MTUME AOA MKE WA PILI!
Mtume Peter Rashid Abubakari, kiongozi wa
kanisa la RGC lililoko Mbezi Kimara Dar Es
Salaam, ameamua kumuacha mke wake Bi
Zuwena (Catherine) aliyeoana naye tangu mwaka
1985.
Alipohojiwa inakuwaje kwa nini amuache na
kumuoa Pamela Didas Asenga, binti mdogo wa
miaka 20, alidai ndoa yake hiyo ya mwanzo
haikuwa halali kwa kuwa alioa akiwa bado
mwislamu na alifungishwa na shehe! Kwa hiyo
mungu amemfunulia na amempa mke mwingine
mwema!
Ndoa hiyo ilifungwa tarehe 29/08/2014,
ilifungishwa na Askofu Innocent Lugagi, wa
kanisa la White House la Durban Afrika Kusini!
Mtume Peter Rashid Abubakar baada tu ya
kutoka kufunga ndoa yake South Afrika amerudi
nchini Tanzania na Jumapili akiwa kanisani kwake
awatangazia waumini wake kuwa kama una mke
ambaye mlichukuana wakati wa ujinga wenu na
umekaa naye miaka mitatu au zaidi na hana
tabia ya kimungu mkorofi na mchokozi na
hujafunga naye ndoa ACHANA NAYE ILI MUNGU
AKUPE MKE MWEMA. Na mwanamke naye
vilevile.
Alipohojiwa na mmojawapo wa marafiki zake
aliyeshangazwa na tukio hilo, kwenye ukurasa
wake wa Facebook mtume huyo alijibu hivi:
“…… tafsiri ya mke ni yule uliyefunga naye ndoa
kanisani au kwa DC 1Kor 7:15. Huyo nilikuwa
nazini naye tu!! Mungu aliponifunulia siri hiyo
nikatubu na kumuomba Mungu anipe mke
mwema na amenipa.”
KWA MAELEZO ZAIDI TEMBELEA UKURASA WAKE
WA FB (PETER RASHID)
Hizi hpa akipokelewa airport
Mwandishi wa MTANZANIA JITAMBUE
Alhamisi, 18 Septemba 2014
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
0 maoni:
Chapisha Maoni