Innocent Melleck Shirima mwanaharakati wa vijana |
Ameyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano maalumu na mtandao huu wa jamii.."nawasihi sana ndugu zangu wa vunjo kutorudia yale makosa ya mwaka 2010, kiongozi mzuri ni yule ambaye atakuwa daraja zuri kati yao na serikali kuu, halmashauri, wafadhili wa ndani na nje na hata wananchi wenyewe kwa wenyewe na sio uwezo wake binafsi wa mali au utajiri"
Innocent Melleck Shirima anasema kuwa baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakiwaaminisha wananchi kuwa mbunge tajiri atawasaidia wananchi wake hata kama hana uwezo au maarifa ya kuwasaidia wananchi wake. Hali hiyo ndio ambayo imewapelekea wananachi wa jimbo la vunjo kukosa maendeleo kwa kipindi kirefu sana. Anasema kuwa mwaka 2010 kijana ambaye ndiye alipaswa kuwa mtu sahihi kuwawakilisha wananchi wa jimbo la vunjo (Crispin Meela) kutokana na uwezo wake wa kuwa daraja zuri kwao alikosa nafasi hiyo kwa imani tu hana uwezo wa kimali hatimaye wananchi wa jimbo la vunjo wakamchagua mbunge ambaye kwasasa kwao ni mwiba na hakuna anaetaka kumsikia.
Mkuu wa wilaya ya Rungwe Crispin Meela |
James Mbatia mbunge wa kupitia Nccr-Mageuzi mwaka 1995 |
Amewataka wananchi wa jimbo la vunjo kutokubali kudanganywa kuwa hao wanaotaka kupewa nafasi kwa mara nyingine kama wataweza kuwaletea maendeleo kama vile kuboresha vipato vyao kwa kuishawishi serikali kuwawekea mazingira bora kama vile kuwajengea miundombinu bora ya barabara, umeme pamoja na kunufaika na rasilimali mlima kilimanjaro. Anasema" kwanza wananchi wa vunjo wanapaswa kujiuliza haya maendeleo ambayo leo wanadai watakuja kuyaleta, kwanini kipindi walivyokuwa wabunge hawakuweza kutimiza hayo? iweje leo waje na kusema kuwa wataweza kuleta hayo mabadiliko? huo ni utapeli wa mchana kabisa"
Innocent Melleck Shirima |
Anasema" nawaomba sana vijana waweze kuwahoji wabunge hao dhamira yao ya dhati kwao na sio tu dhamira yao iwe kuwatumia kisiasa kwa maslahi yao binafsi"
Mwisho, amewataka wananchi wa jimbo la vunjo kuwa wavumilivu kipindi hiki kigumu cha kuchagua viongozi wawatakao lakini wafanye maamuzi ya busara na sio ya kutaka kukomoa mtu au chama fulani.
0 maoni:
Chapisha Maoni