Jumamosi, 31 Januari 2015

Mhe.Mboni Mhita ambaye ni Makamu Mwnyekiti UVCCM TAIFA pia ni Kiongozi wa Vijana Africa Mashariki akiongelea Maswala ya Vijana Africa.
Akiongea na MTANZANIA JITAMBUE Ameseme;-Ninaongelea Mpango kazi wangu nilio tengeneza kwa Ajili ya vijana wa Africa mashariki.
Hasa swala la Amani, Ajira, Elimu, Afya, Fursa za vijana kwenye nafasi za uongozi,Fursa sawa kwa watoto wa kike.na mpaka sasa nimeshaweza kuyafanya mengi mno,
Ninampongeza Rais Jakaya kwa kuhusisha vijana kwenye nafasi za maamuzi
Na nafasi za uongozi
Na kuwaasa Viongozi wengine waige huo mfano huo wa Rais Dr.Kikwete wa Tanzania ni Mfano kwa marais wa Afrika na kwa sasa na baadaye kwani ameleta ufumbuzi wa mambo mengi mno, Uko mfano wa juzi pia ameweza kuwatanisha Viongozi wa Sudani na hakika sote tumeweza kuona...
Napenda kusema vijana wenzangu tujitume na katika kufikiria nchi yetu na nchi za Afrika kwa jinsi gani tutaweza kutatua yetu na pia tusiwe vijana wa kuchagua kazi za kufanya kwani kazi pia tunaweza kuanzisha wenyewe, Tuondokane na Siasa za kimuamko za kichochezi kwani Siasa hizo huleta machafuko na hii Amani ni Tunu kwetu vijana tuepukane na Siasa za machafuko kwani tunakuja kuataabika ni Sisi Vijana/wanakimama na Watoto....!!
Wito wangu kwa vijana tuungane na kushirikiana katika kutatua yetu kwa Umoja na Uaminifu.Ahsante sana
Pia MTANZANIA JITAMBUE iliwasiliana kwa simu na Ndg.Nassoro Kimario nchini Tanzania na kuweza kuongea naye kuhusu kiongozi wa UVCCM TAIFA-Ndg.MBONI MHITA yeye Alisema;- UVCCM tuliona uwezo wake. Na sasa Africa Imetambua uwezo wake.na kuongezea ni Makamu Mwenyeiti ambaye ni wa mfano kwa sasa na baadaye kwenye Umoja wa Vijana Tanzania....!!!
Mahojiano hayo yamefanywa na Mtanzania Jatambue-Nchini Nairobi

Jumatano, 28 Januari 2015

Wafanyabiashara wa Mbuyuni Sokoni wafungiwa Maduka leo na Manspaa ya Moshi, Mtanzania Jitambue yafanya mahojiano na Wafanyabiashara hao wamesema kodi imekuwa kubwa sana kwani ukienda TRA kodi,
Huku wanasema tusipange Bidhaa nje ya Duka,Kodi imepanda mara mbili ya kodi ya Zamani na ukipanga Kitu barazani hawataki hivi ukiweka ndani nani ataona hizo bidhaa???Wafanyabiashara hawataki kusikia Chadema kabisa hapa Moshi..
Wanalaumu Baraza la Madiwani wa Chadema kwa kupisha Sheria Ambazo kabla hawajawa na Council walisema tutapanga vitu nje ya baraza hata kwenye Barabara tutapanga ila sasa imekuwa tofauti na jinsi walivyotuahidi, 
Kuna aliyejitambulisha kwa jina:-Asha alisema Huyu Meya Jafar hatutaki hata kumsikia na madiwani wao kwani wametuahidi uongo mtu na sasa tunataabika hivi kama leo nimefika manspaa naambiwa nilipie Faini Tsh.700, 000 (Laki saba) na biashara nimefungua Tarehe 09/01/2015 na muda wote nilikuwa nafatilia TRA nimemaliza kulipalia TRA jana leo manspaa wanataka Hela zote hizi hivi ni maisha gani haya???
Naomba waangalie hizo Sheria zao na sisi wanatanzania tunaojituma kujikwamua kwa kukosa Ajira tunakuja kufanya biashara wanakuja kunifungia...

Wenu,
Mtanzania Jitambue-Moshi

Jumanne, 27 Januari 2015

Makamu Mwenyekiti wa UVCCM TAIFA-Mhe.Mboni Mhita ameshiriki Kwenye Semina ya Ujasiriamali na jinsi ya kufanya biashara na Marekani, Huku akiwa  ameongozana na Vijana 5 ambao walishiriki kuweza kupata elimu ya Ujasiriamali kutoka kwa Wamarekani kwa kweli Mhe.Mboni Mhita anapaswa kupongezwa sana kwani anajituma sana katika kuwatafutia vijana Fursa na kuweza kujitambua ambapo hatukuwa na Utaratibu huu ambao tunauona kwa Mhe.Mboni Mhita...
Na kupambana kwake ameweza na amehakikisha kuwaombea fursa,
Pia alisema kuna safari ya marekani ambayo nitaongozana nao hao Vijana 5 au Zaidi kwani anaongea na Wamarekani wampe hizo nafasi za vijana wake!
Kutoka na uhodari wake wa kutoa Semina kwa vijana hapo kwenye Semina hakika Wamarikani walimpongeza na kusema wanahitaji kiongozi wa aina yake na wamesema kwa hatua hii hakika Tanzania imepata kijana anayependa Taifa lake na watu wake mpaka wameweza kumualika aende Marekani akatoe Somo kwa gharama zao Marekani...
Mahojiano hayo yalifanywa na MTANZANIA JITAMBUE na kumpongeza sana kwani ni viongozi wachache huweza kujitolea hivi kwa vijana wa kitanzania...!!!
Wenu
Mtanzania Jitambue-Dar es Salaam

Jumapili, 4 Januari 2015


TAASISI YA WAZALENDO TANZANIA
Taarifa ya uteuzi wa viongozi wa Mkoa wa Mwanza tarehe 04/01/2015
Walioteuliwa ni:-
1: Ndg. Hamza Shido- Mwenyekiti
2: Ndg. Robert Gwanchele- Katibu
3: Ndg. Jensen Manyerere- Hazina na Maadili
4: Ndg.Kheri James- Habari na Maelezo
5: Ndg. Mtaalam Kanoute- Elimu na Jamii
6: Ndg. Jane Kajoke- Jinsia na Watoto
Taasisi ya wazalendo Taifa inawatakia majukumu mema uongozi wa wazalendo mkoa wa Mwanza


©Imetolewa na Idara ya Habari na Maelezo Taifa
Hassan husein- Katibu
Inaendeshwa na Blogger.

Machapisho Maarufu

Machapisho ya Karibuni

Recent Posts Widget