Mtanzania Jitambue
facebook tweeter google linked in you tube rss
  • Home
  • Biashara
  • Burudani
    • Michezo
  • Siasa
  • Breaking News
    • Tanzania
      • Serikalini
  • Afya
  • Wazalendo
  • Ulimwenguni

KARIBU TANZANIA.

CLICK HERE FOR BREAKING NEWS.

BAADHI YA WAZALENDO KASKAZINI.

.

.

First slide Next

Ijumaa, 13 Machi 2015

  • 00:22
  • Mtanzania Jitambue
  • No comments

WANANCHI WA VUNJO WAMCHANGIA PESA INNOCENT MELLECK SHIRIMA KWA AJILI YA KUCHUKULIA FOMU YA UBUNGE


Innocent Melleck akiwa na baadhi ya wananchi waliojitokeza
Wananchi wa vunjo walijitokeza kwa wingi sana kumchangia mbunge wao mtarajiwa pesa ya kuchukulia fomu ya ubunge. Tukio hilo lilifanyika tarehe 07.03.2015 siku ya jumamosi mji mdogo wa Himo. Katika tukio hilo wananchi hao walimuomba kijana huyo Innocent Melleck akubali ombi lao la kugombea nafasi ya ubunge jimbo la vunjo kwakuwa wana imani naye sana.
Furaha ya wananchi kwa Innocent Melleck
Wengi waliohudhuria katika viwanja hivyo walionekana kuwa na imani ombi lao litakubaliwa na kijana huyo. Katika mchango huo wa kumchangia kijana huyo zaidi ya kiasi cha shilingi za kitanzania milioni 2.6 ziliweza kupatikana.
Alipotakiwa kujibu ombi la wanavunjo kijana Innocent Melleck alisema.." Kwakuwa wazee wangu, vijana wenzangu mmeamua kunifanyia suprise katika hili na kuamua kutoa pesa zenu ambazo binafsi sifahamu mmeipataje, nataka niwaahidi ombi lenu nimelipokea kwa mikono miwili na muda ukifika nitafanya maamuzi sahihi. Naomba tujiandae kuvuka daraja hili. Asanteni sana tena sana"
Moja ya mashuhuda waliokuwepo eneo la tukio walioneka kujawa na furaha ya kila aina hasa kutokana na ombi lao kupokelewa na mbunge wao mtarajiwa. 
Ni kwa miaka mingi sasa jimbo la vunjo limekuwa likikosa mtu sahihi wa kuwaletea maendeleo yao. Kutokana hali hiyo kijana Innocent Melleck anaonekana ni mtu sahihi na anaeungwa sana mkono na wananchi wa jimbo la vunjo. Hasa kutokana na historia yake kwa wananchi wa jimbo la vunjo kutokuwa na mashaka juu yake.
Mwananchi akipokea na kuanadika michango ya pesa
Mmoja wa watu waliohudhuria alinukuliwa akisema kuwa.." Jimbo la vunjo watu wameligeuza kuwa shamba la bibi, kila anayejisikia anakuja. Lakini imekuwa ni fedheha kwetu kwa kitendo hiki mana nje ya jimbo la vunjo tunadharaulika sana. Kwa mfano wapo baadhi ya watu wanaotaka kugombea jimbo hili lakini ukifatilia historia yao tayari walishapata nafasi hiyo lakini walishindwa kabisa kuiweka vunjo katika hali ya nzuri ya kimaendeleo. Wapo wengi leo James Mbatia na Mrema wanataka tena hii ni dharau kubwa sana kwa wanavunjo na hakika hatupo tayari kuvumilia hili kutokea. Mana hatuwezi kuifanya vunjo kama nyanya ukienda sokoni na pesa unazipata nasema haiwezekani kabisa. Tuliwapa nafasi 1995-2000 na 2010-2015 hakuna jipya walilofanya halafu leo bila haya wala aibu wanakuja tena kwa mara nyingine huu ni udhalilishaji wa makusudi kabisa"
Uchaguzi wa nafasi za ubunge unatarajiwa kufanyika oktoba 2015 huku vyama vinne vya kisiasa kila kimoja kimejinasibu kusimamisha wagombea wake.
Innocent Melleck Shirima akiongea na wananchi waliomuomba atangaze nia haraka iwezekanavyo

Read More

Alhamisi, 12 Machi 2015

  • 23:35
  • Mtanzania Jitambue
  • No comments

TAMKO LA MABALOZI WA USALAMA BARABARANI KUHUSU AJALI NA HALI YA USALAMA BARABARANI

TANZANIA ROAD SAFETY AMBASSADORS-RSA

(MABALOZI WA USALAMA BARABARANI)

TAMKO LA RSA KUHUSU AJALI NA HALI YA USALAMA BARABARANI

13.03.2015

Ndugu wananchi,

Napenda kuchukua nafasi hii, kwa niaba ya mabalozi wa usalama barabarani, kuungana na watanzania wote kutoa pole kwa wafiwa na majeruhi wa ajali ya basi la Majinja Express iliyotokea huko Mafinga mkoani Iringa tarehe 11.03.2015 kupoteza maisha ya watu 50 mpaka sasa na kuacha majeruhi wengi. Ajali hii ni ya kustua na kusikitisha sana. Poleni majeruhi na mwenyezi mungu awajalie majeruhi uponyaji wa haraka na marehemu awapokee kwenye nuru ya uso wake.

Kwa miaka mingi sasa ajali za barabarani zimeendelea kukatisha maisha ya watanzania walio wengi na kuwaacha wengi mayatima na ulemavu wa kudumu. Hatua mbalimbali zimekuwa zikichukuliwa na serikali, lakini ufanisi wa hatua hizo bado umekuwa wenye mashaka. Imekuwa kawaida kuwa ajali inapotokea jibu la haraka limekuwa mwendo kasi na hatimaye tumeishia kutoa salamu za rambirambi tu na kusahau. Hatukatai ni kweli kabisa makosa ya kibinadamu inasemekana yanachangia sana hizi ajali. Hata hivyo ipo haja ya kwenda mbali zaidi ya majibu mepesi kuwa ni mwendo kasi. Katika ajali hizi daima suala la haki za majeruhi baada ya ajali limeendelea kuwa tatizo kubwa sana. Wengi wamekuwa hawapati haki zao kabisa au hupata kwa kuchelewa jambo linalopelekea kuwapa machungu zaidi majeruhi na hata yatima na wajane wanaobakia baada ya ndugu zao kufariki dunia. Ifike hatua tuache kutoa majibu mepesi kwa maswali magumu na kuchukua hatua stahiki ili kukabiliana na hali hii.

Sisi kama mtandao wa mabalozi wa usalama barabarani(RSA) tunaitaka serikali na wadau wanaohusika kuchukua hatua stahiki na za makusudi kukabiliana na hali hii hasa zinapotokea ajali kubwa(Major accidents).
  1. Kuundwa kwa taasisi huru na ya kitaalamu (Road Accidents Investigation Board) kuchunguza kwa kina ajali husika ili kubaini chanzo halisi cha ajali hiyo na vitu vilivyochangia.
  2. Kuwaajibisha wote watakaobainika kwa namna moja ama nyingine kuchangia kusababisha ajali. Hii ihusishe uwajibikaji wa mamlaka mbalimbali kama vile Polisi Usalama Barabarani, SUMATRA, TANROADS na wamiliki wa magari husika.
  3. Bima za magari ya abiria na ya mizigo zichunguzwe ili kuona kama zinakidhi vihatarishi (Risks) vinavyoweza kusababishwa na magari hayo, uhai na uhalali wa bima hizo na ukubwa fidia zinazotolewa na bima hizo (coverage).
  4. Shule za udereva na sheria zake ziangaliwe upya ili kuona kama shule hizo zinakidhi mafunzo ya udereva kulingana na teknolojia ya sasa ya maendeleo ya magari na hasa mitaala inayotumika.
  5. Mfumo wa upatikanaji leseni uangaliwe kwa kina kuona kama hauna mianya ya kuwafanya watu wapate leseni bila kupitia mafunzo au kufuzu vizuri na ikiwezekana mamlaka inayojitegemea ya utoaji leseni na ukaguzi wa magari ianzishwe kama ilivyoainishwa kwenye sera ya usalama barabarani, 2009.
  6. Bodi ya uchunguzi wa ajali pamoja na mambo mengine ichunguze mambo yafuatayo na kuweka wazi ripoti yake:-  
  • Iwapo TANROADS wana programu ya ukaguzi wa mara kwa mara wa barabara na kuzifanyia marekebisho.
  • Iwapo mabasi yanayohusika kwenye ajali yanakuwa na Bima sahihi na inayotosha kufidia wahanga wa ajali hizo.
  • Iwapo kila mamlaka ilitekeleza wajibu wake kabla na baada ya kutokea kwa ajali, pawepo na bajeti ya kutosha kufanya matengenezo ya barabara na kama ipo kwanini ukaratabati haufanyiki kwa wakati.
  • Iwapo wamiliki wa mabasi wana sera na taratibu zozote za kukabiliana na ajali na nidhamu za watumishi wao.
  • Mafunzo ya dereva husika aliyepata ajali, historia ya maisha yake, na siku kabla ya ajali au wakati wa ajali hali ya akili yake ilikuwaje.
  • Nafasi ya hali ya kijiografia katika ajali husika mathalani, muundo wa kijiografia eneo hilo, hali ya hewa n.k
  • Mwendo wa gari husika na hali ya gari hadi wakati wa ajali (Roadworthiness).
  • Abiria kwa kiasi gani walichangia mwendo mbaya kwa kutoripoti na je iwapo waliripoti ni hatua gani stahiki zilichukuliwa dhidi ya dereva au abiria husika.
  7. Kutungwa kwa sheria ya mauaji ya bila kukusudia yanayosababishwa na taasisi (Cooperate            manslaughter Act) kama ilivyo nchini Uingereza ili kuziwajibisha taasisi zisizojali usalama wa watu.
  8. Kutekeleza kwa vitendo malengo ya sera ya usalama barabarani 2009, na kuweka adhabu kali kwa wanaokiuka sheria za usalama barabarani.
  9. Kuweka utaratibu mzuri wa kushughulikia malipo ya fidia ya bima kwa waathirika wa ajali ikiwemo wale wanaopata athari kutokana na magari ya serikali kusababisha ajali.
 10. Kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuelimisha na kuwaongezea abiria nguvu za kisheria za kudhibiti mwendo madereva njiani tunaamini haya yatatekelezwa vyema, tunaweza kupunguza ajali kwa kiwango kikubwa sana. 

Sisi kama mabalozi wa usalama barabarani tunaendelea kutii sheria bila shuruti na kuendelea kwa nguvu zetu zote kutoa elimu ya usalama barabarani kila siku kupitia mbinu mbalimbali.


Imetolewa na

JOHN SEKA
Kwa niaba ya Mabalozi wa usalama Barabarani- Tanzania

Read More

Jumanne, 10 Machi 2015

  • 07:22
  • Mtanzania Jitambue
  • No comments

JAMES MBATIA: WANANCHI WA VUNJO WANATAKA VITOCHI NA SI MAENDELEO

 http://www.24tanzania.com/wp-content/uploads/2013/01/c4c1James-Mbatia1.jpg
   (Mb) James Mbatia
Mbunge wa kuteuliwa na Rais (Mb) James Mbatia ameiambia radio KILI FM 87.5 Mhz ya Moshi Mkoani kilimanjaro wakati wa mahojiano yake tarehe 20/02/2015 siku ya Ijumaa kuwa kipindi alipokua mbunge wa jimbo hilo 1995 mpaka 2000 alishindwa kufanya vema upande wa michezo kwasababu wananchi wa vunjo hawapendi michezo hiyo bali wao hupenda zaidi pombe(VITOCHI).
Hayo yalitokana na swali aliloulizwa na mtangazaji wa kipindi hicho juu suala la maendeleo ya michezo kuwa nyuma sana katika jimbo la vunjo. (Mb) James Mbatia alisema"Swali lako ni zuri sana ndugu mtangazaji, nakumbuka kipindi ni mbunge nilijaribu kukuza michezo lakini wazee wakanionya kuwa hawataki, wao wanahitaji vitochi"
Pia, alitoa msimamo wake wa kutozikubali hata kidogo shule za kata za serikali ijapokuwa amewahi kuzitembelea shule hizo.
Read More

Alhamisi, 12 Februari 2015

  • 09:10
  • Mtanzania Jitambue
  • No comments

WAFANYABIASHARA NDOGO NDOGO WAMUOMBA KADA WA CCM DAUD BABU MRINDOKO KUGOMBEA JIMBO LA MOSHI MJINI

Ndg. Daud Babu Mrindoko akiwa na baadhi ya akina mama wafanyabiashara ndogondogo
Katika tukio lisilokuwa la kawaida wakina mama ambao ni wafanyabiashara ndogondogo wamuomba kijana na kada wa chama cha Mapinduzi Ndg. Daudi Babu Mrindoko akubali wito wao wa kugombea jimbo la moshi mjini.
Tukio hilo limetokea mapema ya siku ya leo Alhamisi mara alipofika maeneo ya wafanyabiashara hao ili kupata mahitaji yake ya kawaida. Wakina mama hao ambao pia ni wafanyabiashara ndogondogo wamemtaka kijana huyo kugombea nafasi hiyo ya ubunge na kumuahidi kumuunga mkono katika kila hatua.
Wafanyabiashara hao wanasema kuwa wamelazimika kufanya hivyo hasa kutokana na kumfahamu vema kijana huyo uwezo wake wa kujitolea na kusaidia jamii. Baadhi yao wamesikika wakisema "kwasasa tunahitaji mabadiliko makubwa ya kiutawala mana hawa ambao wapo sasa bado hatujaona mchango wao kwetu, zaidi ni hali ya kimaisha kuzidi kuwa mbaya kila kukicha. Tunakuomba kijana wetu ukubali ombi letu mana tunatumbua uwezo wako wa kutumikia jamii"
Wafanyabiashara hao wamesikika wakisema safari hii hawatakubali kufanya makosa tena, shida ambayo wameipata kwa kipindi cha miaka kumi na tano hawapo tayari kuona hali hiyo inajirudia kwa mara nyingine tena..." Mwaka 2010 tulimpatia tena nafasi hiyo tukiamini kuwa kosa si kosa bali kurudia kosa, lakini bado makosa amezidi kuyarudia yale yale tena safari hii hali ndio mbaya zaidi sasa tumechoka na tunahitaji kufanya mabadiliko makubwa katika jimbo letu la moshi mjini"
Ndg. Daud Mrindoko akiwa anapata huduma
Kwa upande wa kijana huyo Ndg. Daudi Mrindoko amesema " Mimi kijana wenu sina mengi ya kuwaambia ila tuzidi ombeana kwa mwenyezi mungu mana ushauri wenu ni mzito sana, muda ukifika kila kitu kitakuwa wazi ila nimeupokea kwa mikono miwili ushauri wenu na hakika nitaufanyia kazi asanteni sana na mungu awabariki ninyi"
Wafanyabiashara wakiendelea na shughuli zao za kila siku sokoni
Read More
  • 08:04
  • Mtanzania Jitambue
  • No comments

MH. MREMA:-"MBATIA HANA UWEZO WA KUWA MBUNGE WA JIMBO LA VUNJO"

Mbunge wa jimbo la Vunjo Mh. Augustino L. Mrema akiwa katika kipindi maalumu cha mahojiano na redio Times fm ya jijini Dar es salaam juzi, amesema kwamba aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la vunjo mwaka 1995(James Mbatia) kwasasa hana uwezo wala jeuri ya kuwa mbunge wa jimbo la vunjo kwa mara nyingine tena.
Mbunge wa jimbo la vunjo Mh. Augustino Mrema
Aliyasema hayo kutokana na mchuano mkali uliopo jimboni kwake kwa baadhi wa watu mbalimbali kujitosa kutaka kupata ridhaa ya wananchi wa jimbo la vunjo kwa nafasi hiyo ya ubunge. Anasema kuwa Mh. James Mbatia hana nafasi kwa vunjo kwasababu tayari alishapewa nafasi kama hiyo mwaka 1995 tena mimi Mrema nikiwa mwenyekiti wake wa chama wakati huo, lakini sote ni mashahidi kwa kile ambacho amekifanya kipindi cha uongozi wake na mustakabali wa maisha ya jamii ya wanavunjo hali ilivyokuwa wakati huo.
Nikisema hafai si kwasababu namchukia la hasha ila uwezo wake wa kuwatumikia wananchi na rekodi yake ndio inayomhukumu moja kwa moja. Anasema kuwa kwa kipindi cha miaka mitano aliyowahi kuwa madarakani hakuna jipya la maana alilowahi kulifanya katika mambo ya elimu, barabara, umeme, kilimo, maji, afya, mazingira, ulinzi na usalama, michezo pamoja na uboreshaji wa kipato cha mtu mmoja mmoja sasa leo akisema anaouwezo wa kuyafanya hayo huo ni uongo uliokithiri na kuwafanya wananchi wa jimbo la vunjo ni wajinga kupita kiasi huku ni sawa na kuwadharau.
Mrema II
Mh. James Mbatia akiwa na Mh. Mrema
Wakati huo huo, katika hali isiyo ya kawaida mbunge huyo wa vunjo mh. Mrema amesema kwasasa mtu ambaye ana uwezo mkubwa kama akikosa nafasi ya kuwawakilisha wananchi wa vunjo bungeni katika uchaguzi wa oktoba 2015 ni mmoja tu kwa wote ambao tayari wamejitokeza nae si mwingine bali ni kijana INNOCENT MELLECK SHIRIMA.
Anasema akimzungumzia kijana huyo ni kwamba ni mtu pekee na sahihi kwa watu wa jimbo la vunjo hasa kutokana na uwezo na kipaji chake alichonacho cha kuwatumikia wananchi. Anasema kuwa huyu ni kijana ambaye wananchi wa jimbo la vunjo wanapaswa kutokuja kufanya makosa hata kidogo na wahahakishe wanamchagua ili aweze kuwatumikia ipasavyo.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhqDOtlc68k4RfZS4HXD6QSvWIk6ZXhr_hE68KNoEi12GVfUX3DfKoAoNbsFG477kUsU9fE0hyphenhyphenCpu4XDUy2JzIGIwM7ervHpWsz2BUlRVzRtuwULkGfIKuK833r-GRJZAxHZdZn9sWp-CI/s1600/unnamedI1.jpg
Innocent Melleck
Anasema.." Mtu sahihi kwa vunjo kama sio mimi mrema basi ni yule kija Innocent Melleck na sio wengine, hivyo wananchi wangu wa jimbo la vunjo msikubali kununulika hata kidogo"
Pia, ametumia muda huo kukanusha tuhuma zote zilizoelekezwa kwake na Mh. James Mbatia dhidi yake, amemtaka kufanya siasa safi na sio hizo anazoendelea nazo kwasasa hivi kwasababu hazijengi bali hubomoa.
Read More

Jumatano, 11 Februari 2015

  • 08:22
  • Mtanzania Jitambue
  • No comments

KIJANA INNOCENT MELLECK SHIRIMA AWATAHADHARISHA WANAVUNJO KUTORUDIA MAKOSA YA 1995, 2000 NA 2010

Innocent Melleck Shirima mwanaharakati wa vijana
Kijana Innocent Melleck Shirima awatahadharisha wananchi wa jimbo la vunjo kutokuja kufanya makosa ya mwaka 2010 kwa kumchagua mbunge ambaye leo hii ni mwiba mkali kama sio sindano inayowatesa katika mioyo yao katika uchaguzi mkuu ujao oktoba 2015 wa kuwapata viongozi wapya kuanzia ngazi ya udiwani, ubunge na uraisi.
Ameyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano maalumu na mtandao huu wa jamii.."nawasihi sana ndugu zangu wa vunjo kutorudia yale makosa ya mwaka 2010, kiongozi mzuri ni yule ambaye atakuwa daraja zuri kati yao na serikali kuu, halmashauri, wafadhili wa ndani na nje na hata wananchi wenyewe kwa wenyewe na sio uwezo wake binafsi wa mali au utajiri"
Innocent Melleck Shirima anasema kuwa baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakiwaaminisha wananchi kuwa mbunge tajiri atawasaidia wananchi wake hata kama hana uwezo au maarifa ya kuwasaidia wananchi wake. Hali hiyo ndio ambayo imewapelekea wananachi wa jimbo la vunjo kukosa maendeleo kwa kipindi kirefu sana. Anasema kuwa mwaka 2010 kijana ambaye ndiye alipaswa kuwa mtu sahihi kuwawakilisha wananchi wa jimbo la vunjo (Crispin Meela) kutokana na uwezo wake wa kuwa daraja zuri kwao alikosa nafasi hiyo kwa imani tu hana uwezo wa kimali hatimaye wananchi wa jimbo la vunjo wakamchagua mbunge ambaye kwasasa kwao ni mwiba na hakuna anaetaka kumsikia.
Mkuu wa wilaya ya Rungwe Crispin Meela
Anaendelea kusema kuwa endapo wananchi wa jimbo la vunjo watarudia kosa la mwaka 2010 katika uchaguzi huu wa mwaka 2015 hakika watakuja kujutia sana kuliko hata namna ambavyo wanajutia hivi sasa. Anasema kuwa yupo mgombea kwa sasa amekuwa akiwalaghai wananchi wa jimbo la vunjo kwa kutumia pesa nyingi sana kwa kuzigawa huku akiwaaminisha kuwa ana uwezo mkubwa wa kuletea mabadiliko makubwa katika jimbo la vunjo.

James Mbatia mbunge wa kupitia Nccr-Mageuzi mwaka 1995
Amewataka wananchi kutokubali kudanganywa na hatimaye kurudia makosa tena. Anasema kuwa.."nawasihi sana hao wagombea kujipima kwanza kama wanafaa kuwawakilisha hao wananchi kwa kutizama rekodi zao za nyuma katika jimbo hilo la vunjo halafu ndipo wajitokeze mbele za wananchi. Kwani wananchi wa jimbo la vunjo bado wanakumbuka vizuri maumivu makali ya kimaisha waliyoyapata kipindi ambacho hao viongozi walipata hiyo fursa ya kuwawakilisha wananchi wa jimbo la vunjo"

Amewataka wananchi wa jimbo la vunjo kutokubali kudanganywa kuwa hao wanaotaka kupewa nafasi kwa mara nyingine kama wataweza kuwaletea maendeleo kama vile kuboresha vipato vyao kwa kuishawishi serikali kuwawekea mazingira bora kama vile kuwajengea miundombinu bora ya barabara, umeme pamoja na kunufaika na rasilimali mlima kilimanjaro. Anasema" kwanza wananchi wa vunjo wanapaswa kujiuliza haya maendeleo ambayo leo wanadai watakuja kuyaleta, kwanini kipindi walivyokuwa wabunge hawakuweza kutimiza hayo? iweje leo waje na kusema kuwa wataweza kuleta hayo mabadiliko? huo ni utapeli wa mchana kabisa"

Innocent Melleck Shirima
Anasema kwamba leo vijana wa jimbo la vunjo wanahangaika na namna ya kuboresha vipato vyao ili waweze kujiendesha na kujikimu maisha yao na familia zao lakini sote ni mashahidi juhudi ndogo ambazo zinazofanywa na hawa wawakilishi ambao wapo bungeni kukosa ushawishi kwa serikali kuu na hata wafadhili wa ndani na nje na hatimaye hali za vijana wa vunjo kuendelea kuwa katika wakati mgumu sana.

Anasema" nawaomba sana vijana waweze kuwahoji wabunge hao dhamira yao ya dhati kwao na sio tu dhamira yao iwe kuwatumia kisiasa kwa maslahi yao binafsi"

Mwisho, amewataka wananchi wa jimbo la vunjo kuwa wavumilivu kipindi hiki kigumu cha kuchagua viongozi wawatakao lakini wafanye maamuzi ya busara na sio ya kutaka kukomoa mtu au chama fulani.


Read More

Jumanne, 10 Februari 2015

  • 11:54
  • Mtanzania Jitambue
  • No comments

UN YAIPA LAWAMA TANZANIA KWA HALI ILIVYO DRC


Hali ilivyo DRC
Umoja wa mataifa imezituhumu serikali za Tanzania na Burundi kuhusiana na hali katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Ripoti
mpya ya kundi la wataalamu wa umoja huo kuhusu Congo, imeituhumu
Tanzania kwa kuwaruhusu viongozi wa kundi la waasi wa FDLR kuandaa
mikutano nchini humo.

Imeeleza pia kwamba wanajeshi wa Burundi wametekeleza unyanyasaji wa kingono.

Taarifa
hiyo ya Umoja wa mataifa inasema kuwa tangu mwaka wa 2013, viongozi wa
FDLR na baadhi ya washirika wao wa kisiasa kutoka Ulaya wamekuwa
wakikutana nchini Tanzania.

Majeshi ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo wakipambana na waasi
Lakini wachunguzi wa Umoja wa
mataifa walipoiuliza serikali ya Tanzania kujibu madai haya ilikanusha
kabisa kuwahi kuakaribisha mikutano yoyote ya waasi ndani ya ardhi yake
na kuongeza kuwa hakujawahi kuwa na mazungumzo yoyote kati ya majeshi
yake na wapiganaji wa FDLR.

Umoja wamataifa umesema pia kuwa una
ushahidi wa pesa zilizotumwa kutoka taifa hilo la Afrika Mashariki kwa
baadhi ya washukiwa nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Ripoti
hiyo pia imelaumu kundi hilo la FDLR kwa kutotekeleza ahadi yao ya
kusalimisha silaha na kujisalimisha kufikia Januari mwaka huu.

UN
inasema kuwa FDLR wamewatuma wazee waliodhoofika kiafya pekee
kujisalimisha na kukabidhi silaha chache sana ambazo zina hitilafu.

Kundi
la FDLR, liliundwa mwaka wa 2000 na wahutu waliokimbilia Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo kufuatia mauaji ya kimbari ya Rwanda.

Wapiganaji wa kundi la FDLR
Kundi hilo linapinga utawala wa kitutsi na ushawishi wake katika eneo la maziwa makuu.

Rwanda
imekuwa ikitazama kundi hilo kama tisho kubwa kwa utawala uliopo na kwa
kauli moja na Umoja wa mataifa imekuwa ikishinikiza kupokonywa silaha
kwa wapiganaji wake.

Ripoti hiyo pia imetoa madai ya ubakaji na unyanyasaji wa kimapenzi unaofanywa na wanajeshi wa Burundi katika Kivu ya Kusini .

Wataalamu
hao wa Umoja wa mataifa wamependekeza serikali za Burundi na Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo zifanyie uchunguzi madai hayo ambayo wanasisitiza
yalifanywa namajeshiya Burundi pamoja na kikundi cha vijana wapiganaji
wajulikanao kama Imbonerakure.



@bbc news


Read More
← Machapisho Mapya Machapisho ya Zamani → Nyumbani
Jisajili kwenye: Machapisho (Atom)

Lebo

  • Biashara
  • Michezo
  • Serikalini
  • Siasa
  • Tanzania
  • Ulimwenguni
  • UVCCM
  • Wazalendo

Kumbukumbu la Blogu

  • ▼  2024 (2)
    • ▼  Julai (2)
      • CHANGAMKIENI ASILIMIA 10 ZA MIKOPO YA HALMASHAURI .
      • RAIS DKT.SAMIA SULUHU HASSAN MGENI RASMI MAADHIMIS...
  • ►  2015 (22)
    • ►  Septemba (1)
    • ►  Aprili (2)
    • ►  Machi (5)
    • ►  Februari (10)
    • ►  Januari (4)
  • ►  2014 (97)
    • ►  Desemba (34)
    • ►  Novemba (27)
    • ►  Oktoba (3)
    • ►  Septemba (33)
Inaendeshwa na Blogger.

Machapisho Maarufu

  • WAFANYABIASHARA NDOGO NDOGO WAMUOMBA KADA WA CCM DAUD BABU MRINDOKO KUGOMBEA JIMBO LA MOSHI MJINI
    Ndg. Daud Babu Mrindoko akiwa na baadhi ya akina mama wafanyabiashara ndogondogo Katika tukio lisilokuwa la kawaida wakina mama ambao n...
  • KIJANA INNOCENT MELLECK SHIRIMA AWATAHADHARISHA WANAVUNJO KUTORUDIA MAKOSA YA 1995, 2000 NA 2010
    Innocent Melleck Shirima mwanaharakati wa vijana Kijana Innocent Melleck Shirima awatahadharisha wananchi wa jimbo la vunjo kutokuja ku...
  • PICHA ZA MATUKIO ZA MH. OLIVIA SANARE ALIPOHUDHURIA MAAZIMISHO YA MIAKA 38 YA CCM MKOANI RUVUMA
    Kada wa ccm Olivia Sanare akiwa na baadhi ya walioshiriki maadhimisho uwanjani   Picha ya kwa pamoja na mh. Olivia Sanare Mh. Oliv...
  • DAUDI MRINDOKO ASHAWISHIKA NA KAKUBALI OMBI LA WANANCHI WA JIMBO LA MOSHI MJINI KUGOMBEA UBUNGE 2015
    Thursday, 23 April 2015 DAUDI MRINDOKO ASHAWISHIKA NA KAKUBALI OMBI LA WANANCHI WA JIMBO LA MOSHI MJINI KUGOMBEA UBUNGE 2015 Yafuatayo ndi...
  • break News:MABUS YA KILENGA YAGONGANA ILA YAMEARIBIKA KIDOGO.
    Ajali imetokea hapa daraja la kifaru Himekuwa ya Ajabu ajabu ni Bus moja la Kilenga limegonga nyuma ya Gari lingine la Kilenga majira ya 10...
  • UTEUZI WA NAFASI ZA UONGOZI KATIKA TAASISI YA WAZALENDO TANZANIA
    TAASISI YA WAZALENDO TANZANIA TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Tarehe 07/12/2014. Mwenyekiti wa Wazalendo Taifa Ndg. Daud Mrindok...
  • CHIEF MRINDOKO: "MUDA UKIFIKA NITAJIBU MAOMBI YENU YA KUNISHAWISHI KUGOMBEA UBUNGE MOSHI MJINI"
    Leo Jumapili tarehe 12/04/2015, mwenyekiti wa taasisi ya wazalendo Taifa Ndg. Chief Daud Mrindoko ameyasema hayo katika uzinduzi wa Album ya...
  • CCM WILAYA YA MOSHI VIJIJINI YAADHIMISHA MIAKA 38 YA KUZALIWA KWAKE KWA KUWATEMBELEA WAGONJWA HOSPITALI YA KILEMA MKOANI KILIMANJARO
    Viongozi wa chama cha mapinduzi wilaya ya moshi vijijini wakiwasili hospitali ya Kilema Chama cha Mapinduzi wilayani moshi vijijin...
  • WANANCHI WA VUNJO WAMCHANGIA PESA INNOCENT MELLECK SHIRIMA KWA AJILI YA KUCHUKULIA FOMU YA UBUNGE
    Innocent Melleck akiwa na baadhi ya wananchi waliojitokeza Wananchi wa vunjo walijitokeza kwa wingi sana kumchangia mbunge wao mtaraj...
  • DR.SLAA AFUNGUKA UKWELI...UKAWA MASHAKANI
    LIVE UPDATE Kutoka Serena Hotel Ambako Dr. Slaa Anaongea 1.Napenda  kumshukuru  mwenyezi  mungu  kwa  kutujali  uzima. 2. Nimeamua  kujito...

Machapisho ya Karibuni

Recent Posts Widget

Kurasa

  • Home

Kunihusu

Mtanzania Jitambue
Tazama wasifu wangu kamili

Sample Text

Copyright © Mtanzania Jitambue | Powered by Blogger
Template Designed by Kanoutechno™
Blogger Templates