Jumatano, 3 Desemba 2014



Kada wa chama cha Mapinduzi Ndg. Oliver Sanare atembelea kituo cha kulelea watoto yatima na kujumuika nao. Kada huyo wa chama cha Mapinduzi ambaye pia ni mwanachama wa Umoja wa vijana wa CCM alitembelea kituo cha KILI CENTER MOSHI VIJIJINI Mkoani Kilimanjaro.

Tukio hilo limeenda sambamba na kusherehekea siku ya kuzaliwa kwake, akinukuliwa na blog hii Oliver anasema.." leo ni siku yangu ya kuzaliwa hivyo nimeona ni busara siku ya leo kutembelea kituo hiki cha kulelea watoto yatima na kujumuika nao, lakini nikaona ni vema nikaja na zawadi hizi ili nao wafurahi kama mimi. Nimefanya haya kwa mapenzi yangu na kwa utashi wangu.."







Pia, aliambatana na baadhi ya marafiki zake ambao walijumuika nae katika lengo la kumpa sapoti siku ya leo ambayo kwake ilikuwa ni muhimu sana.

Baadhi ya marafiki zake ambao ameweza kuambatana nao kwa nafasi zao wamempongeza sana kwa kitendo chake cha kiungwana cha kuamua kutumia siku yake nzima ya leo kujumuika na watoto hao.





 Baadhi yao wamesema kuwa kitendo hiki ni cha mfano wa kuigwa na watu wote katika jamii. Walisikika wakisema.." nampongeza sana Oliver kwa hatua hii alioamua kuchukua kujumuika na hawa watoto, siku ya leo aliweza kuamua kufanya jambo lolote ili kuweza kutimiza lengo lake kusherehekea siku ya kuzaliwa, tumezoea kuona wengine wakialika marafiki tu lakini huyu ameamua kujumuika na marafiki na watoto kama hawa ambao hawana wazazi kwa kweli nampongeza sana kwa kitendo hiki na wengine tuige jambo kama hili.."



 Kwa upande wa watoto waliotembelewa na mgeni wao Oliver Sanare wanasema wamefurahishwa sana na ujio wake na msaada wake aliowapatia.

Baadhi walisikika wakisema.." siku ya leo ni nzuri kwetu kutokana na ujio huo, tunapenda wageni na tunajisikia amani kutembelewa na wageni hakika kwetu ni  faraja kama vile mgonjwa anapotembelewa akiwa hospitalini. Tunawaomba na wengine waige mfano wake.."



 Oliver Sanare akikabidhi msaada kwa watoto hao alipowatembele kituoni hapo
 Baadhi ya zawadi alizozitoa alipotembelea kituoni hapo


 Baadhi ya marafiki zake aliojumika nao wakipata chakula wa kwanza kulia ni Juma Raibu, Chief Daud Mrindoko(Mwenyekiti wa wazalendo Taifa), Pantaleo Meela na Oliver Sanare



 Oliver Sanare akicheza na watoto aliowatembelea kituoni hapo

 Oliver Sanare akiwa amewabeba watoto wa kituoni hapo wakifurahu jambo
 Picha ya kwa pamoja
 Akikabidhi zawadi kwa watoto wa kituoni hapo




















Kwa hisani ya Mtanzania Jitambue:

0 maoni:

Chapisha Maoni

Kumbukumbu la Blogu

Inaendeshwa na Blogger.

Machapisho Maarufu

Machapisho ya Karibuni

Recent Posts Widget