Alhamisi, 12 Februari 2015

Ndg. Daud Babu Mrindoko akiwa na baadhi ya akina mama wafanyabiashara ndogondogo
Katika tukio lisilokuwa la kawaida wakina mama ambao ni wafanyabiashara ndogondogo wamuomba kijana na kada wa chama cha Mapinduzi Ndg. Daudi Babu Mrindoko akubali wito wao wa kugombea jimbo la moshi mjini.
Tukio hilo limetokea mapema ya siku ya leo Alhamisi mara alipofika maeneo ya wafanyabiashara hao ili kupata mahitaji yake ya kawaida. Wakina mama hao ambao pia ni wafanyabiashara ndogondogo wamemtaka kijana huyo kugombea nafasi hiyo ya ubunge na kumuahidi kumuunga mkono katika kila hatua.
Wafanyabiashara hao wanasema kuwa wamelazimika kufanya hivyo hasa kutokana na kumfahamu vema kijana huyo uwezo wake wa kujitolea na kusaidia jamii. Baadhi yao wamesikika wakisema "kwasasa tunahitaji mabadiliko makubwa ya kiutawala mana hawa ambao wapo sasa bado hatujaona mchango wao kwetu, zaidi ni hali ya kimaisha kuzidi kuwa mbaya kila kukicha. Tunakuomba kijana wetu ukubali ombi letu mana tunatumbua uwezo wako wa kutumikia jamii"
Wafanyabiashara hao wamesikika wakisema safari hii hawatakubali kufanya makosa tena, shida ambayo wameipata kwa kipindi cha miaka kumi na tano hawapo tayari kuona hali hiyo inajirudia kwa mara nyingine tena..." Mwaka 2010 tulimpatia tena nafasi hiyo tukiamini kuwa kosa si kosa bali kurudia kosa, lakini bado makosa amezidi kuyarudia yale yale tena safari hii hali ndio mbaya zaidi sasa tumechoka na tunahitaji kufanya mabadiliko makubwa katika jimbo letu la moshi mjini"
Ndg. Daud Mrindoko akiwa anapata huduma
Kwa upande wa kijana huyo Ndg. Daudi Mrindoko amesema " Mimi kijana wenu sina mengi ya kuwaambia ila tuzidi ombeana kwa mwenyezi mungu mana ushauri wenu ni mzito sana, muda ukifika kila kitu kitakuwa wazi ila nimeupokea kwa mikono miwili ushauri wenu na hakika nitaufanyia kazi asanteni sana na mungu awabariki ninyi"
Wafanyabiashara wakiendelea na shughuli zao za kila siku sokoni

0 maoni:

Chapisha Maoni

Inaendeshwa na Blogger.

Machapisho Maarufu

Machapisho ya Karibuni

Recent Posts Widget