Jumatano, 24 Septemba 2014

WISTON MOGHA, ZITTO KABWE USO KWA USO 2015.
Mbunge wa Kigoma kaskazini, Zitto Kabwe aliyetangaza kutogombea tena katika Jimbo hilo na kunukuliwa mara kadhaa akisema anakusudia kugombea Urais mwaka 2015 au akikwama atagombea Ubunge Jimbo la Kigoma Mjini, sasa amepata mpinzani katika Jimbo hilo. Akizungumzia jambo hilo, Wiston Mogha alisema ameamua kugombea nafasi hiyo ya Ubunge baada ya kugundua kero nyingi katika Jimbo hilo zimeshindwa kutatuliwa. Alisema ameamua kugombea Ubunge kwa ajili ya kuleta mabadiliko ya kweli kwa Wananchi ikizingatiwa kwamba ipo ndoto ya kufikia malengo ya Kigoma tuitakayo ambayo bado Wawakilishi waliopo sasa wameshindwa kuifikia, lakini anaamini yeye (Mogha) ataweza kufanya haya yaliyowashinda wengi. Amedai  kuwa Mbunge wa sasa (Peter Serukamba) ameshindwa kuleta mabadiliko ya Mji wa Kigoma Ujiji na matokeo yake hali ya kiuchumi kwa Watu inazidi kuwa ngumu licha ya kuzungukwa na fursa za kila aina kama vile Ziwa Tanganyika, ardhi nzuri kwa ajili ya kilimo na uwepo wa Bandari ya uhakika Kigoma Mjini. Anasema akifanikiwa kuwa Mbunge wa Kigoma Mjini atahakikisha anaibana Serikali kutangaza vivutio vya Ziwa Tanganyika ikiwa ni pamoja na kutafuta Wawekezaji katika sekta ya uvuvi ili walete Meli za kuvulia Samaki, hivyo kufikia malengo ya kujenga kiwanda cha kusindika Samaki Mjini Kigoma. Kujengwa kwa Kiwanda cha kusindika Samaki kutaongeza fursa ya ajira kwa Wananchi kiasi kwamba itasaidia kupunguza wimbi la Vijana kukimbilia katika Mikoa mingine kutafuta ajira. Hata hivyo amesema Mbunge wa sasa hana mahusiano mazuri na Madiwani wengi ambao ndio wanaoongoza Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji, pia hajui shida za Wananchi kwa kuwa ameshindwa kufanya mikutano ya hadhara na badala yake amekuwa akivizia ziara za Viongozi wa Kitaifa kuongea na Wananchi. Mogha ambaye amedai atagombea kupitia Chama cha ACT Tanzania anatarajiwa kutoa upinzani mkali kwa Zitto Kabwe endapo ataamua kugombea Ubunge Kigoma Mjini japokuwa hajatangaza ni Chama gani atapitia ingawa kuna tetesi kutoka kwa Rafiki zake wa karibu kwamba atagombea kupitia ACT Tanzania. Wakati Mogha akieleza nia yake aliyodai haikutokana na kuombwa au kushurutishwa na yeyote, amesema amejipanga vizuri kukabiliana na Mtu au Watu watakaojitokeza kuanzia kura za maoni ndani ya Chama chake na hata Uchaguzi mkuu wenyewe kwa kukabiliana na Wagombea wa Vyama vingine vya siasa.

Wiston Mogha akiwa anaongea na MTANZANIA JITAMBUE amesema kwanza anaomba Uzima wa afya na pia anawashukuru sana vijana wenzake kumuonyesha anaweza kugombea 2015 Katika jimbo hilo na demokrasia na Kushindana na si kushindana tu bali ni kuleta Maendeleo kwa Wananchi...

2015 Patachimbika....alimalizia kwa hilo...

Jumamosi, 20 Septemba 2014

Yanga yapigwa na walima Miwa wa Morogoro....Washabiki wa yanga hawakuamini yanayotokea uwanjani huku Mchezaji wao mahiri JAJA akiwa anakosa magoli km Vile miguu imefungwa mawe...Watani wao Simba amabao Mashabiki waliokuwepo uwanjani wanasema yanga ililambishwa Sukari guri wakaona ni Tamu sasa wanaipata uchungu wakiwa uwanjani...MTANZANIA JITAMBUE akimsikiliza Mshabiki wa MTIBWA anasema kwao YANGA c timu tishio mpk wamewapiga 2-0 Na JAJA wao kwani kwetu JAJA sasa Sisi tunaye JUJU...

MPAKA MWISHO WA DAKIKA 90
YANGA O-2 MTIBWA
KWA MANTIKI HIYO MTIBWA NDIYO ALIYEIBUKA MSHINDI....

Kauli za kishujaa za Mashabiki wa YANGA...
YANGA MSIOGOPE KUFUNGWA KWANI KAFUGWA BABU SEYA, NA BADO ANAENDELEA KUFUNGWA.....NAIPENDA YANGA!!!!!

Mleta habari wenu kutoka MOROGORO-MTANZANIA JITAMBUE

Alhamisi, 18 Septemba 2014

MTUME AOA MKE WA PILI!
Mtume Peter Rashid Abubakari, kiongozi wa
kanisa la RGC lililoko Mbezi Kimara Dar Es
Salaam, ameamua kumuacha mke wake Bi
Zuwena (Catherine) aliyeoana naye tangu mwaka
1985.
Alipohojiwa inakuwaje kwa nini amuache na
kumuoa Pamela Didas Asenga, binti mdogo wa
miaka 20, alidai ndoa yake hiyo ya mwanzo
haikuwa halali kwa kuwa alioa akiwa bado
mwislamu na alifungishwa na shehe! Kwa hiyo
mungu amemfunulia na amempa mke mwingine
mwema!
Ndoa hiyo ilifungwa tarehe 29/08/2014,
ilifungishwa na Askofu Innocent Lugagi, wa
kanisa la White House la Durban Afrika Kusini!
Mtume Peter Rashid Abubakar baada tu ya
kutoka kufunga ndoa yake South Afrika amerudi
nchini Tanzania na Jumapili akiwa kanisani kwake
awatangazia waumini wake kuwa kama una mke
ambaye mlichukuana wakati wa ujinga wenu na
umekaa naye miaka mitatu au zaidi na hana
tabia ya kimungu mkorofi na mchokozi na
hujafunga naye ndoa ACHANA NAYE ILI MUNGU
AKUPE MKE MWEMA. Na mwanamke naye
vilevile.
Alipohojiwa na mmojawapo wa marafiki zake
aliyeshangazwa na tukio hilo, kwenye ukurasa
wake wa Facebook mtume huyo alijibu hivi:
“…… tafsiri ya mke ni yule uliyefunga naye ndoa
kanisani au kwa DC 1Kor 7:15. Huyo nilikuwa
nazini naye tu!! Mungu aliponifunulia siri hiyo
nikatubu na kumuomba Mungu anipe mke
mwema na amenipa.”
KWA MAELEZO ZAIDI TEMBELEA UKURASA WAKE
WA FB (PETER RASHID)
Hizi hpa akipokelewa airport
Mwandishi wa MTANZANIA JITAMBUE

TAMKO!!
UMOJA WA VIJANA WAZALENDO WA VYUO VYA ELIMU YA JUU DAR ES SALAAM!!

TAMKO!!
KULAANI KAULI ZA MWENYEKITI WA CHADEMA TAIFA!!

TAMKO
KULAANI KUHAMASISHA UASI KWA NJIA YA MAANDAMANO

Sisi ni vijana wasomi wazalendo kutoka vyuo vikuu mbalimbali vilivyoko Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM); Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU); Dar es Salaam University College of Education (DUCE);USTAWI WA JAMII; Chuo Kikuu cha Mtakatifu John (St. John); Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM); Chuo KikuuHuria cha Tanzania (OUT); Kampala International University (KIU); Dar es Salaam Institute of Technology (DIT); Institute of Adult Education (IAE); Tanzania School of Journalism (TSJ); College of Business Education (CBE), Chuo cha Uhasibu (TIA) na Chuo cha kumbukumbu ya Mwl JK Nyerere.Tunachukua fursa hii kulaani vikali kauli zilizotolewa na Mh. Freeman Mbowe ambae ni Mwenyekiti wa CHADEMA ya kutaka kuitisha maandamano ya nchi nzima bila kikomo pamoja na kuhamasisha asasi nyingine za kiraia kufanya na kuratibu maandamano kama hayo ya CHADEMA kwa ajili tu ya kupinga kuendelea kwa Bunge Maalumu la Katiba.Tunawaambia watanzania wenzetu kuwa tumekerwa na kusononeshwa sana na kauli ya kibabe ya kiongozi huyu wa CHADEMA ya kuhamasisha vurugu ambazo tumezishuhudia zikisambaratisha umoja wa nchi nyingina kuwa chanzo cha vita vya wenyewekwa wenyewe ambavyo huwa haviishi na hatimaye kuendelea kulipakazia Bara la Afrika kuwa halijastaarabika na siasa za kidemokrasia. Tulimsikia akiahidi maandamano bila kikomo kwa kibali cha polisi au bila kibali cha polisi mbele ya wajumbe ambao wengine sio watanzania. Ndugu watanzania wenzetu, kauli kama hii haiwezi kusemwa hata na Rais yeyote ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu anaeongoza kwa kufuata misingi ya sheria na utawala bora, je Mh. Mbowe anapata wapi uhalali na ujasiri huo? Maana Rais na Amiri Jeshi Mkuu ambae ni dikteta anaweza kusema lakini yule anaetawala kwa misingi ya sheria, katiba na utawala bora kamwe hawezi kusema kauli kama hizo. Maneno aliyoyasema Mh. Mbowe amejivalisha madaraka zaidi hata ya yale ya Rais wetu ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama. Lakini kwa mtazamo wetu ni kuwa Mh. Mbowe amejivalisha UDIKTETA ambao unatakiwa kulaaniwa na kila mtanzania aliyeko ndani na nje ya nchi hii. Uzito wa kauli zake haubebeki na mtu yeyote kwenyetaifa hili. Hatuna shaka kuwa ametoa kauli mbaya sana kuliko zote za kisiasaambazo zimewahi kusemwa majukwaani. Watanzania kwa ujumla wetu na makundi yetu tukikaa kimya bila ya kuzilaani na kuzikemea vikali kauli zake, tutakuwa hatujitendei haki sisi wenyewe na pia hatutavitendea haki vizazi vijavyo vya nchi yetu.Ndugu zetu watanzania, kama ambavyo yeye mwenyewe alisema kabla ya kutoa amri kwa watu kuandamana kuwa anaamini watanzania wapo tayari kufanya mageuzi ili chama chake kingie IKULU ya Magogoni. Hayo yatafanikiwa endapo tu vijana wataacha uoga, maneno ambayo yanaashiria kutaka kuchukua uongozi kwa nguvu bila kufuata misingi ya kidemokrasia inayosimamiwa na serikali iliyo madarakani.Sisi umoja wa vijana wazalendo wa vyuo vya elimu ya juu Dar es Salaam tunasema kuwa uzito na ubaya wa kauli hizi unaonesha wazi kuwa Mh. Freeman Mbowe hafai kupewa dhamana ya kuwa Rais wa nchi na Amiri Jeshi Mkuu wa vikosi vya ulinzi na usalama na pia amedhihirisha kuwa CHADEMA haina sifa ya kuiongoza nchi hii kwa sasa kwa kufuata misingi ya demokrasia na kudumisha amani, utulivu na mshikamano wa watanzania kwa lengo la kudumisha umoja, na muungano wetu.Tunaomba watanzania mkumbuke na mtilie maanani kuwa, Mh. Freeman Mbowe katoa kauli hizi akiwa raia tu wa kawaida. Je itakuwaje akiwa Rais wa nchi na Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vyetu vya Ulinzi na Usalama wa nchi hii? Kwa maoni yetu ni kuwa kwa upeona mtazamo wa akili yake hakuna atakaebaki salama ndani ya nchi hii kwa kuwa atatuingiza kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe na pia atatuingiza kwenye vita na nchi majirani. Hafai, hafai, hafai hata mara moja kuwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu. Ndugu watanzaia, hivi ni mtu gani anaeweza kuishi kwa amani na viongozi kama Mbowe na wenzake wanaotumia ubabe kwenye maisha yakawaida ya kila siku? Na hapa ndipo wanatuthibitishia kuwa Mh. Freeman Mbowe na Kikundi cha viongozi wa chama chake wote karibu wameshindwa kuzichunga na kuziweka pamoja familia zao na hatimaye zimesambaratikakwa ubabehuo huo, hivyo hawataweza kutuongoza na kutuweka pamoja watanzania ili tuishi kwa amani.Ndugu watanzania wenzetu tumebaini kuwa Mh. Freeman Mbowe na viongozi wenzake wa CHADEMA wanatumia maandamano na damu za watanzania kutafuta fedha kwa wafadhili wao ambao hawaitakii mema nchi yetu. Wakiaandaa maandamano, wanapiga picha na kuwapelekea wafadhili wao, wanapatafedha, wanajenga majumba na kununua magari ya kifahari na kusafiri ulaya, marekani na familia zisizo rasmikwa kujificha kwenye pazia la DEMOKRASIA huku watanzania wakiendelea kuathirika na maandamano. Hapo ndugu watanzania hakuna DEMOKRASIA bali tunaona DOMO-KRASIA na BONGO-KRASIA, yaani wanatumia ulimi na akilindogo za kitoto kujinufaisha na familia zisizo rasmi kwa siasa za ulaghai, ghilba, fitina, majungu, choyo, chuki, usanii wa kisiasa na uhaini alioutangaza Mh. Mbowe.Ndugu zetu watanzania, fahamuni kuwa Mh. Freeman Mbowe, Dk. Wilbroad Slaa, Tundu Lissu, Godless Lema, Mchungaji Peter Msigwa, Hezekiah Wenje na wengine wana familia. Swali je mmeshawahi kuwaona wake, watoto, na ndugu zao wa karibu kwenye maandamano yoyote yale waliyowahi kuyaandaa? Siku zote huwaambia watu wao hao bakini majumbani mtadhurika. Pale damu za watanzania zinapomwagika kwenye maandamano baadae huwa wanajifungia na kushangilia ushindi mkubwa wa kuvuna mabilioni ya fedha za kigeni, kwa kuwa huwa wanapiga picha matukio hayo na kwenda kuonesha wafadhili wao kwa taswira kwamba demokrasia inanyanyaswa. Wanakinga mabilioni ya fedha za kigeni wanatia kwenye akaunti zao, wanagawana, na mambo yao yanaenda sawasawa, huku watanzania wengine wakiwa wana vilio vya kupoteza ndugu na baba zao, waume, wake, wapenzi/wachumba, na watoto wao na kadhalika. Swali kwa nini hawaoni umuhimu wa kujali utu, ubinadamu na uhai wa watanzania wengine?Sisi umoja wa vijana wazalendo wa vyuo vya elimu ya juu Dar es Salaam tunapenda kuwahakikishia kuwa thamani ya maisha ya watanzania wote au hata kwa mtanzania mmoja nikubwa sana kuliko hiyo katiba mpya wanayoidai. Tunawaomba watanzania wenzetu msikubali kufanywa kama mbuzi wa kafara na watu wenye tamaa, pupa, ulevi, na uroho wa madaraka kama hawa akina Mbowe na kundi lake. Tusijiendee tu kama kuku aliekatwa kichwa halafu akaachiwa atembee, na tusishikiwe akili zetu kama za mbayuwayu kwani “Akili za Kushikiwa, ongeza na zako”. Tuwakataeni wanasiasa uchwara waliofilisika kihoja na kutaka kuwatumia ili kujinufaisha. Wanataka kutupeleka wapi? Ni dhambi isiyosameheka kulitumbukiza taifa hili katika machafuko yenye majuto makubwa kama ya Misri, Syria, Afrika ya kati, Libya, Sudan ya Kusini na kwingineko. Tusikubali watupeleke huko, waacheni waende wenyewe kama wanaweza. kwani nchi yetu ina mgogoro wa kisiasa?!!!!! Waulizeni wanataka nini?Ndugu watanzania wenzetu, tunaomba mjue kwenye nchi hizo hizo zenye demokrasia pevu watu wa aina ya Mh. Freeman Mbowe (hasa kwa kauli zake alizozitoa juzi tarehe 14.09.2014) wanaotaka kuvuruga na kuvunja misingi mikuu ya utaifa wao (core values) kama vile amani, usalama na umoja huwa hawavumiliwihata kidogo.Sisi umoja wa vijana wazalendo wa vyuo vya elimu ya juu Dar es Salaam tunaviomba vyombo vyetu vya dola visizivumilie kauli kama hizi zilizotolewa na Mh. Freeman Mbowe hata mara moja. Kwani vyombo vya dola vina dhamana ya kulinda, kutunza na kuendeleza amani na utulivu wa nchi yetu. Umoja wetu, kwa heshima na taadhima kubwa, tunaviomba vyombo hivi kumchukulia hatua kali za kisheria Mh. Mbowe kwa kauli hii ya kutishia uvunjifu wa amani kabla hajaiingiza nchi yetu kwenye machafuko ya kisiasa.Sisi umoja wa vijana wazalendo wa vyuo vya elimu ya juu Dar es Salaam hatutaki kuona vijana wenzetu na watanzania wote kwa ujumla wakiathirika kwa ujinga huo wa maandamano yanayofanywa mradi wa kutafuta fedha. Kwani maandamano hayo yatawaathiri wanavyuo wa Dar es Salaam pamoja na kuathiri shughuli nyingine za kiuchumi, na kijamii za wananchi wa kawaida. Kwa nini shughuli zetu na za wananchi zisimame kwa sababu tu ya machafuko ili Mh. Mbowe apate picha za kwenda kuuza huko kwa wafadhili wao? Sisi umoja wa vijana wazalendo wa vyuo vya elimu ya juu Dar es Salaam tulisikiliza na kutazama hotubaile kwa umakini wa hali ya juu, tunapenda kuwathibitishiakuwa hotuba ile haikuwa ya kisomi, ilikuwa haijengi chama chake wala ilikuwa haijengi nchi yetu isipokuwa ilikuwa yakibabe, ilikuwa ya kejeli, ilikuwa ya kichochezi iliyolenga kuvunja misingi ya amani na utulivu wa nchi yetu. Ni matumaini yetu kuwa hata kwa mwanafunzi wa shule ya msingi hawezi kujifunza kitu chochote cha maana kutoka kwenye hotuba ile. Hotuba ya Mh. Mbowe haiwezi kutusaidia kujenga taifa lenye dira kwavizazi vijavyo.Mwisho, Sisi kama umoja wa vijana wazalendo wa vyuo vya elimu ya juu Dar es Salaam, tunawataka watanzania wenzetu mzipime na kuzitafakari kwa makini kauli za Mh. Mbowe, na kujiuliza je anafaa kuwa kiongozi wa nchi hii?Asanteni kwa kutusikiliza,

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika

Imesomwa na Mussa Omari, Mwanafunzi OUT, kwa niaba ya umoja wa vijana wazalendo wa Vyuo vya elimu ya juu Dar es SalaamTarehe 17.09.2014
Mbele ya Mwandishi wa MTANZANIA JITAMBUE....

Jumatano, 17 Septemba 2014

Ajali imetokea hapa daraja la kifaru
Himekuwa ya Ajabu ajabu ni Bus moja la Kilenga limegonga nyuma ya Gari lingine la Kilenga majira ya 10:34 am..
Ila kutoka na Trafiki kufika na kuangalia hali iko nzuri kwa Abiria wakapima na kuwaruhusu wafike Mjini Moshi....
Mtoa Habari akiongea na MTANZANIA JITAMBUE:-Amesema anawaomba Madreva wa Mabus wawe makini katika uendeshaji wa mabus kwani hii Ajali ni ya kizembe Mno...Ila anashukuru kwani hakuna Madhara yaliyojitokeza

Tumeruhusi niko ndani kwenye bus
tayari ndo tumeruhusiwa tunaondoka

Wenu Mtoa Habari Mwkt Wazalendo Mkoa Shinyanga-Charles Mbaga
Ni mmoja wapo wa Abiria katika Moja wapo ya BUS LA KILENGA

Jumanne, 16 Septemba 2014


Ni mfabiashara maarufu mjn moshi anaitwa Yesus pafyum au Sharif Mussa msanii maarufu na mchungaji ndg Emanuely Mgaya almaarufu Masanja mkandamizaji a.k.a mchungaji mtarajiwa baada ya kuomba kwa muda mrefu,kufunga na kusali atimaye akutana na Yesus laivu

Mtoa habari  MTAN ZANIA JITAMBUE-Jerry Nzowa

Traffic Agongwa na gari aina DCM leo akiwa kazini,point mbagala rangi 3,aliwahisha Temeke Hospital na baadae kuhamishiwa Muhimbili. Baada ya kufuatilia kwa ndani zaidi aliepata ajali ni WP 2806 Cpl Riziki, chanzo cha habari kinasema hali yke c mbaya sana.
Mleta habari wenu MTANZANIA JITAMBUE-DAR

Huyu binti bana alikuwa anaishi nahuyo mama hapo nyumbani kwa miaka mitano akapata ujauzito mama mwenye nyumba akamrudisha nyumbani kwao , baada ya muda kidogo yule binti akampigia tena yule maama simu mama maisha ni magummu, kwa kuwa yule mama alikuwa anampenda akamwambiia rudi tuu nitakulea wewe na mtoto wako, basi ni wiki tu tangu arudi hapo nyumbani jana alianguka jikoni watu kwenda kumuangalia wakagundua amekunywa pombe,
Leo akashindwa kabisa kufanya kazi na saa saba mchana wa leo ndo akachukua maamuzi hayo
Huyo ndo mama mwenye
Nyumba Amemkuta Bafuni kajinyonga..
Huyu ni mtoto ambaye hyo dada alirudi naye kwa mama RAZI
Tukio limetokea kata ya pasua leo mchana..
Akiongea na MTANZANIA JITAMBUE amesema ameshitushwa sana na kusema hii hatua aliyochukua si nzuri na pia hakujua kilicho msibu huyu Mfanyakazi wake na pia angepaswa kunieleza kilicho msibu ila naona Shetan alimpitia..Mwenyezi Mungu amsamehee.....!!!
Wenu Mtanzania Jitambue-Jerry Nzowa

Jumapili, 14 Septemba 2014

Kutokana na kipigo kilitokea kwa YANGA KUWAPIGA AZAM BILA HUTUMA kwa sasa habari ya Mjini imekuwa nu JAJA....
WATOTO WAMJINI WANASEMA MWISHO UZEE CHALINZE MJINI BABY...
NDIYO IMEKUWA---OKWI MWISHO CHALINZE MJINI KILA MTU JAJA...HII NDIYO HABARI YA MJINI KWA SASA..

MAHOJIANO HAYA YALIKUWA MTANZANIA JITAMBUE NA MSHABIKI WA YANGA MAARUFU ALLY SIX ambaye alitoa mpya hii jana baada ya kumalizika kwa mpira wa AZAM NA YANGA...
Wenu Mtanzania Jitambu  kutoka Jiji Dar

Steve Yanga ahamia Azam .
Yule Shabiki no 1 wa Yanga ahamia Rasmi Azam.
Steve ambaye alijipatia Umaarufu wkt wa mechi ya Yanga na Simba baada ya Yanga Kufungwa Goli 5 ndio akalia kwa Uchungu .
Leo ameonekana najezi ya Azam.
Baada Ya Mtanzania Jitambua Kumuhoji akadai amehama baada yakupata Fedhea siku ya Kumpokea Maximo Airport eti Mashabiki wenzake  wa Yanga walitaka kumpgia kisa Kuonekana Kushiriki Shindano la Kwetu House lililokua Likiendeshwa na Azam Tv. Hata hvyo Steve alikimbilia Wanapoondokea Wasafiri akaokolewa na Askari wa Doria Uwanja wa Ndege

Sijui leo baada ya kufungwa 3 na Yanga atalia kwa mapenzi mapya ya AZAM????? SOKA LA BONGO HILI

YANGA VS AZAM FC.
YANGA MSHINDI 3 -0
JAJA KAFUNGA MAGOLI 2 NA MSUVA KAFUNGA 1-14 minutes ago ·
Mpira umemalizika, Young Africans 3 - 0 Azam
FC
Jaja DAKIKA YA 58. DAKIKA YA 66
Msuva DAKIKA YA 88
Yanga 3 vs Azam fc 0
Mashindano ya ngao ya
La tatu MSUVA ndio mfungaji....
YANGA WALISEMA LEO NI USHINDI NI 100% KWA KWELI HICHI KIPIGO NI CHA MBWA MWIZI....KWANI WASHABIKI WA AZAM AWAAMINI KILICHOKEA UWANJANI LEO....

WACHEZAJI KAMA WAMELOA LEO KWELI VIJANA WA YANGA WAMEIVA NA HUKU MWENYEKITI WAO MANJI AMETOA DAU NENE KWA WACHEZAJI WA YANGA....

WENU MTANZANIA JITAMBUE KUTOKA UWANJA WA TAIFA.....

[23:29, 13/09/2014] WILLIAM SWAI ABDUL KIGAMBONI:
Alikupo mh six,farida,fety me mishi rusma,filbt sumaye njano 5 iren asmine hamxa majuto naisi ndo hao kaka

[07:07, 14/09/2014] WILLIAM SWAI ABDUL KIGAMBONI:
MAREHEMU Mwalim Dainess Swai

[07:19, 14/09/2014] WILLIAM SWAI ABDUL KIGAMBONI: Ndugu Zangu jamaa na marafiki zangu napenda kutoa shukran zangu za dhati kubwa kwa ushirikiano nilioupata toka kwa ongea na sumaye mzalendo toka dada yangu anaumwa mwalim dainess swai hadi mauti inamfika ongea na sumaye mxalendo wamenipa msaada mkubwa sana toka mwanzo hadi mwisho wa safari ya dada yangu walikuja na kunifariji na kushughulikia taratibu zote za mazishi napenda kusema asante sana ongea na sumaye mxalendo sina cha kuwalipa ila mungu atawalipa na pia natoa shukran zangu za dhati kwa mhe sumaye mzalendo kwa kuwa pamoja nasi toka mwanxo hadi mwisho nashukuru sana mhe waxiri mkuu mstaafu kwa moyo wako na kuwa nasi mwanxo hadi mwisho asanteni sana wana ongea na sumaye mzalendo pamoja tunaweza amani na upendo.Nashukuru sana WAZALENDO TANZANIA KWA KUNIPA USHIRIKIANO MKUBWA NA KUONYESHA UPENDO TOKA DADA YANGU ANAUMWA MPK ALITOTUTOKA WALIKUWA NAMI NA PIA NIFIKISHE SHUKURANI ZANGU KWA MWENYEKITI WAZALENDO TANZANIA NDG.MRINDOKO BABU MWIDADI DAUDI kwa Kuweza kutuonganisha sote na kuwa ndugu Moja na Umoja wetu naomba kwa Mungu uzidi kuongezeka...
Pia napenda kupeleka Shukurani za Pekee kwa Mhe.FREDERICK SUMAYE-WAZIRI MKUU MSTAAFU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWA KUWA KARIBU NASI WAZALENDO WA TANZANIA MWENYEZI MUNGU AMBARIKI SANA NA AMJAALIE MEMA
WENU ABDUL 'WILLIAM'SWAI -KIGAMBONI........
YAMERIPOTIWA NA MTANZANIA JITAMBUE KUTOKA KIGAMBONI

Jumamosi, 13 Septemba 2014

Leo nimetimiza ahadi ya ombi la kuwapatia SEMINA ya UJASIRIAMALI wananchi wenzangu wa kata niliyozaliwa ya Mchikichini Wilayani ILALA. Namshukuru sana Mhe. Mwenyekiti wa CCM WIlaya ya ILALA Bw. Assah Simba kwa kutufungulia Semina hii pamoja na Bw. Paul Mashauri kwa kutoa mada ya Ujasiriamali kwa Vijana! Nawashukuru sana CCM kata ya Mchikichini kwa ushirikiano wao!

ILALA ni yote sote!
Tunaamini kuwa Tukipata viongozi vijana km MRISHO GAMBO ni Faida kwa vijana kwani anajitolea kwa ajili ya Wilaya atokako naamini anapanda kwao na c mkataa kwao...Hii semina imewafungu mno wana ILALA...

WENU MLETA HABARI MTANZANIA JITAMBUO KUTOKA JIJINI DAR..

Kumbukumbu la Blogu

Inaendeshwa na Blogger.

Machapisho Maarufu

Machapisho ya Karibuni

Recent Posts Widget