Ijumaa Ethiopia ilitangaza kujitoa kuwa mwenyeji wa michuano hiyo iliyokuwa imepangwa kuanza Septemba 24 hadi Desemba 9
BARAZA la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA, limeiomba Sudan kuandaa michuano ya Kombe la Chalenji inayotarajiwa kuanza
mwishoni mwa mwezi huu baada ya Ethiopia kujitoa, Goal imegundua.
Sudan ilitinga hatua ya fainali katika michuano iliyofanyaka Kenya
mwaka jana na wenyeji Harambee Stars’kuibuka na ushindi wa mabao 2-0
mfungaji akiwa Allan Wanga ambaye kwa sasa anaichezea timu ya El
Marreikh ya Sudan.
Kwa mujibu wa Mtandao wa Futaa.com umemnukuu Katibu Mkuu wa CECAFA,
Nicholas Musonye amethibitisha wanasubiri majibu ya ombi lao kutoka kwa
shirikisho la soka la Sudan ambayo wanatarajia kuyapata ndani ya wiki
hii.
Musonye amesema hakuna nafasi ya nchi kutuma maombi ya kuwa mwenyeji wa michuano hiyo baada ya Ethiopia kujitoa, hata hivo.
“Tumeiomba Sudan kuwa mwenyeji. Tumewaandikia barua na sasa
tunasubuiri majibu, na tunatarajia watatujibu kabla ya kufika mwishoni
mwa wiki hii.
Ijumaa Ethiopia ilitangaza kujitoa kuwa mwenyeji wa michuano hiyo
iliyokuwa imepangwa kuanza Septemba
24 hadi Desemba 9, mwaka huu kwa
sababu mbalimbali ambazo Musonye hakuwa tayari kuziweka wazi.
Katibu mkuu wa CECAFA
0 maoni:
Chapisha Maoni