Alhamisi, 13 Novemba 2014



Mjumbe wa kamati kuu ya CCM taifa Dkt. Emmanuel Nchimbi apokea wanachama wapya zaidi ya mia moja. Afanya zoezi hilo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya TPC katika kijiji cha Mikocheni.

Hii ni kata inayoongozwa na diwani wa chadema Ndg. Rodgers, katika hali isiyo kuwa ya kawaida wananchi hao walimlalamikia Diwani huyo wa chadema wa kata yao kwa ahadi za uongo alizowahadaa kipindi cha uchaguzi mkuu 2010.

Baadhi ya wananchi hao walisikika wakisema " huyu diwani rodgers ni muongo sana, alituahidi endapo tutampa ridhaa atahakikisha anafungua uzio wa kiwanda cha TPC ili wapate sehemu za malisho, sasa ni miaka minne jambo hili ameshindwa kututekelezea. Sisi tunaamini ni CCM pekee ndio ina uwezo huo na ndio maana LWAIGONANI wetu amebariki sisi kuichagua CCM kuanzia sasa. Huyu RODGERS hatutaki kumuona tena akija huku.."

Mlezi wa CCM mkoa wa kilimanjaro Ndg. Emmanuel Nchimbi amewataka wananchi hao safari hii wasifanye makosa tena, upinzani haufai hata kidogo mana wao wanachojua ni kupinga tu.



Mlezi wa CCM mkoa wa kilimanjaro akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Mikocheni
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa kilimanjaro akihutubia wananchi wa kijiji hicho


Katibu wa CCM Mkoa wa kilimanjaro akifafanua jambo katika mkutano huo
Katibu wa CCM wilaya ya moshi vijijini akitoa akihutubia wananchi wa kijiji cha mikocheni


Katibu mwenezi wa CCM wilaya ya Moshi vijijini Ndg. Jamal Husein akitoa utambulisho wa viongozi

0 maoni:

Chapisha Maoni

Kumbukumbu la Blogu

Inaendeshwa na Blogger.

Machapisho Maarufu

Machapisho ya Karibuni

Recent Posts Widget