Ijumaa, 21 Novemba 2014

Scott alichukua usukani baada ya aliyekuwa Rais Michael Sata kufariki

Chama tawala nchini Zambia (PF) kimemtimua kaimu rais wa nchi hiyo Guys Scott kutoka chamani na kuvunja utaratibu wa katiba.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa msemaji wa chama hicho.

''Amekuwa akiwaajiri na kuwafuta watu kazi ovyo na pia bila ya kushauriana na kamati kuu ya chama,'' amesema Malozo Sichone.

Bwana
Scott, ambaye licha ya hatua hiyo ataendelea kuwa mwanachama wa chama
hicho, ataendelea kuhudumu kama kaimu rais hadi uchaguzi utakapofanyika
tarehe 20 Januari.

Scott aliteuliwa kuwa kaimu rais kufuatia kifo cha hayati Rais Michael Sata aliyefariki mwezi jana.

0 maoni:

Chapisha Maoni

Kumbukumbu la Blogu

Inaendeshwa na Blogger.

Machapisho Maarufu

Machapisho ya Karibuni

Recent Posts Widget