Jumatatu, 1 Desemba 2014

Mwenyekiti wa wazalendo Taifa Ndg. Chief Daud Mrindoko
Leo Mwenyekiti wa wazalendo Taifa Ndg. Daud Mrindoko akiongea na waandishi wa habari mbali mbali ametangaza uteuzi wa viongozi wa wazalendo ngazi ya Taifa.

Nafasi kama ifuatavyo:-



1. Ndg. Adamu Mapusa- Nafasi ya Mwenyekiti Baraza la wazee wazalendo Taifa

2. Ndg.  Athuman Kala- Nafasi ya Katibu Baraza la wazee wazalendo Taifa

3. Ndg. Hamza King Majuto- Nafasi ya Katibu wa wazalendo Utamaduni na Michezo Taifa

4. Ndg. Hassan Husein- Nafasi ya Katibu wazalendo Maelezo na Habari Taifa.



Mwenyekiti wa wazalendo Taifa akinukuliwa na waandishi  wa habari amesema kuwa Wazalendo Tanzania ni taasisi inayojitegemea. Na inajumuisha watu wote ambao ni wazalendo wa Taifa lao kutoka katika vyama vyote vya siasa na dini zote na wote ambao hawana vyama vya siasa na wasio na dini na watu wote huwa huru.

Pia, amewataka watanzania kuuweka mbele uzalendo wao kwa maslahi ya Taifa letu na sio kwa maslahi yetu binafsi, jambo ambalo hupelekea kuwepo kwa vitendo vya kifisadi nchini.


0 maoni:

Chapisha Maoni

Kumbukumbu la Blogu

Inaendeshwa na Blogger.

Machapisho Maarufu

Machapisho ya Karibuni

Recent Posts Widget