Alhamisi, 11 Septemba 2014

Mzee Mengi kwa muda mrefu ameonekana ni mshirika wa karibu  wa CDM.

Sasa jiulize  kwanini Mzee Mengi alimtaka Upendo Peneza ashinde Uenyekiti wa BAVICHA?

Amemuwezesha kifedha na alitumia vituo vya ITV na EATV kujinadi katika  kampeni zake.

Pia Chadema wametakaa kuwaadaa watu kupitia uchaguzi wa Bavicha kama  wao hawana ukanda.
Wametumia nguvu kubwa kuhakikisha Ephata Nanyaro hawezi kushindaa licha ya usmart wake katika uongozi na anakijua chama.
Lengo ni kufanya  hivyo ni sababu Nanyaro anatokea Arusha.

Heche alitokea Kanda ya Ziwa katika Mkoa  wa Mara.
Mrithi wake Petrobas nae anatokea Kanda ya Ziwa huko Shinyanga/Mwanza.

Lakini wamesahau kuwa Patrick Ole Sosopi ni wa Kaskazini anayeishi Iringa.

Sasa subirini vituko maana kwa sasa KAMATI TENDAJI YA BAVICHA inakutana kumchagua Katibu na Naibu wa Baraza hilo.
Kuna Dada anaitwa Pamela ndiye atakuwa Katibu na huyu anatokea Kaskazini na wanataka kufukia kombe ili mwanaharamu apite(mfumo dume wa Chama).

Ila napenda kuwaambia tu kuwa mzimu wa mtoto wa kigoma umeendelea kutawala kwenye uchaguzi huu wa Bavicha.
Wapo wanaojaribu kumuhusisha Petrobass na Mbowe pamoja na Heche kama chaguo lao si kweli.
Petrobass anazipenda sana siasa na falsafa za Zitto sambamba na Makamu wake Sosopi ambaye kwa upande mwingine ni kijana wa Msigwa.

Chaguo la Mbowe na washirika wake walikuwa ni;

Daniel Naftari- Uenyekiti
Jesca Kishoa-M/Mwenyekiti.

Sasa ngoma ipo kwenye Bawacha maana Chaguo la Wanawake ni Sophia Hebron Mwakagenda lakini Mbowe na washirika wake wanamtaka Halima Mdee(huyu ni wa Kaskazini)

Nataka niwahakikishie kuwa safari hii Mbowe atashinda kama yeye(mazwazwa watamchagu tu) lakini wagombea wake wote watapigwa chini.
Kama tukifuata Demokrasia na uzoefu na kukijua Chama basi nafasi ya Makamu Mwenyekiti Chadema Bara anatakiwa awe ni binti hodari Martha Noah lakini mfumo dume unamnyima nafasi pia umaarufu wa kisiasa wa kina Prof. Safari.

Kituko kingine cha Mbowe na washirika wake ni kulazimisha yule Mzanzibar awe Mwenyekiti Baraza la Wazee kigezo cha Uislam na upande wa Muungao lakini hana uwezo zaidi ya Arcado Ntagazwa aliyeongoza kura kwa awamu zote 2.

Kichekesho kingine ni wagombea kutofanyiwa usaili(hapa ndio CCM wanapotuzidi na kuonekana Chama makini)
Lengo la Chama ni kuhofia watakaokatwa watakimbia na kujiunga CCM na hasa wengi ACT.

Uchaguzi wenyewe wa Shuleni au Vyuoni kunakuwa na Usaili sasa Kulikoni Chadema???

Hivi unadhania bila usaili pale Simba hii leo Michael Wambura angekuwa ni Rais wa Klabu hiyo.

Bila ya Usaili kule UVCCM hii leo wangekuwa na uongozi wa yule Muunguja Jamal na Mgogo Mavunde.

Sasa uoga wa Mbowe na washirika wake ni upi juu ya Usaili?

Namalizia kwa kusema hivi Bavicha inaelekea kufa kwa kushikwa masikio na Mbowe.
Huwezi ukawa Live Mitandao yote na televisheni kisha ukatoa maneno ya kupandikiza chuki na hasira kwa vijana.
Ndicho alichokifanya jana Mbowe hapa Mlimani City.

Tahadhali vijana mjitambue na mjue kuna maisha nje ya Siasa na tuna Taifa linaloitwa Tanzania(maana mie cjawahi kuiona Tanganyika).
Hivyo tunapaswa kuwa na familia na kujimudu katika Uchumi wa kipato katika kuendesha familia zetu zaidi ya kuandamanishwa.

Naombeni uzi huu usambae kwenye Mitandao yote hasa kwenye wall na group za fb na whatsapp.
Muhimu upelekeni JF na MWAHAHALISI FORUM ili Watanzania waone ujinga wa Chadema katika kujificha ndani ya vivuli vyetu.

Nikiripoti toka hapa Mlimani City.

Wako,

MSEMAKWELI UCHUKIWA.

0 maoni:

Chapisha Maoni

Kumbukumbu la Blogu

Inaendeshwa na Blogger.

Machapisho Maarufu

Machapisho ya Karibuni

Recent Posts Widget