Alhamisi, 13 Novemba 2014

Mjumbe wa Kamati kuu ya ccm taifa Dkt. Emmanuel Nchimbi akizungumza mbele ya viongozi wa ccm wilaya ya moshi vijijini


Katika tukio la jana tarehe 12/11/2014 la ziara ya mjumbe wa kamati kuu ya ccm taifa na mlezi wa ccm mkoa wa kilimanjaro hakusita kumpongeza Katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya moshi vjijijini MIRIAM SANGIT KAAYA kwa kazi kubwa na juhudi zake za kukijenga chama cha mapinduzi.

Aliyasema hayo mbele ya makatibu kata wote wa chama cha mapinduzi kwa upande wa jimbo la vunjo. Mlezi huyo alisema ".. kwa kuwa niliwapa nafasi ya kusema lolote ili mtoe dukuku zenu, nimefurahishwa kwa namna mnavyomsemea vizuri katibu wenu wa wilaya. Hivyo, mimi nampa alama za asilimia mia moja 100%."

Wakati akiyasema hayo makatibu kata walimshangilia Dkt. Emmanuel Nchimbi kwa alama alizompa katibu wao wa wilaya.

Mlezi wa CCM mkoa wa kilimanjaro Dkt. Nchimbi aliwataka viongozi hao kushikamana na kutokubali kushushwa thamani yao kwa kuhongwa pesa na wasaka madaraka.



Katibu wa CCM wilaya ya moshi vijijini  Miriama Kaaya na Dkt. Emmanuel Nchimbi wakiwa katika mkutano wa hadhara


 Wakati huo huo, Mlezi wa CCM mkoa wa kilimanjaro hakusita kumsifia tena Katibu huyo wa CCM wilaya ya moshi vijijini katika mkutano wa hadhara. Hayo aliyasema baada ya mapokezi makubwa aliyoyapata , anasema".. wilaya ya moshi vijijini ndio wilaya pekee niliyopata mapokezi makubwa kiasi hichi, tumefurahi sana na nina waahidi kurudi tena katika kijiji hiki cha mikocheni.."


0 maoni:

Chapisha Maoni

Kumbukumbu la Blogu

Inaendeshwa na Blogger.

Machapisho Maarufu

Machapisho ya Karibuni

Recent Posts Widget