Jumamosi, 6 Julai 2024

- SOKO LA BWILINGU NI FURSA KWA KILA MTU  AELEZA MHE. MBUNGE RIDHIWANI KIKWETE


Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambaye pia ni Mbunge wa Chalinze  Mhe.Ridhiwani Kikwete amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chalinze kuwapeleka Maafisa Maendeleo kukutana na kina Mama, Vijana na Kina Baba ili kuwaelekeza namna yakuunda makundi yatakayowawezesha kukopa fedha kwaajili ya kunufaika na fursa mbalimbali za mikopo ya Halmashauri ya asilimia 10  isiyo na riba ambayo imeanza kutolewa tena kuanzia tarehe 01.07.2024 baada ya Rais kuelekeza yafanyike maboresho ya utoaji mikopo hiyo ambayo inaokoa makundi maalum katika kujiinua kiuchumi.


Amesema "anataka vikundi vyenye utaratibu mzuri ambavyo vinatoa haki sawa kwa wanachama wote kunufaika na fedha hizo za mikopo na kwakuzingatia hakuna mtu mbabe, hakuna mtu mwizi, hakuna mtu anayetumia nafasi hiyo kujinufaisha mwenyewe kwakua moja ya jambo kubwa ambalo lilifanya utaratibu huo ukasimamishwa ni baadhi ya watu wanakuja katika jina la kikundi alafu fedha zinazoingizwa zinakwenda kwa mtu mmoja na yeye ananufaika pekeyake", alisema Mhe. Ridhiwani.


Ameyasema hayo kwenye mkutano na wananchi wa Chalinze mkoani Pwani ambapo ameongeza kuwa "maelekezo yameshatolewa na mimi kwangu ni maelekezo kwa Ofisi ya Mkurugenzi kuhakikisha kwamba wananchi wa Chalinze hususani wafanyabiashara wanakua ni sehemu ya kundi la kwanza lakufaidika na fursa hiyo, aliendelea kusema Mhe. Ridhiwani


Katika hatua nyingine Mhe. Ridhiwani amewaambia wananchi wa Chalinze kwa utaratibu waliojiwekea Baraza la Madiwani waliamua kutumia makusanyo ya ndani kwa kutenga fedha kwaajili ya ujenzi wa soko la Bwilingu na kununua baadhi ya majengo yaliyokuwepo katika eneo hilo ili kupata soko lenye ukubwa ambalo limewaweka wafanyabiashara wengi  kwenye eneo hilo, na litatumika na watu mbalimbali kutoka maeneo yanayozunguka eneo hilo na mikoa ya jirani kwaajili ya biashara zakujiingizia vipato.


Amesema "wananchi hawakukosea kuwachagua na kuwatuma viongozi wanaowatumikia kwakua wanatengeneza fursa ambalimbali zakibiashara bila ubaguzi kwa kuzingatia afya za wafanyabiashara na wateja wanaofika kupatiwa huduma katika eneo hilo, alisema Mhe.Ridhiwani.


Aidha amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amewezesha kila halmashauri kupata fedha hizo ambazo zinakwenda kuongeza vipato vya makundi maalum nakujikwamua kiuchumi.



Na.Elisa Shunda, Dar Es Salaam.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi  (CCM) anatarajiwa kuwa mgeni rasmi Katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Wazazi Kitaifa Julai 13 mwaka huu Mkoani Katavi.


Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam, leo tarehe 29/06/2024. Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi Tanzania Jumuiya ya CCM, Ndg. Ally Salum Hapi *(MNEC)* amesema  maadhimisho hayo yataanza  Julai 8 na kufikia kilele chake Julai 13 mwaka huu.


Hapi amesema  Katika maadhimisho  ya wiki ya Wazazi yataambatana na shughuli mbalimbali za kijamii na kichama,


Amesema shughuli zitakazofanyika katika maadhimisho hayo ni pamoja na ufunguzi wa Wiki ya Wazazi Kitaifa ambayo  itafanyika Julai 8  Wilayani Mlele Mkoani Katavi.


Aidha amesema katika ufunguzi huo wanatarajia kupanda miti zaidi ya laki  moja *(100,000)*


Hata hivyo amesema Rais Dkt. Samia Atawakagulia shughuli mbalimbali za ustawi wa Jamii ambazo zinafanywa na Dawati la jinsia la Jeshi la Polisi na  Shughuli zingine za Chama Cha Mapinduzi za usajili wa kielekroniki.


Wanatarajia pia kuwa na Kongamano la Maadili na Malezi, huku akisema Kama wanavyofahamu wanalo tatizo la mmomonyoko wa Maadili Katika Jamii na tatizo hilo linafungamana na malezi.


Amebainisha kuwa Katika maadhimisho ya Wiki ya Wazazi Kitaifa kutakuwa pia na usiku wa utamaduni ambao utashindanisha vyakula vya asili vya kitanzania.


Akizungumzia kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025, amesema Jumuiya hiyo imejipanga kuhakikisha inashiriki  kuhamasisha watanzania kujitokeza kuboresha taarifa zao kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga Kura na wapiga kura wapya wajitokeze  kujiandikisha.


Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unatarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu, ambapo kauli mbiu ya Maadhimisho ya wiki ya Wazazi Kitaifa kuhamasisha Jumuiya ya Wazazi  inaendelea kutoa mchango na kuhamasisha kufanyika kwa uchaguzi na watanzania kuhamasika kushiriki katika uchaguzi huo.


Mwishoo.

Jumanne, 1 Septemba 2015

LIVE UPDATE Kutoka Serena Hotel Ambako Dr. Slaa Anaongea

1.Napenda  kumshukuru  mwenyezi  mungu  kwa  kutujali  uzima.

2. Nimeamua  kujitokeza  leo  hii  ili  kumesha  upotoshaji  na  kuuweka  wazi  ukweli.

3.Sina  tabia  ya  kuyumbishwa  na  ninasimamia  ninachokiamini.

4.Sina  ugomvi  na  kiongozi  yeyote  maana  siasa  sio  uadai.

5. Siasa  inapoongozwa  kwa  misingi  ya  upotoshaji, matokeo  yake  ni  vurugu.

6. Naweka  wazi  kuwa  mimi  sikuwa  likizo  na  hakuna  aliyenipa  likizo  yoyote.

7.Kilichotokea  ni  kuwa  niliamua  kuachana  na  siasa  tangu  28.7.2015  saa  sita  usiku  baada  ya  kutoridhishwa  na  kilichokuwa  kinaendelea  ndani  ya  chama  changu.

8.Ni  kweli  nilishiriki  kumleta  Lowassa  CHADEMA  Lakini  nilikuwa  na  misimamo  yangu  ambayo  ilitufanya  tusielewane.

9. Baada  ya  Lowassa  kukatwa  pale  Dodoma, Gwajima  ambaye  ni  mshenga  wa  Lowassa  alinipigia  simu  kutaka  kujua  nii  cha  kufanya.

10. Nilimpigia   Mwenyekiti    Mbowe  kumjulisha  na  tukakubaliana  kupanga  muda  wa  kuwasikiliza.

11. Kabla  ya  kuanza  kuwasikiliza, msimamo  wangu  ulikuwa  ni  kumtaka  Lowassa  kwanza  atangaze  kuhama  chama, aweke  wazi  ni  chama  gani  anaenda  na  ajisafishe  juu  ya  tuhuma  zake

12.Tangu  akatwe  jina, Lowassa  hakutangaza  kujitoa  CCM  na  wala  hakujisafisha  na  tuhuma  zake, kitu  kilichonifanye  nitofautiane  naye.

13. Niliwauliza  wanachadema  wenzangu  kuwa  Lowassa  anakuja  kama  Mtaji  au  Mzigo?

14. Swala  sio  urais  kama  watu  wanavyozusha, mimi  nilikuwa  nataka  mgombea  mwenye  uwezo  na  sifa  ambaye  ataweza  kuitoa  CCM.  Sikuwa  na  tamaa  ya  urais  kama  watu  wanavyosema

15. Tangu  Gwajima  atupe  taarifa  za  ujio  wa  Lowassa, Swali  langu  la  Lowasssa  kuwa  Mtaji  au  mzigo  halikuwahi  kujibiwa.

16. Nilitaka  kujua  ni  mtaji  gani  lowassa  atakuja  nao  na  ni  viongozi  gan  atakuja  nao.

17. Nilijibiwa  kuwa  anakuja  na  wabunge  50  wa  CCM, wenyeviti  22  wa  mikoa  na  wenyeviti  80  wa  wilaya.

18.Baada  ya  ahadi  hiyo, nilitaka  sasa  nipewe  majina  ya  hawa  watu  lakini  mpaka  tarehe  25  july  sikupewa  hayo  majina

19. Wenzangu  waliniambia  kuwa  tarehe  27  niitishe  kikao  cha  dharura  ila  niligoma  kwa  sababu  nilikuwa  sijapewa  haya  majina

20. Ndani  ya  kikao  hicho,  tulianza  kwa  mabishano  makali  kati  yangu  na  Mbowe, Lissu  na  Gwajima, viongozi  wenzangu  ni  shahidi  na  mungu  anajua. Msimamo  wangu  ulikuwa  ni  uleule  kujua  mchango  wa  Lowassa

21. Kikao  kile  kikavunjika, baadae  tukaingia  kamati  kuu  lakini  bado  msimamo  wangu  ulikuwa  ni  uleule. Baadae  nikaandika  barua  ya  kujiuzulu.

22.Profesa  Safari  aliichana  ile  barua.

23.Cha  kusikitisha  ni  kuwa  Kesho  yake  picha  zikaanza  kusambaa  mtandaoni  zikimuonyesha  la  lowassa  japo  viongozi  wangu  walizikana  zile  picha.  Kibaya  ni  kuwa  viongozi  waliuficha  ukweli

24.  Kesho  yake  niliandika  tena  barua  rasmi  ya  kujiuzulu.

25. Baada  ya  pale  zikaanza  propaganda  za  uongo  zikimuhusisha  hadi  mke  wangu  eti  kanizuia.

26. Naomba  watanzania  wajue  kuwa  mke  wangu  hakuwahi  kunizuia  kwa  lolote, lkn  hata  angefanya  hivyo  sio  mbaya  maana  hata  yeye  ni  mwanaharakati  mwenye  uchungu  na  nchi  hii.

27. Mke  wangu  aliwahi  hadi  kuumia  wakati  akipigania  ukombozi  wa  nchi  hii.....Lakini  sio  mbaya, familia  yangu  imezoea  propaganda.

28. Kikubwa  katika  harakati  ni  credibility  ambayo  lazima  uilinde  na  mimi  sitaki  jina  langu  liharibiwe  na  ni  haki  yangu.

29. Maslah  mapana  ya  taifa  ndiyo  yaliyotufikisha  hapa  na  sio  maslahi  binafsi.

30.Lowassa  na  wapambe  wake  ni  waongo  maana  hakuna  hata  kipengele  kimoja  walichokitekeleza.

31. Tulitaka  hao  wabunge  50  waje  kwanza  kabla  ya  mchato  wa  uteuzi  ccm

32. Napinga  kuchukua  makapi  ya  CCM  kuyaita  MTAJI.

33.Mtu  kama  Sumaye  ni  FISADI  na  nilikuwa  siongei  naye

34. Sumaye  aliwahi  kusema  CCM  wakimchagua  Lowassa  atahama  chama. Leo  Lowassa  kawaje  msafi??

35. Tulitaka  Mtaji  toka  kwa  Lowassa  na  sio  MAKAPI

36. Wenyeviti  walioletwa  na  Lowassa  ni  MZIGO  na  namjua  vizuri. Akithubutu  kunijibu  ntamwaga  UOZO  wake  wote

37.Nani  asiyejua  Guninita  pia  ni  mzigo??

38:  Nawataka  viongozi  wangu  wanijibu  ni  mtaji  upi  walioupata  toka  kwa  Lowassa.

39. Mimi  ni  Padri  Mstaafu, sipendi  siasa  za  uongo.

39. Ukisema  unataka  kuiondoa  CCM  ni  lazima  ujikumbushe  misingi  ya  CHADEMA  ambayo  ilikuwa  ni  uadilifu. Leo  chadema  hii  ina  Uadilifu  gani??

40.  Namshangaa  sana  Lowassa  eti  kusimama  mbele  ya  watu  akijinasibu  kuwa  ni  msafi.....kwamba  mwenye  ushahidi  aende  Mahakamani. Ni  dhambi  kupotosha  watu.

41. CCM    hawana  ujasiri, ni  waoga  na  ndiyo  maana  wamewalea  watu  kama  akina  Lowassa

42. Ukitoa  kinyesi  chooni  na  kukipeleka  Chumbani  maana  yake  hata  chumba  chako  ni  CHOO  na  kitakuwa  kinanuka  zaidi  kulicho  choo  cha  kawaida

43.Mimi  nilikuwepo  wakati  sakata  la  Richmond  likijadiliwa.Mimi  nina  ugomvi  wa  muda  mrefu  na  Lowassa.

44.  Mwaka  2010  mimi  nilimtaka  Lowassa  atangaze  Richmond  ni  ya  nani.

45. Leo  tena  namtaka  Lowassa  namtaka  Lowassa  atoke  hadharani  atangaze  Richmond  ni  ya  nani.  Unaposema  ni  ya  mkubwa, atuambie  mkubwa  gani

46. Ukitaka  kuijua  Richmond  rejea  Ripoti  ya  Mwakyembe. Nampongeza  Mwakyembe  na  Sitta  kujitokeza  hadharan  kuusema  ukweli.

47. Siku  moja  kabla  ya  ripoti  kusomwa, nililetewa  Rushwa  ya  milioni  500  ili  tukaupindishe  ukweli  bungeni  lakini  nilikataa

48. Ripoti  ya  mwakyembe  iliamua   mambo  mawili,  moja; Lowassa  ajipime  au  bunge  lijadili  na  lichukue  ripoti.  Lowassa  kuona  hivyo  akaamua  kukimbilia  kujiuzulu  kukwepa  aibu  ya  kung'olewa  na  bunge

49:  Lowassa  haaminiki, ni  muongo  na  hastahili  kuwa  Rais  wa  nchi....

50.  Lowassa  ni  FISADI  na  kama  mimi  ni  muongo  ajitokeze  hadharani  akanushe

51. Anasema  Lowassa  ataleta  maji, mbona  jimbo  lake  la  Monduli  halina  Maji???

52.  Mnasema  Lowassa  kaanzisha  shule  za  kata, iv  mjua  msingi  wa  shule  za  kata?  waandishi  rudini  shule  mkajifunze  upya.

53.Nilifanikiwa  kuijenga  Chadema  na  ikawa  tumaini  jipya  la  watanzania.....Vijana  wangu  wa  Chadema, naomba  niwe  mkweli  propaganda  imekivamia  chama.

54.  Inasikitisha  kuona  CHADEMA  inajaza  mabasi  pale  jangwani  badala  ya  watu.....alafu  mnawadanganya  watu  eti  ni   MAFURIKO

55.  CHADEMA  ya  kipindi  changu  ilikuwa  inakemea  Rushwa. Niambien  leo  chadema  watasema  nini  kwenye  majukwaa?

56. Mnaomtetea  Lowassa  na  nyie  jitokezen  hadharani...mimi  nasema  kwa  sababu  nina  ushahidi  na  sio  lazima  ushahidi  huu  niupeleke  mahakamani.

57. Wenye  uwezo  wa  kumpeleka  Lowassa  Mahakamani  ni  Serikali, na  mwakyembe  alisema  juzi  kuwa  kesi  ya  jinai  haina  kikomo, mtu  anaweza  kushitakiwa  muda  wowote

58. Sitaki  kuingila  swala  la  Babu  Seya, lakini  waliolawitiwa  ni  watoto  waliokuwa  chini  ya  umri. kwa  nini  haki  yao  ipotee?

59.  Rais  hana  mamlaka  ya  kumtoa  Babu  Seya. Lowassa  asiwadanganye.

60.  Kuhusu  swala  la  Masheikh, Sumaye  ndiye  aliyeamuru  mapolisi  wavamie  misikiti  wakiwa  na  mbwa......Watanzania  msikubali  kudanganywa. hizo  ni  propaganda  za  wasaka  urais

61. Masikubali  Rais  Muongo  na  mimi  naapa  ntapiga  kelele  kila  kona  kumpinga  Lowassa.

62.Lowassa  alipokuwa  waziri  mkuu, matatizo  yanayotokea  leo  hayakuwepo?  mapigano  ya  wakulima  na  wafugaji  hayakuwepo?

63.  Lowassa  akiwa  waziri  mkuu  alisababisha  migogoro  mizito  sana  kati  ya  monduli  na  karatu.  Rais  wa  aina  hii  wa  nini?

64.  Naomba  nisiongee  mengi  kwa  sababu  ntakosa  ya  kusema  siku  nyingine.....Nawataka  Lowassa  na  Sumaye  wajitokeze  kunijibu.

65. Siku  nyingine  ntakuja  kuongelea  kuhusu  hisa  za  Lowassa  kwenye  makampuni

66.  Nahitimisha  kwa  kusema  kuwa  Nimestaafu  siasa  na  sina  chama  lakini  nina  nchi, hivyo  ntaendelea  kuwatumikia  watanzania  kwa  jinsi  mungu  alivyonipa  vipawa

67.  Narudia  tena, Sina  chama  na  sitajiunga  na  chama  chochote.

Waandishi  wanauliza  Maswali:
Mwandishi:  Umesema  ujiungi  na  chama  chochote, utawasaidiaje  watanzania?  Rais  gan  unamuunga  mkono?

Mwandishi  Guardian:  Ulisema  Lowassa  atakuwa  assert  kama  atakuja  na  wabunge  na  hao  wenyeviti.  Je  angekuja  kama  assert  ungeyasema  haya  yote?

Mwandishi  binafsi:  Umesema  waliohamia  Chadema  ni  makapi.  Mwaka  1995  Uliihama  CCM,   ukahamia  chadema. Je  na  wewe  ni  KAPI?

Mwandishi-Azam:  Umetangaza  kustaafu  siasa, lakini  bado  unakadi  ya  CCM  na  CHADEMA?  Je  utazirudisha?

Mwandishi  Blog:  Unaonekana  baada  ya  chedema  kukutosa  ndo  maana  unamshambulia  Lowassa, je  ni  kweli?

Majibu:
1. Kadi  ni  mali  zangu  na  siwezi  kuzirudisha. Ya  chadema  nimeilipia  miaka  20.

2. Kuhusu  urais, mimi  sijagombea  urais  na  sikuchukua  fomu.  sasa  kwa  nini  nikasirike  kisa  wamempa  Lowassa?
Sina  ugomvi  na  Mbowe  na  nakumbuka  alinisaidia  nyumba

3.  Mimi  sio  KAPI....Ili  kuujua  ukweli  unahitaji  kutumia  kigezo. KAPI  ni  yule  aliyekataliwa  na  chama  flani, mimi  sikuwahi  kukataliwa.  Sikuwa  na  uchafu  wowote  wakati  naingia  CCM.

4.  Lowassa  ni  mzigo  tu  hata  kama  angetuletea  hao  watu  wake.....Lowassa  ana  makandokando  mengi. Angetuletea  hao  watu  ndo  tungeamua  tumpokee  au  tusimpokee

5.Mimi  sina  chama  na  sitampigia  kampeni  mtu  yeyote. Mimi  nimefanya  utafiti  kwa Lowassa  pekee, kwamba  taifa  litapata  madhara  gan  Lowassa  akiwa  Rais.....Lowassa  ni  Fisadi.

-Kazi  yangu  leo  ilikuwa  ni  kuwaambia  watanzania  waachanane  na  ushabiki.Ukihamishia  CHOO  chumbani, manake  harufu  itahamia  huko.
-Chadema  ya  leo  kwa  sasa  imetekwa  na  Lowassa  na  hawawezi  tena  kuongelea  Ufisadi

Maswali  ya  nyongeza

1.Umesema  waliohamia  chadema  kwa  sasa  ni  sawa  na  mfano  wa  Choo. Je, wewe  ulipohama  hukuwa  choo?  kwa  nini  wewe  uliweza  kukibadili  chama  halafu  akina  Lowassa  washindwe?

Jibu:  Wakati  mimi  nahama  sikuwa  mchafu  kama  hawa

Alhamisi, 23 Aprili 2015

Thursday, 23 April 2015
DAUDI MRINDOKO ASHAWISHIKA NA KAKUBALI OMBI LA WANANCHI WA JIMBO LA MOSHI MJINI KUGOMBEA UBUNGE 2015

Yafuatayo ndio maelezo yake haya:

"Kwa nianze kwa kumshukuru mwenyezi Mungu anawezesha yote na kutujalia uhai...

"Waheshimiwa Mabibi na mabwana,vijana na wazee,watoto na wakubwa, Baba zangu na mama zangu na wanadau wote wanaoishi Moshi na wenyeji wa Moshi walio ndani na nje ya Moshi. Mimi mtoto wenu,mdogo wenu na  Kijana wenu.  DAUDI BABU MRINDOKO

"Nina heshima kubwa na unyeyekevu kwenu ,Pia nawashukuruni sana kwa kunishawishi niweze kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya ubunge wa jimbo
la Moshi Mjini katika uchaguzi mkuu 2015,nafasi ambayo Ubunge ! ambayo mimi mwenyewe kwa tafsiri ya Ubunge yaani utumishi,mtetezi,msemaji,mwakilishi n.k
katika baraza la kutunga sheria na katiba yaani Bunge, na katika tafsiri hii ya majina ya kazi hii lazima mtumishi awe mkweli,muwazi na aliyeweka mbele kwanza maslahi ya walio mchagua.
"Waheshimiwa Mabibi na mabwana, vijana na wazee, watoto na wakubwa ,Baba zangu na mama zangu Kunishawishi kwenu Kulinifanya niwe kimya kiasi na nikiwa najiuliza maswali mengi kichwani ! Lakini maswali makubwa yalikuwa 3 (a) Nashawishiwa na jamii nichukue fomu kwa kuwa mimi ni kijana mwenywe uwezo wa kuifanya kazi hii?

(b)Nashawishiwa kwa kuwa kijana niliozaliwa na kuelimishwa na wanao nishawishi? yaani wanachi wa Moshi mjini na ndio wananitambua tabia na uwezo wangu wa kikazi.

"Swali lingine nililojiuliza ni: Hivi mtoto au kijana mwenye adabu ,Nidhamu na heshima kwa wazee na wakubwa zake walikuwa katika jamii wakimteua au kumtuma kufanya kitu au jambo tena kwa faida na maslahi ya jamii,itakuwa vema kijana huyo akatae? au asikubali kutumwa huko?
"Baada ya kujiuliza maswali hayo na mengineyo nimepata jibu ambalo ni:
         NAKUBALI WITO WENU NA USHAWISHI WENU
Kuwa nitachukua fomu ya kuomba kugombea Ubunge 2015 jimbo la Moshi Mjini. Mmenishawishi nami nashawishika na kuthubutu kuchukua fomu ya kugombea ubunge,kwa kuwa siwezi kuwa mvunjifu au mtovu wa adabu kukataa wito na ushawishi wenu ambao wazee wangu,vijana  wenzangu,mama na baba zangu wa Moshi mjini
mmeniteua kwa kunishawishi niweze kuja kuwa mtumishi wenu mbunge.

"Kwa kuwa mmenizaa, mmenilea, mmenisomesha mpaka elimu ya juu na mmenishawishi kwa kuwa mnaniamini mimi ni mmoja wenu katika maisha ya kila siku katika jamii yetu Moshi,yanafahamu wazi mahitaji yetu,kero zetu na kipi jamii yetu haitaki na kipi? Jamii yetu inataka hapa jimboni Moshi Mjini,Marekebisho gani ?yanatakiwa hapa Moshi mjini
ili palete tumaini jema na maana kamili wa wakazi wote jimboni hapa Nayafahamu yote.
"Nanyi mmemshawishi Kijana Daudi Babu Mrindoko,mtoto wenu  kwa hakika mmetuma mtumishi anayeguswa na yanayowagusa, anayekerwa na yale mnayokelwa ! anafurahishwa na yale mnayofurahia
"Kwani mwenzenu katika jamii jimboni Moshi mjini.
Nawashukuruni sana na Asante sana kwa Kunishawishi, Nimeshawishika Nangojea wakati ukifika nami nifuate taratibu zote za kuchukua fomu kupitia Chama tawala"

"NAKUBALI NITACHUKUA FOMU 2015,KWA NIA YA USHIRIKIANO WETU TULETE MABADILIKO MOSHI MJINI YENYE MASLAHI KWA WOTE"
               
                       Mungu Ibariki Tanzania!

Usikose kujiunga nae at www.facebook.com/mrindoko.mwidadi

Jumapili, 12 Aprili 2015

Leo Jumapili tarehe 12/04/2015, mwenyekiti wa taasisi ya wazalendo Taifa Ndg. Chief Daud Mrindoko ameyasema hayo katika uzinduzi wa Album ya Victor Mbagga ijulikanayo kwa jina la FURAHA KUWA NA YESU.

Fuatilia hotuba ya Chief Daud Mrindoko kuanzia mwanzo na mwisho:

HOTUBA YA MH. CHIEF DAUD BABU MRINDOKO KATIKA UZINDUZI WA ALBUM YA VICTOR MBAGGA TAREHE 12/04/2015: (UMOJA HOSTEL) MOSHI-KILIMANJARO.

Ndg. Victor Mbagga(mwibaji),
Ndg. viongozi wa dini,
Ndg. viongozi wa kwaya,
Ndg. waimbaji mbalimbali,
Wageni waalikwa, mabibi na mabwana:
Bwana yesu asifiwe, tumsifu yesu kristu;
Assalam Aleykum...!!!

Ndg. wageni waalikwa..

Naomba tuanze kumshukuru M/mungu kwa kutupa afya na uzima  na kutuwezesha kukutana katika hafla hii ya uzinduzi wa Album ya kwaya ya ndg yetu. Kwani sio kwa ujanja wetu bali ni kwa nguvu zake M/mungu mwingi wa rehema.

Ni furaha yangu kuona wote tupo hapa na tumejumuika kwa umoja katika uzinduzi huu kwani ni furaha sana kwasababu ya amani aliyotujalia Mungu aliyetuwezesha kukutana hapa na kujumuika sote kwa pamoja.

Nilipopata mualiko huu kweli nilistuka sana kwakuwa sikutegemea mimi kuweza kupewa heshima kama hii, kwakuwa kuna watu wengi sana wenye uwezo mbalimbali na vyeo ambao wangeweza kualikwa kuwa miongoni mwa wageni rasmi. Lakini naamini mmenipa heshima kubwa sana kuweza kunialika mimi hapa na kujumuika nanyi ingawa sistahili. Basi kutokupenda kwenu makuu mkaona mnialike mie kuwa mgeni rasmi. Nawashukuru sana, kwani Mungu huvichagua vinyonge ili kjwashusha wenye nguvu, utukufu wake uonekane mbele za watu.

Ndg. wageni waalikwa, lengo la kuwa hapa ni kushiriki katika uzinduzi wa Album ya "FURAHA KUWA NA YESU" ya mwimbaji wetu Victor Mbagga.

Ndg. wageni waalikwa, kwaya hii ni yetu sote hivyo tujitahidi kuweza kuwawezesha hawa wanakwaya wenzetu kwa namna mbalimbali ikiwemo kwa kununja Album zao na kazi zao. Kwani kwa kufanya hivyo utapata faida kubwa kwa kuwa yale yanayo imbwa ndani ya nyimbo hizi za Injili ni ibada tosha na inatufanya tuweze kumwabudu na kumsifu Mungu wetu muumba wa mbingu na ardhi.

Vilevile tutakuwa tunawapa fursa wenzetu wanakwaya hawa kujiajiri na kuweza kuweza kujipatia kipato zaidi, kwani ukinunua kazi zao ndio wanajipatia kipato na fedha kuweza kuboresha zaidi na zaidi kazi zao za sanaa.

Ndg. wanakwaya, mimi binafsi naahidi niitawaunga mkono katika kazi yenu hii, na njtanunua kazi yenu. Lakini ninawaomba sana mjitahidi kuwa wabunifu ili kuboresha kazi zenu ziweze kushindana katika soko la kimataifa na kukubalika na watu wote, ili muweze kufikia katika viwango vya kimataifa lazima mkubali kuboresha kazi zenu na mfanye kazi kwa bidii kweli kweli ndio mtaweza kufanya vuzuri. Lakini mkibweteka hamtoweza kufanya vizuri katika anga za kimataifa.

Ndg. wageni waalikwa, ningependa kupitia jukwaa hili niweze kuwaomba mliombee taifa amani kwasababu tunaelekea katika kipindi cha uchaguzi mkuu wa serikali kama mjuavyo uchaguzi mkuu huwa unagubikwa na hali ya kutishia uvunjifu wa amani, basi tuliombee sana taifa letu na pia tumuombee raisi wetu Prof. Jakaya M. Kikwete aweze kumaliza kipindi kilichobakia salama na tupate Rais mwingine mchamungu, mchapa kazi, mmoja wetu kutoka katika watu wenye utu wa kweli na uzalendo halisia.

Aidha, tupate wabunge na madiwani wenye kulijali taifa katika maeneo husika.

Kwakuwa, wabunge na madiwani hutokana na watu, hupendekezwa, kushawishiwa na kupigiwa kura na watu. Hivyo, suala la kupendekezwa na kushawishiwa linaanza kujitokeza ingawa muda bado. Mfano katika gazeti la Mwananchi la tarehe 08/03/2015 nilishangaa kuona watu Moshi manispaa wakinipendekeza kugombea kiti cha ubunge kwa kuongelewa hata kupigiwa simu na baadhi ya watu kunishawishi moja kwa moja. Walatini husema "VOX POPULI EST VOX DEI" yaani sauti ya watu ni sauti ya Mungu. Hivyo, nitajaribu kusikiliza sauti ya Mungu. Ndugu zangu, naomba sala zenu kwa mawazo, maneno na katika nyimbo zenu. Mungu atukuzwe!!!!

MWISHO:
Ndg. zangu mwisho kabisa naomba niwapongeze kwa mara nyingine tena wale wote waliohusika na maandalizi ya hafla hii na pia kuipongeza kwaya yetu hii na mwimbaji wetu Victor Mbagga, narudia tena kuwa nitawaunga mkono na tutashirikiana sote kwa pamoja kuhakikisha kwaya yetu hii inafanya vyema katika tasnia ya nyimbo za injili.

Ninawashukuru waimbaji wengine wote toka Kenya, Congo na Tanzania(wakiwemo Kilimanjaro, Arusha na Dsm).

Mungu awabariki sana,

Asanteni sana kwa kunisikiliza.

Chief Daudi Babu Mrindoko.

Jumatatu, 30 Machi 2015

Mabalozi wa Usalama Barabarani wafanya Kikao Kujadili Suala la Ajali nchini. Na Kupata Semina Ya Bima kwa Mtaalam Bw. Mwandu

Shukrani

 KWA RSA WOTE.

Kwa namna ya pekee kabisa na moyo wa dhati natumia fursa hii kuwashukuru RSA wote ambao mmejitoa kwa moyo mmoja kuhudhuria mkutano wa leo war obo mwaka uliofanyika Police Officers’Mess Jijini Dar es Salaam. Kwa kweli, japo sikuwepo nanyi, lakini nimehamasika sana, kila nilipoona picha zenu na kusikia sauti zenu toka kwenye recordings mlizokuwa mkizituma niliona nimekosa kitu kikubwa sana. Mahudhurio yenu yamenifanya nijiulize maswali mengi sana, kuwa wakati nimejikuta nikitokwa na machozi, lakini tofauti na machozi mengine haya yalikuwa machozi ya furaha.Binafsi kama moja ya waanzilishi wakubwa wa mtandao wa RSA nimefarijika sana kuona kwamba kumbe kitu tulichokianzisha kama utani vile sasa kimeshika kasi na kukita mizizi mioyoni mwa watu kiasi kwamba kinakuwa cha kitaifa. Pale unaposikia watu wametoka Mwanza, Arusha, Mbeya, Songea nk kwaajili ya kuja kuhudhuria mkutano wa RSA tu then inakubidi utafakari mara mbili tatu commitment watu waliyonayo katika kuhakikisha kuwa kuna usalama barabarani. Kila mmoja wetu naomba atafakari hili na mkutano wa leo uwe chachu mpya ya kuongeza mashambulizi dhidi ya ajali. Unapoona watu na vyeo vyao tena vikubwa kabisa kama vile Wakurugenzi wa mashirika mbalimbali ya umma na binafsi, watendaji wakuu, askari wav yeo vya juu kabisa, watu wazima kwa umri nk wanajiunga na rsa na wanakubali kukaa kwenye mkutano kuanzia saa 8 mchana hadi saa 2 Usiku hapo ndipo utakapoona umuhimu wa hili jambo.Hawa watu sio kwamba hawana kazi za kufanya, je ni nini kina waleta rsa? Wala hatugawi hela, wala rsa hakuna posho, wala hakuna vyeo vya kisiasa lakini watu hawaachi kuja. Nimeguswa Zaidi na rsa wenzetu ambao pamoja na kupata msiba leo hii bado waliweza kufika, na kuna rsa mwenzetu pamoja na kuwa na msiba huko Iringa wiki hii bado aliweza kupanda ndege na kufika Dar ili kuwahi mkutano. Kuna watu wamekodi vyombo mbalimbali vya usafiri ili mradi tu wamekuja kwenye mkutano wa RSA.
Hakika nawapongezeni sana. Mkutano nimeambiwa umeenda kwa utulivu sana, mada ya bima wengi mmeifurahia na kuonesha kuitaka Zaidi. Nadhani mtatupa feedback hapa. Wengi mmekaa hadi mwisho wa mkutano, mmenunua fulana za RSA na ktoa michango mbalimbali ya mawazo kwaajili ya kuboresha RSA. Mimi kama kiongozi ninaona nawiwa deni kubwa kwenu kuendelea kuratibu RSA kutoka popote duniani, na sasa ninaona kuwa juhudi zangu si bure haziishii patupu.Ninawashukuruni sana kwa kutambua michango ya RSA mbalimbali katika kuimarisha RSA kwa kuanzia na admins, mimi mwenyewe hususani, Mwenyekiti, Katibu, Kamati tendaji, RSA mmoja mmoja, Kamati ya zawadi na tuzo nk. Kwa namna ya pekee nazidi kumpongeza na kwa kweli nashindwa niweke neon lipi ili niwape uzito unaostahili, Kamanda Mohammed Mpinga na Johansen Kahatano kwa moyo wao wa dhati wa kuwa tayari kufanya kazi na RSA. Tangu, Mwaka 2014 December, tulipokutana mara ya kwanza kwaajili ya kuwa na mkutano wa kwanza na kuifanya rsa isimame kama taasisi, Mpinga na Kahatano wameendelea kuisapoti RSA kwa hali na mali. Wameendelea kufanya kazi na sisi bega kwa bega, wameendelea kutufadhili kutumia ukumbi wa polisi pamoja na vifaa vingine kufanyia mikutano. Hii sasa ni changamoto kwetu RSA kuweza kujiimarisha ili kujitegemea, tuwe na ofisi zetu hata kama sio ofisi kama ofisi basi uwezo wa kuwa na fedha kwaajili ya kukodi ukumbi wa mikutano, kuendesha mikutano yetu na kampeni zetu mbalimbali. Naamini kwa umoja huu na ushirikiano wetu tutafika na tutayatimiza yote haya.Lengo letu ni kukabiliana na hili jinamizi la ajali kwa kusisitiza utii wa sheria bila shuruti. Shukrani za pekee ziwaendee Adam Phillip-Mwenyekiti wa Kamati ya Muundo wa Kitaasisi na Bw. Justine Mwandu kwa mawasilisho yao ya leo. Kuanzia sasa RSA natangaza kauli mbiu mpya ya RSA. Kauli mbiu yetu mpya ni “USALAMA BARABARANI NI HAKI NA JUKUMU LETU SOTE” Kwa maana ya kwamba kila mtu ana haki ya kuwa salama barabarani na pia ni wajibu kila mmoja wetu kuhakikisha barabarani kunakuwa salama. Hivyo ningependa hata salama yetu iwe “Usalama barabarani”Jibu: “Ni jukumu langu”. Kila mmoja aseme hivi moyoni mwake na kwa kinywa..Pia palikuwa na Semina za Kampuni za Bima;- Leo RSA mtapigwa shule ya maana sana kuhusu bima, ni nafasi yenu kuwahi ili kupata uhondo wa somo la bima toka kwa nguli wa tasnia ya Bima ambaye uzoefu wake wa kinadharia na kivitendo kwa muda mrefu hauna chembe ya shaka kuwa anaifahamu vema tasnia hiyo. Wewe jipange tu na maswali yako, tumempa muda wa saa nzima kufanya wasilisho lake na kujibu maswali. Kwa ufupi tu Mr. Mwandu ni mwalimu(lecturer) na mtendaji (practitioner) ktk tasnia ya masuala ya bima. Amepata kufundisha watu wengi darasani na pia kuwasimamia kama mkuu wa kazi na mkuu wa shirika la bima la taifa. Mr. Mwandu ameshiriki ktk mageuzi ya sekta ya bima nchini Tanzania hivyo ukikosa somo la leo utakuwa umekosa mambo mengi sana. Jongea ukimbini mara moja kwani wakifika watu 20 tu mkutano unaanza.



Pia Mwenyekiti alikumbushia ya kikao cha Mwaka jana December; -MOJA YA ILIYOWAHI KUWA MIJADALA MIREFU SANA YA RSA KUHUSU NOTIFICATION KATI YA JUNE 20-24, 2014SWALI/HOJANaomba kukumbushwa hivi ni kwa nini ikiwa na kosa la barabarani traffic police wanangangana ukifika kosa na ilipe fine hapo barabarani ... Na ukiwaelezea options zilizopo ktk notification wana kuwa wakali, na kusema uache leseni ama gari ....Kama tatizo ni watu kuingia kiti ni basi si notification zibadilishwe ....maana sidhani Kama ni sawa maduhuli ya serekali kukusanywa maporini na wasio hata watu za fedha! Fungo Augustus nisaidie kwenye hili, maana ukigoma kutoa hela ya soda/chai unalazimika kubishia notification na government revenue receipts..... #‎tubadilike•        John Seka Hahaaa. Vile vitabu sio vya ukweli. Wengi wamechongesha!! Ila jibu zuri anaweza kutupa mkuu wa trafiki kamanda Mohammed Mpinga•        Asina A Omari John Seka leo mie nimegombezwa sana baada kusema niandikie nielekeze nikalipie wapi ....na sio Mara ya kwanza ....mie naomba kamanda Mohammed Mpinga anipe trusted status na cheti kuwa nikifanya kosa nitaenda lipia kwa OCD anaye husika ....it feels soo funny kulipia hela barabarani. Leo mie wamenirudishia hela zangu maana niliwaambia hatuachi leseni wala nini na notification iambatane na grr Kama wako busy kukusanya maduhuli porini! Kwa hasira waka nirushia hela zangu na kusema mie sio mlipaji ....alafu hawaja vaa number zao! Yaani hizi tochi naomba nihadithie siku nyingine habari yake ...kamanda hao watu wenu barabarani wanatugeuza mitaji na tochi zao!•        Prudens Rweyongeza Mimi utaratibu wangu siku hizi silipi pesa barabarani and after all si lazima niwe na pesa kwenye wallet! This needs clarification Asina A Omari•        Asina A Omari Si ndo hapo! Pia what if na kataa kosa? Prudens Rweyongeza•        Angelo Rumisha Maana ya kulipia notification maana yake unakubali kosa. Lakini notification siyo lazima ulipa on sport. Kuna sheria na utaratibu wa notification ni mzuri ila changamoto iko kwenye usimamizi wa sheria•        Fungo Augustus Ngoja na mimi niseme. Ni kweli utaratibu wa kulipia faini barabarani kwa askari ilhali askari wenyewe hawana risiti unakera sana. Afande Mohammed Mpinga alishawahi kulikubali hili hapa na kueleza kuwa kwa kawaida ilitakiwa polisi wasipokee kbsa hizo pesa kama ingekuwa uamuzi wake na akasema kuna utaratibu unafanyika kuhakikisha polisi hawapokei hizo hela au wengine wanavyotaka, zitumike efd.•        Fungo Augustus Ile notification ina sehemu mbili moja ya kukubali kosa na kulipa hapo hapo au kulipia kituoni na ya pili ni kukataa kosa hivyo upelekwe mahakamani. Wengi huwa tunaopt kukubali kosa sasa shida inakuja pale tunapotakiwa kulipa kwa wale askari ambao hawana risiti za exchequer unalipishwa tu na kupewa notification. Na hatuna uhakika zile pesa hufikishwa kwa mhasibu au hata km vile vitabu ni halali. Lkn jambo jingine hata ukaamua utalipa kituoni? Askari ataaminije kuwa utacomply hivyo akuachie uende? Ndo maana ukiinsist wengine watataka uache leseni au uliache gari au ukalipaki polisi then ukalipe kisha uje uchukue gari. Hapa ndipo kero kuu ilipo bi Asina A Omari sasa mimi huwa naamua kulipa then nachukua jina na namba ya askari na kituo nikirudi toka safari huwa nafuata risiti yangu.•        Mohammed Mpinga Nipo likizo sikuweza kuuona mjadala huu mapema. Nashukuru kwa maelezo ya Fungo Augustus naona alinielewa vizuri katika maelezo yangu ya nyuma - Ahsante sana. Utaratibu wa Electronic ticketing uko katika mchakato unakuja. Sikatai kunaweza kuwa na notification fake kama ambapo hata GRR inaweza kuwa fake lakini ieleweke notification (PF 101) ni doc ya serikali hivyo iaminiwe katika ulipaji na risiti yako utaipata tu baadae tatizo madereva wengi wanakubali makosa lakini wanaweka kisingizio cha kutaka risiti ili wasilipe faini. Mabishano yanakuwa makubwa na kuchukua muda, 'kwanza ni fake mbona ya 2011, speed sio yangu, alama iko wapi, mbona mko polini, rushwa tu, mnanionea, hamnijui mimi, nampigia .... utakoma n.k.' YOTE hii hupelekea baadhi ya askari kuamua kuwaachia. Kwa kweli ni usumbufu usio wa lazima na ndio matunda ya kuto tii sheria - kuepuka yote haya tuzingatie UTII WA SHERIA BILA SHURUTI.•       
Asina A Omari Asante kwa maelezo Fungo Augustus nadhani maelezo yako ni vema sie madereva wote tukayaelewa. Ila reservation yangu ni moja tu kwamba utaratibu huu unassume nimetembea na hela ....pia unassume kuwa mie naenda kukaa mahali maana na weza kuwa naenda naminywili kusalimia narudi same day sasa naambiwa nirudie receipt kesho why? Najua kuwa wengi wetu tutaingia mtini tukiwa na utaratibu wa kistaarabu wa Kutii sheria bila shurti na kuaminiana ....so hizo electronic ticketing/citations mie nazingojea kwa hamu sana! Kamanda Mohammed Mpinga tatizo sie raia wengi tunaanza kubembeleza na kujijengea wenyewe mazingira ya kuombwa hela ya chai ...Mara nyingi askari ana kuwa ana reciprocate tu nia ya raia ya kusuggest atoe kitu kidogo asemehewe. Sasa sie ambao hatujawahi master the art ya kubembeleza Askari barabarani ukikutana na Askari ananza kuona unamdharau kisa baada ya kujua kosa umesema niandikie, kumbe we una taka tu umalize uendelee na shughuli zako. Habari ya kupiga simu kwa mtu kisa umekamatwa na traffic ni TABIA MBAYA (unless kuna shida nyingine zaidi ya kosa ulio fanya). Ila pia kamanda wasihi Askari wasitubambikie makosa ya ku overspeeed maana haiwezekani gari kadhaa zote zina enda speed hio hio sehemu hio hio imepimwa na mtu huyo huyo ....probability na margin of error hapo inakuwaje!?•        Janemary Ruhundwa Nami nikushukuru Kamanda Mohammed Mpinga kwa kutukumbusha utaratibu. Nakubaliana na wewe kuwa ni muhimu kuacha leseni endapo umekutwa na kosa na hauna uwezo wa kulipa on the spot ili watu wasiingie mitini. Tatizo nililokutana nalo mimi mara kadhaa ni kuwa ninapossugest niache leseni Askari wanakataa na wanadai nikaache gari kituoni hadi nitakapopata pesa ya kulipa fine. Na maelezo ni yale yale kuwa naweza kuingia mitini nisirudi kuchukua leseni yangu.•        Janemary Ruhundwa Kwa ufahamu wangu ni kuwa hizi leseni mpya zina information zote za muhimu zinazonihusu na endapo nitadefault kuna mengi tu yanaweza kufanywa kunilazimisha nikalipe hiyo fine. Kwanza kuna namba yangu ya simu kwenye system, pili hii leseni ipo linked na TIN yangu so TRA wanaweza kuwa notified kuwa nimedefault nikakamatwa wakati wa kulipia Motor Vehicle licence nk. sasa nashindwa kuelewa kwa nini leseni isiwe dhamana tosha endapo nashindwa kulipa on the spot. Na ninachoshangaa zaidi ni kwamba Kamanda Mpinga ulituambia kuhusu hii option ila Askari wako huko njiani hawana taarifa nayo kabisa, hasa hawa wa barabarani za mijini. Elfu 30 si ndogo na si kila mtu anatemea nayo kila wakati. naamini ndio maana hata notification imetoa option ya kulipa fine within some days.•        Janemary Ruhundwa Na pia naungana na Asina kuwa kuna makosa ni ya kubambika kabisa hadi unashangaa. So si kuwa watu hatutaki kutii sheria kuna muda makosa yanaibuliwa hata unashangaa yametokea wapi.•        Asina A Omari Janemary Ruhundwa umenikumbusha Siku nimekamatwa na askari ananiuliza kwanini gari yako chafu sana ...... Alafu ni saa mbili asubuhi Siku ya jumapili ....yaani Nilishiwa nguvu ...! Mie nadhani the best method ni kuharakisha e-ticketing maana kuacha leseni mbwewe wakati naenda Arusha nayo ni issue! Ndio notification nitakuwa nayo but jamani wengine leseni wanatumia Kama ndio Kitambolisho! Technolojia ya e ticket wala sio ngumu jamani na leseni zina bar code ....mie nasikitikia mapato ambayo serekali inakosa toka kwa wanao amua kubembeleza kuliko kulipia fine maana logistics za fine ni usumbufu!•        Mohammed Mpinga Janemary Ruhundwa ni kweli CDL zetu zina information nyingi sasa tukisuburi mpaka utakapokwenda kulipa MV licence miezi 10 ijayo ndipo ulipe faini yetu sijui itakuwaje. Hata hivyo utaratibu wa anuani utatusaidia baadae kuwekewa bill yako nyumbani kwako. Ni kweli kuna baadhi ya madereva wanaacha leseni zao Polisi, ni kwamba askari anapochukua leseni au kubaki kituoni, dereva huyo huenda mkoa mwingine anaripoti Polisi amepoteza au kuibiwa na anapokwenda TRA anapata nyingine ! kwa hiyo harudi tena Polisi kulipa faini na leseni inabaki kituoni (bado hatuna utaratibu mzuri wa kufuatilia kwa wanao pata leseni baada ya kupotea au kuibiwa) - zipo leseni nyingi kwa sasa vituoni zilizoachwa na madereva hawatokei kuzichukua.•        Janemary Ruhundwa Duuh hao watu wana mahesabu mahali kweli. Fine ya elfu thelathini ukimbie ukaanze process ya kuomba leseni mkoa mwingine kisha uilipie 40,000! Labda kama wana fine kubwa. Na pengine kuna haja ya kutofautisha hapo, kiwango cha fine, probability ya mtu kutorudi (mnaweza kuangalia masuala kama yale mnayoangalia wakati wa kuwapa watu dhamana, ukiondoa habari za utambulisho Wa serikali za mitaa of course). Yaani akili yangu inagoma kuamini na kuelewa kuwa mbadala Wa kulipa fine ya Tshs 30,000 ni kuacha gari kituoni. Hata hizo e ticket zikianza bado kuna issue ya mtu kuwa na hela hapo hapo anapokamatwa.•      
Asina A Omari ,Janemary Ruhundwa umeona ambavyo tunatofautiana akili ….maana usumbufu wa kutafuta leseni mpya khaaa!!! anyhow mie nilisha sikia mahali mtu analipa rushwa 20m ili asidaiwe deni la 35m badala ya kupunguza deni! hilo la kuwa na hela hapo hapo nalo ni tatizo ndio maana mie am all for niambiwe nikalipe wapi na nisipo lipia nikutane nayo TRA …mbona kwa nchi nyingine ndio hivyo tunaishi ….utakimbia deni weeee ipo siku unakutana nalo na penalty juu!!! hii italeta efficiency katika ukusanyaji lakini pia katika mapato kutoingia mifukoni mwa watu! Ifike mahali tuwe responsible citizens kwa kutii sheria bila shurti, ila na mamlaka nazo zitusaidie kutii sheria.•        Janemary Ruhundwa Ha ha haaa, hizo ndio zinaitwa akili matope. Mie nakubaliana na wewe, tukalipe mahali maalum, na tupewe muda wa kulipa kama hatuwezi kulipa siku hiyo hiyo. Penalty ya kudefault iwe kubwa period. Mbona motor vehicle tunalipia na tupo makini sana maana tunajua tukivusha mwezi penalty ni 100% Tatizo la defaulters haliwezi kuisha ila nadhani we have to choose a lesser evil.•        Fungo Augustus Nadhani kwa mjadala huu na mingine mipana ijayo inaweza kuboresha huu utaratibu wa kulipa faini, mfano uholanzi fine ni kama mara tatu ya malipo halali kwa baadhi ya makosa. Mf. Bima, Parking and Crossing Zebra or Red Lights without stopping na hakuna uniform penalty km hapa bongo. Sijajua kwa nini kila kosa fine yake ni 30,000 Mohammed Mpinga maana makosa mengine ni madogo mno au ya onyo tu wakati mengine ni makubwa sana kutozwa elfu 30. Hili lifanyiwe kazi.
Afu pia uzoefu wangu unainesha kuwa askari ukishampa leseni yako lazima atafute namna ya kuiretain kwa kukutafutia kosa ila usipompa ni rahisi kukuachia so mara nyingi huwa nadeclare kusahau leseni au kutoa copy japo kwa sasa kwakuwa nishajua kuwa askari atakayetaka kubaki na leseni yangu itabidi anijazie form no 114 hili ndo ntalitumia zaidi•       
Asina A Omari Fungo Augustus umenikumbusha kitu hio PF 114 ni muhimu sana maana hii biashara ya kubadilishana number za simu na askari sio rasmi after all ile ni simu yake binafsi anaweza akaamua kuzima au akapata amri ya kuondoka alipo sasa leseni inakuwaje?? Janemary Ruhundwa ni kweli akili ni nywele! defaulters watakuwepo hio ndo fact but sie wengine tusiteswe kisa kuna wachache watakao default! I hope haya yote ytunayo toa kama mawazo yataat least kufikiriwa maana ….•        Mohammed Mpinga Nimesoma mawazo ya wengi kwa hakika ni mazuri tutayafikisha kwa wadau wenzetu na kama yatakubalika mwisho wa siku. Aidha kule SA J'Burg ukipatikana na Traffic Offence ukilipa pale pale unapata punguzo lakini kadri siku zinavyoongezeka kwa kosa hilo hilo utalipa zaidi na pia makosa hayalingani kwa faini tofauti na kwetu ambapo kosa lolote mmoja ni Tshs 30,000, pia wana mfumo mzuri wa kufuatilia wasiolipa fine.•       
John Seka Jamani hivi kungekuwa na askari 20 wenye akili kama kamanda Mohammed Mpinga nchi hii ingefika mbali sana. Ukiacha askari ambao ni classmates wangu sidhani kama nishawahi kukutana na askari engaging na anayejua polisi jamii. Sidhani kama ntakuwa nakosea kumtabiria makubwa Kamanda Mpinga (ingawa ofkoz wale wenzake wanaweza kuhisi anatafuta umaarufu) #mawazonandoto# Asina A Omari Janemary Ruhundwa Augustus FungoKamanda Mohammed Mpinga na Afande Johansen Kahatano wana kile kinachoitwa responsible leadership jambo ambalo kwa wenye akili finyu au akilisiasa watasema wanatafuta umaarufu ila kwa kweli kwa mtu km Mpinga kwa nafasi aliyonayo angeweza kujitetea sana kwamba hatujibu coz is too busy but muda mchache alionao anatufaidisha sana hapa na kikubwa yuko tayari kukiri udhaifu na kupokea mawazo mapya.
Emmanuel Kihaule hawa wawili Mohammed Mpinga na Johansen Kahatano ni Exceptional Kwa kweli kikao kilihudhuriwa na wajumbe kutokea mikoa mbalimbali Tanzania'walio mikoani walipata muendelezo wa kikao kupitia mitandao ya Kijamii km Telegram kwenye RSA-KULIKONI BARABARANI yenye wajumbe zaidi 150 hivi pia WhatsApp ya  RSA-KULIKONI BARABARANI-MKOA KILIMANJARO;
Pia Kamanda Mohamed Mpinga aliwapongeza japo yuko likizo:- Hongereni kwa kikao, naona kinakwenda vizuri, ahsanteni kwa clips mlizotuma.Pole sana Gagedu naamini bila shaka ulivaa Helmet na kama hukuvaa fikiria ingekuwaje, pia alitoa pole kwa mjumbe aliyepata ajali ya Pikipiki..
Kikao kiliendelea huku Mlezi wa RSA-anakaimu nafasi ya Kamanda Mohamed Mpinga alikuwepo Afande Kahatano ndiye alikuwa kwa niaba ya Kamanda hakika maswala yalikwenda Vizuri sanaaa!!!

Na Kauli mbiu;-USALAMA BARABARANI, NI JUKUMU LETU SOTE!!Wenu;

Mtanzani Jitambue-Dar es Salaam 29/03/2015

Jumapili, 15 Machi 2015

Hivi karibuni mbunge mtarajiwa wa jimbo la vunjo Ndg. Innocent Melleck Shirima ameweza kutimiza ahadi kwa kutoa zawadi ya mipira kwa mshindi wa mechi ya kirafiki kati ya timu ya marangu ttc na wageni wao iliyofanyika tarehe 08.03.2015 katika viwanja vya marangu ttc.

Mechi hiyo iliisha kwa timu ya Marangu ttc kuibuka na ushindi wa magoli matano kwa matatu dhidi ya wageni wao.

Mh. Innocent Melleck akikabidhi ahadi yake ya mipira kwa mshindi wa kwanza
Mh. Innocent Melleck akikabidhi zawadi kwa mshindi wa pili
Mh. Innocent Melleck akiongea jambo na vijana
Mh. Innocent Melleck akipiga picha ya pamoja
Mh. Innocent Melleck akifurahia jambo na vijana


Inaendeshwa na Blogger.

Machapisho Maarufu

Machapisho ya Karibuni

Recent Posts Widget