Ndege ya mizigo iliyosheheni silaha za kivita imekamatwa katika uwanja wa ndege wa Kano nchini Nigeria.
Licha
ya kukanusha awali, Urusi imesema inamiliki ndege ya mizigo iliyozuiwa
katika uwanja wa ndege wa Kano kaskazini mwa Nigeria baada ya
kugunduliwa imebeba silaha ambazo hazikuwa zimearifiwa.
Hata
hivyo, Msemaji wa Ubalozi wa Urusi nchini Nigeria, ambaye aliliambia
Shirika la Habari la Urusi TASS kwamba wanamiliki ndege hiyo, amesema
silaha hizo ni za kikosi cha kulinda amani cha Ufaransa.
Kwa mujibu wa Mwandishi wa habari wa BBC ndege hiyo bado inashikiliwa uwanjani hapo.
Awali,
msemaji wa kikosi cha kulinda amani cha Ufaransa katika Jamhuri ya
Afrika ya kati aliiambia BBC kwamba hawafahamu chochote kuhusu helikopta
mbili, magari ya kijeshi na silaha nyingine zilizokuwa katika ndege
hiyo.
Hata hivyo baadaye alipiga simu kufuta usemo wake kwa kusema
kuwa ndege hiyo ilikuwa imebeba silaha kwa ajili ya wanajeshi wao,
walioko katika kambi ya N’damena, ambazo zitapelekwa baadaye Ufaransa.
Msemaji
wa Ubalozi wa Urusi mjini Abuja alisema pia ndege hiyo ni yao.
Akitatanisha taarifa aliyoitoa awali kwamba ndege hiyo si yao.
Kwa
nini Ufaransa inatumia ndege ya Urusi kubeba silaha zake? na kwa nini
ilisimama katika uwanja wa Kano, wakati ikiwa inaelekea nchi jirani ya
Chad na hata Cameroun ikitokea Afrika ya kati? Kwanini baadhi ya silaha
hazikuorodheshwa katika ndege hiyo kama zimebebwa?.
Hayo ni maswali yalioulizwa pande zote.
Seriakli ya Nigeria ambayo ndio muhusika mkuu wa tukio hilo, haijasema chochote.
Baadhi
ya wachambuzi wanasema Nigeria inamiliki silaha hizo ilizonunua katika
soko haramu. Wengine wanasema silaha hizo zilinunuliwa kutoka kwa waasi
wa Seleka katika Jamhuri ya Afrika ya kati, wakielezea kwanini ndege
hiyo imeingia nchini humo kutoka mji mkuu wa nchi hiyo, Bangui.
Nigeria
imewekewa vikwazo vya silaha kutoka Marekani na nchi hiyo imekuwa
ikiarifiwa kutumia njia zisizo halali kupata silaha kwa ajili ya
kupambana na wapiganaji wa Boko haram
0 maoni:
Chapisha Maoni