Jumamosi, 6 Desemba 2014

 
                          Rais Mugabe na mkewe, Grace
Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe anatarajiwa kuhutubia maelfu ya wajumbe
katika siku ya mwisho ya mkutano mkuu wa chama tawala cha ZANU-PF mjini
Harare.
Katika hotuba yake Bwana Mugabe anatarajiwa kutangaza nani
atachukua nafasi ya makamo wa rais, Joice Mujuru, ambaye ametuhumiwa
kufanya ufisadi.
Waandishi wa habari wanasema aliyeelekea
kuteuliwa ni waziri wa sheria, Emmerson Mnangagwa, lakini baadhi ya watu
wanasema Rais Mugabe huenda akamteua mkewe, Grace, kuwa naibu wake.
Makamo wa rais ndiye huenda akarithi uongozi kutoka kwa Bwana Mugabe ambaye ametimia miaka 90.

0 maoni:

Chapisha Maoni

Kumbukumbu la Blogu

Inaendeshwa na Blogger.

Machapisho Maarufu

Machapisho ya Karibuni

Recent Posts Widget