Innocent Melleck akiwa na baadhi ya wananchi waliojitokeza |
Wananchi wa vunjo walijitokeza kwa wingi sana kumchangia mbunge wao mtarajiwa pesa ya kuchukulia fomu ya ubunge. Tukio hilo lilifanyika tarehe 07.03.2015 siku ya jumamosi mji mdogo wa Himo. Katika tukio hilo wananchi hao walimuomba kijana huyo Innocent Melleck akubali ombi lao la kugombea nafasi ya ubunge jimbo la vunjo kwakuwa wana imani naye sana.
Furaha ya wananchi kwa Innocent Melleck |
Wengi waliohudhuria katika viwanja hivyo walionekana kuwa na imani ombi lao litakubaliwa na kijana huyo. Katika mchango huo wa kumchangia kijana huyo zaidi ya kiasi cha shilingi za kitanzania milioni 2.6 ziliweza kupatikana.
Alipotakiwa kujibu ombi la wanavunjo kijana Innocent Melleck alisema.." Kwakuwa wazee wangu, vijana wenzangu mmeamua kunifanyia suprise katika hili na kuamua kutoa pesa zenu ambazo binafsi sifahamu mmeipataje, nataka niwaahidi ombi lenu nimelipokea kwa mikono miwili na muda ukifika nitafanya maamuzi sahihi. Naomba tujiandae kuvuka daraja hili. Asanteni sana tena sana"
Moja ya mashuhuda waliokuwepo eneo la tukio walioneka kujawa na furaha ya kila aina hasa kutokana na ombi lao kupokelewa na mbunge wao mtarajiwa.
Ni kwa miaka mingi sasa jimbo la vunjo limekuwa likikosa mtu sahihi wa kuwaletea maendeleo yao. Kutokana hali hiyo kijana Innocent Melleck anaonekana ni mtu sahihi na anaeungwa sana mkono na wananchi wa jimbo la vunjo. Hasa kutokana na historia yake kwa wananchi wa jimbo la vunjo kutokuwa na mashaka juu yake.
Mwananchi akipokea na kuanadika michango ya pesa |
Mmoja wa watu waliohudhuria alinukuliwa akisema kuwa.." Jimbo la vunjo watu wameligeuza kuwa shamba la bibi, kila anayejisikia anakuja. Lakini imekuwa ni fedheha kwetu kwa kitendo hiki mana nje ya jimbo la vunjo tunadharaulika sana. Kwa mfano wapo baadhi ya watu wanaotaka kugombea jimbo hili lakini ukifatilia historia yao tayari walishapata nafasi hiyo lakini walishindwa kabisa kuiweka vunjo katika hali ya nzuri ya kimaendeleo. Wapo wengi leo James Mbatia na Mrema wanataka tena hii ni dharau kubwa sana kwa wanavunjo na hakika hatupo tayari kuvumilia hili kutokea. Mana hatuwezi kuifanya vunjo kama nyanya ukienda sokoni na pesa unazipata nasema haiwezekani kabisa. Tuliwapa nafasi 1995-2000 na 2010-2015 hakuna jipya walilofanya halafu leo bila haya wala aibu wanakuja tena kwa mara nyingine huu ni udhalilishaji wa makusudi kabisa"
Uchaguzi wa nafasi za ubunge unatarajiwa kufanyika oktoba 2015 huku vyama vinne vya kisiasa kila kimoja kimejinasibu kusimamisha wagombea wake.
Innocent Melleck Shirima akiongea na wananchi waliomuomba atangaze nia haraka iwezekanavyo |
0 maoni:
Chapisha Maoni