Jumapili, 8 Februari 2015

Innocent Melleck Shirima akihutubia mamia ya wanavunjo

Innocent Melleck ni kijana mzaliwa Marangu wilayani moshi vijijini mkoani Kilimanjaro lakini pia ni naibu kamanda wa vijana wilaya ya moshi vijijini kupitia UVCCM.
Kwa kipindi kirefu sana kijana huyu amekuwa katika hali ya kutoridhishwa na maendeleo ya jimbo la vunjo, hali ambayo imemlazimu kufanya jitihada za kuweza kusaidiana na wananchi wa jimbo la vunjo kuhakikisha wanaenda kasi ya kuwaletea maendeleo wanavunjo kwa ujumla wao.
Kijana huyo anaamini kuwa kasi ya maendeleo ya vunjo haiendani na uhalisia wa rasilimali ambazo zipo au zilizozunguka eneo hilo. Amenukuliwa akisema" Tukitazama uhalisia wa maendeleo ya jimbo la vunjo na rasilimali ambazo zipo haziwiani hata kidogo. Tuna rasilimali nyingi na za kipekee kabisa kwa mfano huu mlima kilimanjaro na rasilimali ardhi tuliyonayo hivi kunasababu gani ya maendeleo kutoenda kwa kasi kiasi cha kuridhisha?"
Mount Kilimanjaro
Mlima Kilimanjaro

Innocent Melleck anasema rasilimali hizi zinatosha kwa kiasi kikubwa sana kuifanya vunjo kuwa na maendeleo makubwa sana bila utegemezi wa serikali kuu. Kupitia mlima huu kuna uwekezaji mkubwa sana ambao haumfaidishi moja kwa moja mkazi wa eneo husika bali ni serikali kuu ambayo mahitaji kiasi kikubwa hupelekwa maeneo mengine ambayo kwa namna moja ama nyingine wawakilishi wao wana nguvu ya kujenga hoja na ushawishi bungeni.
Watalii wakipanda Mlima kilimanjaro
Kijana huyu anasema kuwa vunjo inapaswa kuwa mahala kwa mfano wa kuigwa mahala pengine hasa kwa kuweza kunufaika na rasilimali hizo muhimu ardhi na mlima kilimanjaro lakini hali iko tofauti sana na ilivyotarajiwa. Anasema kuwa" Ni aibu sana kwa jamii ya wanavunjo kulalamika kuwa kuna tatizo la barabara, maji, umeme, hospitali na zahanati pamoja na pembejeo za wakulima. Milima wa kilimanjaro unaingiza mapato kwa kiasi kikubwa sana. Sote ni mashahidi ni kwa kiasi gani watalii wanavyomiminika kuja kutizama na kuupanda mlima huu wa kilimanjaro, leo kuwa na changamoto za aina hii ndio jambo ambalo limenisukuma sana kuangalia kwa namna gani kuweza kubadili mfumo mzima wa uwakilishi wa eneo letu la vunjo pamoja kuhakikisha tunaleta maendeleo kwa kasi inayoridhisha"
Ramani ya Mlima Kilimanjaro

Innocent Melleck ameawataka wanavunjo wasikate tamaa kupigania maslahi yao lakini kwanza ni lazima kuhakikisha kuwa wanafanya mabadiliko ya uwakilishi wao, mana kichooneka hapa ni suala la uwakilishi ndio tatizo. Tusikubali kurudia makosa ambayo yalitugharimu sana mwaka 1995-2000 awamu ya aliyekuwa mbunge kipindi hicho MBATIA, 2000-2005 na 2010-2015 makosa haya ndiyo ambayo yametufanya leo hii tunazungumza mengi kuhusu vunjo yetu kwanini kasi ya maendeleo ipo chini kiasi cha kuhatarisha maisha ya vijana wengi kwa kukosa ajira na wazee kukosa malezi toka kwa vijana wao ambao ndio nguvu kazi wanayoitegemea.
Mabadiliko kufanyika si jambo la kushauriana wala la kusita, hili ni jambo la ulazima kuliko mambo mengine yoyote yale. Jambo hili linahitaji muda na maamuzi sahih. Mwaka huu ni kipindi cha uchgauzi mkuu wa serikali kwa ngazi ya udiwani, ubunge na Uraisi ni kipindi ambacho wanavunjo wanapaswa kufanya maamuzi ambayo hawatakuja kuyajutia kwa kipindi kingine cha miaka mitano ijayo.
Innocent Melleck amewataka wanavunjo wote bila kujali itakidai zao kumchagua kiongozi ambaye atakuwa na uwezo wa kushawishi serikali kuu kwa hoja ili aweze kuwaletea maendeleo ya kasi katika jimbo la vunjo.
Anaendelea kusema kuwa ni kweli watakuja wengi sana na vyama vyao kuomba ridhaa kwenu, lakini pia wapo ambao watakuja kwenu bila kuona haya kwa kujiuliza kipindi ambacho walipewa ridhaa na sisi wanavunjo waliitumika vipi na kwanini hali ni mbaya na sasa wana mbinu gani mpya ya kuwasaidia wanavunjo ili waweze kuwaamini kwa mara nyingine. Watu wa aina hiyo tuwaogope kama ugonjwa wa ukoma.
Kwa upande wake ameweka dhamira ya kweli kuja kufanya mapinduzi makubwa sana ya kimaendeleo na ana imani wanavunjo kwa umoja wao watamuunga mkono katika harakati hizo. Na ameamua kufanya hivyo baada ya maombi mengi toka kwa vijana na wazee wa jimbo la vunjo lakini pia amefarijika kuona wapo tayari kumchukulia fomu za kuomba ridhaa kwa gharama zao wenyewe.

Mwisho amewataka wanasiasa wote ambao wanadhamira ya kutaka kuomba ridhaa kwa wanavunjo kuweza kujiuliza mara mbili kama anatosha au la, lakini pia wamuogope mungu kwa matendo yao dhidi ya wananchi wa vunjo.




0 maoni:

Chapisha Maoni

Inaendeshwa na Blogger.

Machapisho Maarufu

Machapisho ya Karibuni

Recent Posts Widget