Jumatatu, 2 Februari 2015

Viongozi wa chama cha mapinduzi wilaya ya moshi vijijini wakiwasili hospitali ya Kilema
Chama cha Mapinduzi wilayani moshi vijijini siku ya Jumapili tarehe 01/02/2015 kimeadhimisha miaka 38 kuzaliwa kwake kwa kutembelea wagonjwa waliolazwa hospitali ya Kilema. Wakiongozwa na Katibu wa wilaya wa chama hicho Ndg. Mirism S. Kaaya waliweza kutoa misaada mbalimbali kwa wagonjwa hao waliwakuta hospitalini hapo.



Katibu wa CCM wilaya ya Moshi vijijini Miriam S. Kaaya akisaini daftari la wageni mara alipowasili hospitalini hapo
Baadhi ya misaada waliyotoa hospitalini hapo ni pamoja na vyakula, sabuni za kufulia na kuogea, dawa za miswaki n.k. Zawadi hizo zimetolewa kwa lengo la kuwafariji na kuwaombea kwa mungu wapone kwa haraka ili waweze kurejea katika hali zao za kawaida



Katibu wa itikadi na uenezi CCM wilaya ya Moshi vijijini Ndg. Husein Jamal akisaini kitabu cha wageni hospitalini hapo
Huu ni utaratibu wa kawaida wa chama hicho kufanya kazi za kijamii mara kwa mara. Akihojiwa Katibu wa wilaya wa CCM moshi vijijini Miriam Kaaya amesema "Hili ni jambao la kawaida kwa chama cha mapinduzi kufanya shughuli za kijamii, tunaazimisha miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM kama ofisi ya wilaya safari hii imeona iadhimishe kwa aina hii ya kuwatembelea wagonjwa wa hospital ya Kilema"



Katibu wa CCM wilaya akimfariji mgonjwa ambaye kwa sasa yupo kitandani kwa muda wa mwaka mzima hospitalini hapo
Pia, katibu wa CCM wilaya moshi vijijini ametumia nafasi hiyo kuwapa pole wagonjwa na kuwaombea wapone haraka ili waje kujena Taifa lao. Akinukuliwa akisema " Tumekuja kuwatembelea ili kuwapa pole kwa kuumwa lakini pia kuzidi kuwaombea kwa mungu mpone kwa haraka ili mrudi kulitumikia taifa lenu"



Katibu wa itikadi na uenezi CCM wilaya moshi vijijini Ndg. Husein Jamal akimfariji mtoto aliyevunjika mguu alipotembela wodi ya wagonjwa hiyo
Viongozi wengine waliombata katika msafara huo ni makatibu wa jumuiya za chama hicho Ndg. Kulwa(Katibu msaidizi CCM wilaya), Ndg. Abdulkarim Halamga(Katibu Uvccm wilaya), Ndg. Justina Bayo(Katibu Uwt wilaya), Ndg. Hassan husein(Katibu Hamasa Uvccm wilaya) na viongozi mbali mbali wa Kata ya Kilema Kusini.



Katibu wa Uvccm wilaya moshi vijijini Ndg. Abdulkarim Halamga akikabidhi msaada kwa mgonjwa wodi ya wazazi
Ujio huo umewapa matumaini makubwa wagonjwa wa hospitalini hapo. Wagonjwa wameshukuru kwa kitendo hichokilichofanywa na chama cha mapinduzi wilaya ya moshi vijijini na kuvitaka vyama vingine kuiga mfano wa chama hicho kikongwe nchini.



Katibu wa CCM wilaya akiwa amembeba mtoto mchanga wodi ya wazazi


 FUATILIA PICHA ZA MATUKIO

Katibu Hamasa Uvccm wilaya ya moshi vijijini Ndg. Hassan husein akikabidhi zawadi mbalimbali kwa wagonjwa
Katibu wa UWT wilaya ya moshi vijijini Ndg. Justina Bayo akiwa amembeba mtoto mchanga
Picha ya kwa pamoja viongozi wa chama cha mapinduzi na viongozi wa hospitali ya Kilema


















0 maoni:

Chapisha Maoni

Inaendeshwa na Blogger.

Machapisho Maarufu

Machapisho ya Karibuni

Recent Posts Widget