Uingereza
imesaini makubaliano na Bahrain ya kujenga kituo cha jeshi la wanamaji
nchini humo ambacho kitakuwa ndicho kituo cha kwanza cha jeshi la
Uingereza eneo la mashariki ya kati tangu iondoke eneo hilo mwaka 1971.
Makubaliano hayo yaliafikiwa baada ya mieizi kadhaa ya mazungumzo.
Waziri
wa ulinzi nchini Uingereza Michael Fallon alisema kuwa kituo hicho
kitaliwezesa jeshi la wanamaji la Uingereza kuleta udhabiti eneo la
Ghuba.
Mwandishi wa masuala ya usalama wa BBC anasema kuwa
makubaliano hayo yanafanyika wakati nchi za Ghuba zinakabiliwa na tishio
kutoka kwa wanamgambo wa Islamic State.
0 maoni:
Chapisha Maoni