Jumatano, 28 Januari 2015

Wafanyabiashara wa Mbuyuni Sokoni wafungiwa Maduka leo na Manspaa ya Moshi, Mtanzania Jitambue yafanya mahojiano na Wafanyabiashara hao wamesema kodi imekuwa kubwa sana kwani ukienda TRA kodi,
Huku wanasema tusipange Bidhaa nje ya Duka,Kodi imepanda mara mbili ya kodi ya Zamani na ukipanga Kitu barazani hawataki hivi ukiweka ndani nani ataona hizo bidhaa???Wafanyabiashara hawataki kusikia Chadema kabisa hapa Moshi..
Wanalaumu Baraza la Madiwani wa Chadema kwa kupisha Sheria Ambazo kabla hawajawa na Council walisema tutapanga vitu nje ya baraza hata kwenye Barabara tutapanga ila sasa imekuwa tofauti na jinsi walivyotuahidi, 
Kuna aliyejitambulisha kwa jina:-Asha alisema Huyu Meya Jafar hatutaki hata kumsikia na madiwani wao kwani wametuahidi uongo mtu na sasa tunataabika hivi kama leo nimefika manspaa naambiwa nilipie Faini Tsh.700, 000 (Laki saba) na biashara nimefungua Tarehe 09/01/2015 na muda wote nilikuwa nafatilia TRA nimemaliza kulipalia TRA jana leo manspaa wanataka Hela zote hizi hivi ni maisha gani haya???
Naomba waangalie hizo Sheria zao na sisi wanatanzania tunaojituma kujikwamua kwa kukosa Ajira tunakuja kufanya biashara wanakuja kunifungia...

Wenu,
Mtanzania Jitambue-Moshi

0 maoni:

Chapisha Maoni

Inaendeshwa na Blogger.

Machapisho Maarufu

Machapisho ya Karibuni

Recent Posts Widget