Rais Uhuru Kenyatta mara ya mwisho alipokuwa katika mahakama ya ICC
Mahakama ya
kimataifa ya ICC imetupilia mbali kesi ya jinai inayomkabili Rais wa Kenya
Uhuru Kenyatta.
Mwendesha
mkuu wa mashitaka Fatou Bensouda ameondoa kesi dhidi ya Kenyatta ambaye
alidaiwa kutenda uhalifu dhidi ya binadamu wakati wa ghasia za baada ya
uchaguzi mwaka 2007/2008.
Mahakama
ilikuwa imempa Bensouda wiki moja kuamua ikiwa ataendelea na kesi dhidi ya
Kenyatta au la inagwa alisema muda huo haukutosha kwake yeye kuandaa ushahidi
zaidi dhidi ya Kenyatta.
Kenyatta
alishtakiwa kama mshukiwa mkuu wa ghasia za baada ya uchaguzi wa 2007/2008
akituhimiwa pamoja na William Ruto ambaye ni naibu Rais kwa kutenda uhalifu
dhidi ya binadamu.
Zaidi ya
watu elfu moja waliuawa wakati wa ghasia hizo. Uhuru alikuwa mtu maarufu zaidi
kufikishwa mahakamani na pia mshukiwa mkuu kwani alifikishw amahakamani akiwa
Rais aliye mamlakani.
Hili ni pigo
kubwa kwa upande wa mashitaka, wengi wlaioana keshi dhidi ya Kenyatta kama
mtihani mkubwa katika historia ya mahakama hio.
Upande wa
mashitaka ulitaka mahakama kuupatia muda zaidi ili upate ushahidi zaidi,dhidi
ya Kenyatta kama vile taarifa za akaunti yake ya benki.
Upande wa
utetezi uliteta kuwa ikiwa hakuna ushahidi wa kutosha kesi hio inapaswa
kutupiliwa mbali
0 maoni:
Chapisha Maoni