Katika sherehe hizo zilizoandaliwa na ofisi ya chama cha mapinduzi kata ya Makuyuni viongozi mbali mbali wa chama walihudhuria na kupata nafasi ya kuotoa neno la shukrani kwa wakazi wa mji mdogo wa Himo.Mwenezi wa wilaya ya Moshi vijijini Ndg. Jamal husein na mshindi wa kitongoji cha Miembeni Mji mdogo wa Himo
Baadhi ya viongozi waliojitokeza ni Mjumbe wa kamati ya siasa ya ccm wilaya ya moshi vijijin Ndg. Shayo maarufu kama Kingsize, Mama RP (Mjumbe wa kamati ya siasa wilaya ya moshi vijijini), Ndg. Innocent Melleck Shirima (Naibu kamanda Uvccm moshi vijijini), Ndg. Hassan husein (Katibu hamasa Uvccm moshi vijijini) na Makatibu mbali mbali wa chama cha mapinduzi toka wilaya ya moshi vijijini.Wakazi wa mji mdogo wa Himo waliojitokeza katika sherehe hizo
Wakazi waliojitekeza kusherehekea sherehe hizo za chama cha mapinduzi wamesifu uongozi wa chama cha mapinduiz kata ya Makuyuni kwa kuandaa sherehe hizo ili wakazi wajitokeze kusherehekea kwa pamoja kama shukrani kwa kuwachagua viongozi kupitia chama cha mapinduzi katika uchaguzi wa serikali za mitaa.Mjumbe wa kamati ya siasa wilaya ya moshi vijijin Ndg. Shayo (Kingsize)
Akiwahutubia mamia ya wakazi wa mji mdogo wa Himo, Naibu kamanda wa vijana moshi vijijini amewataka wakazi wa mji mdogo wa himo kuwapa ushirikianao viongozi waliochaguliwa ili waweze kutimiza kiu yao. Lakini pia, amewataka uchaguzi mkuu wa mwakani wasifanye makosa kuchagua madiwani na wabunge wa chama cha mapinduzi.Naibu kamanda wa Uvccm wilaya ya moshi vijijini Ndg. Innocent Melleck Shirima
Akiwashukuru wakazi wa mji mdogo wa Himo Ndg. Jamal Husein ambaye pia ni mwenezi wa ccm wilaya ya moshi vijijini amewataka wakazi kuzidisha imani kwa viongozi waliochaguliwa kupitia chama cha mapinduzi.
Ndg. Oliver Sanare ni mjumbe wa Baraza la uvccm mkoa wa Dar es salaam akiwahutubia wakazi wa mji mdogo wa Himo
Ndg. Pantaleo Meela ni mjumbe wa kamati ya utekelezaji wa uvccm wilaya ya moshi vijijini akiongea na wananchi
Baadhi ya makada wa chama cha mapinduzi waliohudhuria sherehe hizo
Ndg. Peter Msacky akisema jambo kwa wananchi wa Mji mdogo wa Himo alipopata nafasi ya kuongea nao
0 maoni:
Chapisha Maoni