Kwa moyo Wa dhati kabisa nawapongeza wote walioshinda nafasi za Uongozi ndani ya BAVICHA.
Nawapongeza pia wote walioshindwa na nawatia moyo kwamba there is always next battle. Hongereni kwa kushiriki.
Nawashauri muunganishe nguvu zenu wote mlioshindwa na kushinda ili msije kurudia makosa ya waliowatangulia.
Watanzania wanahitaji Mabadiliko, watanzania wanahitaji kuiona CCM ikiondoka madarakani. Watanzania wanahitaji fikra mpya na mbadala.
Uchaguzi wenu usiwe sababu ya kuwa na mpasuko, uchaguzi wenu uwe njia sahihi na salama kuelekea kuimarisha demokrasia ya kweli.
Yawwzekana hamfurahishwi na matokeo, lakini hayo ndio matokeo na lazima muyaheshimu.
Unganisheni nguvu. Msitengane, pendaneni msichukiane.
Habib Mchange
0 maoni:
Chapisha Maoni