Jumamosi, 29 Novemba 2014
Chama cha mapinduzi wilaya ya Monduli mkoani Arusha kimepita bila kupingwa kuelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa vijiji 57 kati ya vijiji 68.
Pia, imepita bila kupingwa katika vitongoji 206 kati ya vitongoji 250. Hali hii ni ishara ya kwamba wilayani Monduli chama cha mapinduzi kimeweza kutekeleza ilani yake kwa kiwango kikubwa kiasi cha kuendelea kuaminiwa na wananchi wa wilayani hapo.
Kwa taarifa za uhakika kuna uwezekano mkubwa kwa vijiji na vitongoji vilivyobakia kuchukuliwa na chama cha mapinduzi.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
0 maoni:
Chapisha Maoni