Mheshimiwa Rais.Prof.Jakaya Kikwete afungua Jengo la NSSF-KILIMANJARO
NSSF yajenga jengo kubwa sana Mjini Moshi, Mhe.Rais Kikwete amewapongeza sana Mhe.Kabaka-Waziri wa Ajira na Kazi pamoja Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro Mhe.Gama pia walikuwepo Mhe.Mrima-Mbunge wa Vunjo pamoja na Mhe.Chami-Mbunge wa Moshi Vijijin pamoja viongozi wa Vyama vyote akiwemo Mwenyekiti wa CCM MKOA-Ndg.Idd Mwanaweza..
Rais Jakaya aliwapongeza sana wabia wate walioshirikiana na NSSF kutoa maeneo yenu na kujengwa Jengo..
Napenda kuwapongeza sana tena sana Uongozi wa NSSF-Ndg.Ramadhani Dau hongereni sana..Pia mmeweza kufanya jambo zuri ambalo litakuwa mnapata Mikutano pia nimeambiwa kuna Hotel/Ofisi/Sehemu za Biashara kwa hiyo tushukuru kipata kitaongezeka na ajira zitaongezeka pia na kipato kitaongezeka pia, Manspaa ya Moshi mtabidi mpokee maombi ya NSSF ili muweze kuongea vizuri kuweza kupata parking,
Pia TAASISI nyingine nawaombeni mutenge sehemu ya kujenga magorofa, Uwe Meya wa maendeleo siyo Meya wa Mbwembwee tu sasa watu wanataka maeneo ya Kujenga..
Hata kesho picha zikatoka kesho basi wawekezaji watakuja kuwekeza ila Manspaa mkitaka kutanuka ni kutanunikia Moshi Vijijini ila Moshi Vijijini ni Kazi kwani wanapenda Viwamba, Nakumbuka siku moja nikiwa ofisi ya Chama nikiwa makao makuu nilikuwa naratibu wageni kumuona Hayati Mwl.Nyerere:Alikuja Mzee Mmoja hivi akatoa vikambakamba hivi kama Saba (7) hivi na akaniuliza unavijua hivi mwanangu nikasema:Sijui yeye akasema kwenye Eneo hili watoto nimewazalia hapo itakuwaje iwe mjini tena!!
Nashukuru sana kwa wana Moshi na ntakuja kwa ajili ya Ziara ya Serikali kipindi kijacho! Ahsanteni sanaaa
Mwenyekiti wa Bodi ya NSSF amshukuru Rais Prof.Kikwete kwa kuja kufungua Jengo na kuwapa moyo ya kuweza na pia Nasema ILANI YA CCM inatekeleza hata kama hawataki ila wanatekeleza na naomba CCM, Na Tutahakikisha CCM inashinda tena na kuendelea kuwa madakani.Ahsante sana Karibu Mhe.Prof.Kikwete
Wenu MTANZANIA JITAMBUE-MOSHI KILIMANJARO...
0 maoni:
Chapisha Maoni