa na chipukizi UVCCM wilaya ya Moshi vijijini Ndg. Hassan husein akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Komela kata ya Marangu amefanikiwa kusambaratisha ngome ya wapinzani katika eneo hilo.
Katika mkutano huo uliohudhuriwa na wanakijiji wa eneo hilo Katibu wa Hamasa na Chipukizi UVCCM wilaya ya Moshi vijijini amewataka wananchi wa kijiji hicho kutokufanya makosa ya kuchagua kiongozi. Katibu huyo amewataka wananchi hao kumchagua kiongozi kwa kuangalia kama ana sifa za kuwa kiongozi ili wapate kiongozi bora na si bora kiongozi.
Amewataka wananchi kutambua sifa za kiongozi wanaye muhitaji ni lazima awe anajua pato la taifa linapopatikana na ajue wananchi ni wachangiaji hivyo wana haki ya kupata huo mgawo. Katibu huyo anasema.." wote tunajua umuhimu wa kupata viongozi hasa kipindi hiki, nawasihi tuchague viongozi si kwa itikadi zao bali tutizame sifa wanazo? Je, anatambua wananchi wake wanahitaji nini?.."
Pia, ametumia nafasi hiyo kuwanadi wagombea wa chama cha mapinduzi wa ngazi zote, huku akiwataka wananchi kuwaamini na kuwapa kura ndiyo siku hiyo ya kupiga kura. Baadhi ya wagombea aliowanadi ni Ndg. Alphonce Mavula kwa nafasi ya Uenyekiti wa kijiji na wagombea wote kwa nafasi za vitongoji.
Katika hali isiyo ya kawaida Mkutano wa chadema na Nccr-Mageuzi uliingia dosari baada ya wagombea wa vyama hivyo kugomba kwa kushutumiana kuhujumiana wenyewe, hali ambayo ilipelekea Mkutano huo kuvunjika hata kabla ya muda kuisha.
Katibu Hamasa na Chipukizi Ndg. Hassan husein akisema jambo mbele ya wananchi
Mkutano huo wa hadhara pia ulihudhuriwa na wananchi wa vitongoji vingine huku wenyeji wakiwa kitongoji cha Komela. Wananchi wamefarijika na namna mkutano huo ulivyoenda vema na elimu nzuri waliyopata toka kwa Katibu hamasa wa vijana wa wilaya.
Katibu wa itikadi ya siasa na uenezi ya kata wa CCM Ndg. Pantaleo Meela akimvalisha Katibu hamasa bendera ya chama cha mapinduzi katika mkutano huo wa hadhara. Upande wa kulia ni Katibu wa CCM kata Marangu Magharibi akifatilia tukio hilo kwa umakini.
Mgombea wa CCM kwa nafasi ya Uenyekiti wa kijiji cha Komela Ndg. Alphonce akipeana mkono na Katibu hamasa na chipukizi UVCCM wilaya ya moshi vijijini Ndg. Hassan husein
0 maoni:
Chapisha Maoni