Ijumaa, 19 Desemba 2014

TAASISI YA WAZALENDO TANZANIA.
Taarifa katika mitandao ya kijamii.
Kutokana na taarifa za uongo na uzushi zinazosambazwa mitandaoni kuhusu Taasisi ya wazalendo Tanzania. Baadhi ya tuhuma hizo ni kama ifuatavyo:-
1) Taasisi ya wazalendo Tanzania imeandaa tafrija maalumu ya kuukaribisha mwaka mpya itakayofanyika Mkoani Manyara wilayani Hanan'g
2: Taasisi ya wazalendo tayari kuwa imepata walezi na mmoja alietajwa katika habari zinazosambazwa ni Waziri Mkuu mstaafu Ndg. Fredrick T. Sumaye..
Taasisi ya wazalendo Tanzania inapenda kukanusha habari hizo za uongo na za upotoshaji wa makusudi wenye lengo la kutaka kuleta mgogoro na chuki baina ya wazalendo na jamii kwa ujumla wake, na wasiotakia mema taasisi ya wazalendo Tanzania.
Tunaomba tukanushe habari hizi za uongo na Katibu Mkuu wa Taasisi ya wazalendo Tanzania Ndg. MARTIN MUNIS hajahusika kwa namna yoyote ile kuandaa habari hiyo ya mitandaoni.
Taasisi ya wazalendo mpaka sasa haijaandaa tafrija ya kupokea mwaka mpya na kama itakuwa na mkakati huo itatangaza katika vyombo vya habari.
Pia, Taasisi ya wazalendo haina mlezi mpaka sasa. Na utaratibu wa kuwapata walezi utafanyika kwa utaratibu maalumu katika mkutano mkuu utakaofanyika hivi karibuni.
Mwisho, Taasisi ya wazalendo Tanzania inawaomba wazalendo wote na wapenda maendeleo ya nchi kupuuza habari zote za uongo zinahusu taasisi ya wazalendo, kwakuwa taasisi hii ina utaratibu wake maalumu wakutoa taarifa rasmi.
©Imetolewa na idara ya Habari na Maelezo.
Hassan husein

0 maoni:

Chapisha Maoni

Kumbukumbu la Blogu

Inaendeshwa na Blogger.

Machapisho Maarufu

Machapisho ya Karibuni

Recent Posts Widget