Katibu wa CCM wilaya ya Moshi vijijini MIRIAM SANGIT KAAYA
Katika tukio lisilokuwa la kawaida Makatibu wa CCM toka jimbo la Vunjo wilayani moshi vijijini wamekanusha taarifa zilizokuwa zimezagaa katika vyombo vya habari kuwa Katibu huyo wa wilaya anampango wa kuigawa CCM.
Makatibu hao waliyasema hayo juzi Jumamosi tarehe 8/11/2014 mbele ya vyombo vya habari katika ukumbi wa Kingsize wilayani Moshi vijijini. Makatibu hao wa kata walitumia muda mwingi kukanusha habari hizo za uongo zilizosemwa na hayo magazeti.
Wakati hayo yakiendelea Katibu wa CCM wilaya moshi vijijini alifika eneo hilo la tukio na kupokelewa kwa shangwe na Makatibu hao wa kata huku wakimwimbia nyimbo za kumsifu.."wana imani na Miriam, oyaa oyaa"..
Makatibu hao wanamuelezea katibu huyo kama ni mkombozi wao katika jimbo la vunjo. Wamuahidi kumpatia ushirikiano wa hali ya juu Katibu wao wa wilaya, nakutoa karipio kali kwa wale wote ambao watazusha taarifa za uongo dhidi ya katibu huyo wa wilaya.
Kwa upande wake Katibu huyo wa wilaya alivyopewa nafasi aliendelea kutoa msimamo ule ule " najua wapo wanaopendezwa na msimao wangu wa kusimamia katiba na kanuni bila ya kumpendelea au kumuone yeyote yule, lakini pia kwa msimamo wangu huu wapo wasiofurahia. Mimi ni mtendaji na jukumu langu ni kusimamia katiba na kanuni pamoja kuzilinda"
Pia, Katibu huyo amewaasa kipindi hiki cha uchaguzi wanachama wote kushikamana " Nawaasa viongozi wenzangu tushikamane kweli, mana ushindi wetu utatokana na mshikamano wetu. Lakini kipindi hichi tuzipuuze habari za kutaka kutugawanya mana hazina tija kwetu"
0 maoni:
Chapisha Maoni