Mtanzania Jitambue
facebook tweeter google linked in you tube rss
  • Home
  • Biashara
  • Burudani
    • Michezo
  • Siasa
  • Breaking News
    • Tanzania
      • Serikalini
  • Afya
  • Wazalendo
  • Ulimwenguni

Jumanne, 10 Februari 2015

  • 11:54
  • Mtanzania Jitambue
  • No comments

UN YAIPA LAWAMA TANZANIA KWA HALI ILIVYO DRC


Hali ilivyo DRC
Umoja wa mataifa imezituhumu serikali za Tanzania na Burundi kuhusiana na hali katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Ripoti
mpya ya kundi la wataalamu wa umoja huo kuhusu Congo, imeituhumu
Tanzania kwa kuwaruhusu viongozi wa kundi la waasi wa FDLR kuandaa
mikutano nchini humo.

Imeeleza pia kwamba wanajeshi wa Burundi wametekeleza unyanyasaji wa kingono.

Taarifa
hiyo ya Umoja wa mataifa inasema kuwa tangu mwaka wa 2013, viongozi wa
FDLR na baadhi ya washirika wao wa kisiasa kutoka Ulaya wamekuwa
wakikutana nchini Tanzania.

Majeshi ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo wakipambana na waasi
Lakini wachunguzi wa Umoja wa
mataifa walipoiuliza serikali ya Tanzania kujibu madai haya ilikanusha
kabisa kuwahi kuakaribisha mikutano yoyote ya waasi ndani ya ardhi yake
na kuongeza kuwa hakujawahi kuwa na mazungumzo yoyote kati ya majeshi
yake na wapiganaji wa FDLR.

Umoja wamataifa umesema pia kuwa una
ushahidi wa pesa zilizotumwa kutoka taifa hilo la Afrika Mashariki kwa
baadhi ya washukiwa nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Ripoti
hiyo pia imelaumu kundi hilo la FDLR kwa kutotekeleza ahadi yao ya
kusalimisha silaha na kujisalimisha kufikia Januari mwaka huu.

UN
inasema kuwa FDLR wamewatuma wazee waliodhoofika kiafya pekee
kujisalimisha na kukabidhi silaha chache sana ambazo zina hitilafu.

Kundi
la FDLR, liliundwa mwaka wa 2000 na wahutu waliokimbilia Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo kufuatia mauaji ya kimbari ya Rwanda.

Wapiganaji wa kundi la FDLR
Kundi hilo linapinga utawala wa kitutsi na ushawishi wake katika eneo la maziwa makuu.

Rwanda
imekuwa ikitazama kundi hilo kama tisho kubwa kwa utawala uliopo na kwa
kauli moja na Umoja wa mataifa imekuwa ikishinikiza kupokonywa silaha
kwa wapiganaji wake.

Ripoti hiyo pia imetoa madai ya ubakaji na unyanyasaji wa kimapenzi unaofanywa na wanajeshi wa Burundi katika Kivu ya Kusini .

Wataalamu
hao wa Umoja wa mataifa wamependekeza serikali za Burundi na Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo zifanyie uchunguzi madai hayo ambayo wanasisitiza
yalifanywa namajeshiya Burundi pamoja na kikundi cha vijana wapiganaji
wajulikanao kama Imbonerakure.



@bbc news


Tuma Hii kwa Barua pepeBlogu Hii!Chapisha kwenye XShiriki kwenye Facebook
← Chapisho Jipya Taarifa za zamani → Nyumbani

0 maoni:

Chapisha Maoni

Jisajili kwenye: Chapisha Maoni (Atom)

Lebo

  • Biashara
  • Michezo
  • Serikalini
  • Siasa
  • Tanzania
  • Ulimwenguni
  • UVCCM
  • Wazalendo

Kumbukumbu la Blogu

  • ►  2024 (2)
    • ►  Julai (2)
  • ▼  2015 (22)
    • ►  Septemba (1)
    • ►  Aprili (2)
    • ►  Machi (5)
    • ▼  Februari (10)
      • WAFANYABIASHARA NDOGO NDOGO WAMUOMBA KADA WA CCM D...
      • MH. MREMA:-"MBATIA HANA UWEZO WA KUWA MBUNGE WA JI...
      • KIJANA INNOCENT MELLECK SHIRIMA AWATAHADHARISHA WA...
      • UN YAIPA LAWAMA TANZANIA KWA HALI ILIVYO DRC
      • MHESHIMIWA Rais Prof.JAKAYA KIKWETE AFUNGUA RASMI ...
      • INNOCENT MELLECK SHIRIMA KIJANA ALIYEPANIA KURUDIS...
      • PICHA ZA MATUKIO ZA MH. OLIVIA SANARE ALIPOHUDHURI...
      • WAASI WA HOUTH WACHUKUA SERIKALI NCHINI YEMENI
      • UVCCM MOSHI VIJIJINI WATIA FORA MIAKA 38 YA CCM
      • CCM WILAYA YA MOSHI VIJIJINI YAADHIMISHA MIAKA 38 ...
    • ►  Januari (4)
  • ►  2014 (97)
    • ►  Desemba (34)
    • ►  Novemba (27)
    • ►  Oktoba (3)
    • ►  Septemba (33)
Inaendeshwa na Blogger.

Machapisho Maarufu

  • WANANCHI WA MJI MDOGO WA HIMO WAJITOKEZA KWA WINGI KUSHANGILIA USHINDI WA CCM
    Siku ya jana tarehe 21/12/2014 wakazi wa mji mdogo wa Himo wajitokeza kwa wingi sana kusherehekea ushindi wa kishindo wa chama cha mapinduzi...
  • PICHA ZA MATUKIO ZA MH. OLIVIA SANARE ALIPOHUDHURIA MAAZIMISHO YA MIAKA 38 YA CCM MKOANI RUVUMA
    Kada wa ccm Olivia Sanare akiwa na baadhi ya walioshiriki maadhimisho uwanjani   Picha ya kwa pamoja na mh. Olivia Sanare Mh. Oliv...
  • CHIEF MRINDOKO: "MUDA UKIFIKA NITAJIBU MAOMBI YENU YA KUNISHAWISHI KUGOMBEA UBUNGE MOSHI MJINI"
    Leo Jumapili tarehe 12/04/2015, mwenyekiti wa taasisi ya wazalendo Taifa Ndg. Chief Daud Mrindoko ameyasema hayo katika uzinduzi wa Album ya...
  • CCM WILAYA YA MOSHI VIJIJINI YAADHIMISHA MIAKA 38 YA KUZALIWA KWAKE KWA KUWATEMBELEA WAGONJWA HOSPITALI YA KILEMA MKOANI KILIMANJARO
    Viongozi wa chama cha mapinduzi wilaya ya moshi vijijini wakiwasili hospitali ya Kilema Chama cha Mapinduzi wilayani moshi vijijin...
  • break News:MABUS YA KILENGA YAGONGANA ILA YAMEARIBIKA KIDOGO.
    Ajali imetokea hapa daraja la kifaru Himekuwa ya Ajabu ajabu ni Bus moja la Kilenga limegonga nyuma ya Gari lingine la Kilenga majira ya 10...
  • MWENYEKITI UVCCM MKOA WA KILIMANJARO AZINDUA RASMI UVCCM CUP KATA YA MAKUYUNI
    Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kilimanjaro Ndg. Fredrick Mushi akihutubia mashabiki wa soka waliohudhuria uzinduzi huo wa ligi ya UVCCM CUP kat...
  • UTEUZI WA NAFASI ZA UONGOZI KATIKA TAASISI YA WAZALENDO TANZANIA
    TAASISI YA WAZALENDO TANZANIA TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Tarehe 07/12/2014. Mwenyekiti wa Wazalendo Taifa Ndg. Daud Mrindok...
  • DR.SLAA AFUNGUKA UKWELI...UKAWA MASHAKANI
    LIVE UPDATE Kutoka Serena Hotel Ambako Dr. Slaa Anaongea 1.Napenda  kumshukuru  mwenyezi  mungu  kwa  kutujali  uzima. 2. Nimeamua  kujito...
  • HONGERA SUMAYE KWA NISHANI YA BIDII NA UDILIFU KATIKA KUULINDA MUUNGANO
    Ikulu Tar 25 April Mh. FREDERICK TLUWAY SUMAYE aliwakilishwa na mwanaye FRANK F.T.SUMAYE  kumpokelea Nishani .Nishani hiyo ni ya kufan...
  • KADA WA CCM NDG. OLIVER SANARE ASHIRIKI HARAMBEE NA UZINDUZI WA KWAYA KATIKA KANISA LA MAWELA URU WILAYA YA MOSHI VIJIJINI
    Ndg. Oliver Sanare akisema jambo katika harambee ya kanisa la Mawella  Kada wa chama cha Mapinduzi Ndg. Oliver Sanare siku ya jana tar...

Machapisho ya Karibuni

Recent Posts Widget

Kurasa

  • Home

Kunihusu

Mtanzania Jitambue
Tazama wasifu wangu kamili

Sample Text

Copyright © Mtanzania Jitambue | Powered by Blogger
Template Designed by Kanoutechno™
Blogger Templates