Ijumaa, 7 Novemba 2014

Katibu wa CCM(W) Moshi vijijini Miriam Sangit Kaaya wa kati akisalimiana na Makamu Mwenykiti wa CCM bara Ndg. Philip Mangula alipotembelea mkoani Kilimanjaro hivi karibuni.




Misimamo ya Katibu wa CCM(W) Moshi vijijini ya kusimamia Katiba na kanuni za Chama cha Mapinduzi, kimepelekea kuwatesa baadhi ya wanachama wanaotaka nafasi ya ubunge kupitia CCM hasa waliofikiria kutaka kubebwa na Katibu huyo kabla ya kura za maoni hasa kwa upande wa Jimbo la VUNJO.

Katibu huyo wa CCM wa wilaya tangu apewe wilaya hiyo kiutendaji, amekuwa akisimamia kanuni za chama kwa kuhakikisha anafanya kazi zake kwa uwazi na ushirikiano mkubwa na viongozi wenzake ili kuhakikisha haki inapatikana kwa wanachama wote wa CCM bila ya kubagua.

Kutokana na misimamo yake ya kusimamia ukweli siku zote, baadhi ya wasaka nafasi hiyo ya ubunge 2015 kwa upande wa vunjo waliotegemea kupendelewa na katibu huyo wameanza mikakati ya kutaka kumchafua mbele ya jamii il aonekane hafai na hatimaye watimize malengo yao ya kisiasa.



Miriam Kaaya(Katibu wa ccm wilaya moshi vijijini) akiwa na timu yake katika harakati za kujenga ma kustawisha chama cha Mapinduzi moja ya ziara zake anazoendelea nazo.


Hivi karibuni zimjitokeza baadhi ya habari toka katika magazeti kadhaa yakiripoti tuhuma mbali mbali zilizotolewa na wanaojiita makatibu kata wa CCm dhidi ya Katibu wa CCM wilaya bila kujitambulisha kwa majina yao kamili kwa vyanzo hivyo vya habari. Imebainika ni uzushi na chuki za kisiasa dhidi ya Katibu huyo wa wilaya kutokana na kusimamia ukweli juu ya utendaji wake ndani ya chama cha Mapinduzi.

Baadhi ya makatibu kata wa ccm toka jimbo la vunjo wakizungumzia habari hizo, wanasema wamesikitishwa sana na hizo habari za uongo na za uzushi dhidi ya Katibu wao wa wilaya. Wanaenda mbali wakimzungumzia katibu huyo wa wilaya kuwa ni katibu wa kipekee kumpata. Ni mwanamke lakini ni mchapakazi hodari kupata kuonekana, amekua karibu na watu siku zote. Ameweza kusimamia ilani ya CCM ipasavyo na amekuwa mkali kwa watendaji wa serikali wanaokwamisha ilani ya CCM.

Pia, makatibu hao wa kata wanasema ni katibu pekee aliyeweza kufanya kazi mpaka ngazi ya matawi kwa kufika huko na kuongea na mabalozi hao.

 Katibu wa ccm wilaya akiwa na katibu wa ccm mkoa Ndg. Deo Rutha, Mwenyekit wa ccm wilaya moshi vijijin Ndg. Masenga na Mbunge wa jimbo la moshi vjijini Ndg. Dkt. Cyrill Chami na baadhi ya wanachama wa CCM katika tukio la kuwapokea wanachama wapya tokea Chadema.


Katibu huyo wa CCM(w) Miriam Kaaya anawakumbusha wanachama wote wa CCM na wanaokipenda kushikamana kipindi hiki cha uchaguzi wa serikali za mitaa. Umoja wetu ndio utakuwa ushindi wa chama cha mapinduzi.





0 maoni:

Chapisha Maoni

Kumbukumbu la Blogu

Inaendeshwa na Blogger.

Machapisho Maarufu

Machapisho ya Karibuni

Recent Posts Widget