WISTON MOGHA, ZITTO KABWE USO KWA USO 2015.
Mbunge wa Kigoma kaskazini, Zitto Kabwe aliyetangaza kutogombea tena katika Jimbo hilo na kunukuliwa mara kadhaa akisema anakusudia kugombea Urais mwaka 2015 au akikwama atagombea Ubunge Jimbo la Kigoma Mjini, sasa amepata mpinzani katika Jimbo hilo. Akizungumzia jambo hilo, Wiston Mogha alisema ameamua kugombea nafasi hiyo ya Ubunge baada ya kugundua kero nyingi katika Jimbo hilo zimeshindwa kutatuliwa. Alisema ameamua kugombea Ubunge kwa ajili ya kuleta mabadiliko ya kweli kwa Wananchi ikizingatiwa kwamba ipo ndoto ya kufikia malengo ya Kigoma tuitakayo ambayo bado Wawakilishi waliopo sasa wameshindwa kuifikia, lakini anaamini yeye (Mogha) ataweza kufanya haya yaliyowashinda wengi. Amedai kuwa Mbunge wa sasa (Peter Serukamba) ameshindwa kuleta mabadiliko ya Mji wa Kigoma Ujiji na matokeo yake hali ya kiuchumi kwa Watu inazidi kuwa ngumu licha ya kuzungukwa na fursa za kila aina kama vile Ziwa Tanganyika, ardhi nzuri kwa ajili ya kilimo na uwepo wa Bandari ya uhakika Kigoma Mjini. Anasema akifanikiwa kuwa Mbunge wa Kigoma Mjini atahakikisha anaibana Serikali kutangaza vivutio vya Ziwa Tanganyika ikiwa ni pamoja na kutafuta Wawekezaji katika sekta ya uvuvi ili walete Meli za kuvulia Samaki, hivyo kufikia malengo ya kujenga kiwanda cha kusindika Samaki Mjini Kigoma. Kujengwa kwa Kiwanda cha kusindika Samaki kutaongeza fursa ya ajira kwa Wananchi kiasi kwamba itasaidia kupunguza wimbi la Vijana kukimbilia katika Mikoa mingine kutafuta ajira. Hata hivyo amesema Mbunge wa sasa hana mahusiano mazuri na Madiwani wengi ambao ndio wanaoongoza Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji, pia hajui shida za Wananchi kwa kuwa ameshindwa kufanya mikutano ya hadhara na badala yake amekuwa akivizia ziara za Viongozi wa Kitaifa kuongea na Wananchi. Mogha ambaye amedai atagombea kupitia Chama cha ACT Tanzania anatarajiwa kutoa upinzani mkali kwa Zitto Kabwe endapo ataamua kugombea Ubunge Kigoma Mjini japokuwa hajatangaza ni Chama gani atapitia ingawa kuna tetesi kutoka kwa Rafiki zake wa karibu kwamba atagombea kupitia ACT Tanzania. Wakati Mogha akieleza nia yake aliyodai haikutokana na kuombwa au kushurutishwa na yeyote, amesema amejipanga vizuri kukabiliana na Mtu au Watu watakaojitokeza kuanzia kura za maoni ndani ya Chama chake na hata Uchaguzi mkuu wenyewe kwa kukabiliana na Wagombea wa Vyama vingine vya siasa.
Wiston Mogha akiwa anaongea na MTANZANIA JITAMBUE amesema kwanza anaomba Uzima wa afya na pia anawashukuru sana vijana wenzake kumuonyesha anaweza kugombea 2015 Katika jimbo hilo na demokrasia na Kushindana na si kushindana tu bali ni kuleta Maendeleo kwa Wananchi...
2015 Patachimbika....alimalizia kwa hilo...
0 maoni:
Chapisha Maoni