KIINIMACHO CHA UKAWA
MIONGONI MWA MBWEBWEZA LEO JANGWANI ETI NI KUSAINIWA KWA MAKUBALIANO YA
USHIRIKIANO.
SWALI:
1. KWANINI WANANCHI WAPIGE KURA YA HAPANA WAKATI WAO WALIKATAA KUPIGA KURA?
Hali hii ni kuonesha upeo mdogo wa kisiasa na kukosekana kwa dhamira sahihi na safi (japo ndio sifa asili ya
kila anae unga mkono demokrasia), pia nidhihirisho la uelewa finyu wa mbinu za kisiasa walizo nazo,
na pia wapo kimaslahi zaidi (sifa ya wanademokrasia na wenye fikra za kibepari)
2. CHAMA KIKUU NIKIPI KATI YA CUF NA CDM?
Vyama hivi vimekuwa na athari katika jamii kwa nyakati tofauti. Na kila kimoja kutaka kujulikana kina nguvu. Sasa kuungana lazima asili ibaki kukiri ninani ana kuwa mkuu. Kimaslahi viongozi wa
CDM hawatakubali kuwa chini ya CUF lakini CUF
kwa unyumbulifu wao kama walivyo funga ndoa na CCM wanaweza kukubali KINJE kama tunavyo shuhudia ndoa yao na CCM.
3. HALI YA UDINI KATIKA CDM NA CUF ITAZIKWA VIPI?
Nijambo dhahiri kwamba CDM kimekuwa na mrengo wa kanisa na shutma hizi zimekuwa nyingi kwa vigezo rahisi vya ngazi za utawala. Imekifanya kukubalika zaidi maeneo yenye waislam wachache, hata mbinu ya kuwaruhusu kina prof safari ni kujaribu kufifisha hoja hii, japo suala la Zitto
linachafua na kunasibihishwa na imani yake pia na ukanda. Nayo CUF katika mambo yaliyo irudisha
nyuma ni kunasibihishwa na Uislam japo kuwa
kiuhalisia hawana dalili yoyote ya uislam. Fimbo
hii ndio iliyo ifanya ikataliwe sana Tanganyika na kukubalika Zanzibar.
4. UMIMI WA CDM UTAISHAJE?
Baadaya kuwa chama kikuu cha ‘upinzani’ chadema haikuwa tayari kuunda serikali kivuli yenye kushirikisha vyama vingine. Walianza kubadilika kiukawaukawa kidogo lakini kijuujuu.
5. CDM ILIPOIONA CUF CHAMA KINACHOUNGA
MKONO USHOGA, IWEJE LEO KUUNGANA NA
MASHOGA, AU NAO WAMEKUBALI KUSIMAMIA USHOGA?
Hii nifikra na mtazamo mkuu wa CDM kwa CUF na haijasemwa nilini mtazamo huu ulifutwa, na ikitokea usahihi wake utakuwa upi. Yaani je itakuwa kigezo walichotumia kimeondoka au wamekubali haliilivyo. Japo katika akili na malengo ya kidemokrasia na kibepari (Baba yao
akiwa Mmarekani) ni “HAKUNA ADUI WAKUDUMU ILA MASLAHI ENDELEVU” au za kiyahudi kwamba
“TUNAO MAADU NA WATU WENGINE”, ni
imma watuunge mkono au wawe dhidi yetu.
6. NI VIPI MTAZAMO WA CDM KUHUSU NDOA YA
CCM NA CUF KWAMBA CUF IMEOLEWA, NAO NI
CCM?
Huu ni mtazamo ambao una nafasi katika kujenga mahusiano na ushirikiano. Namna unavyo mchukulia mshirika (ima hasi au chanya) ndivyo utavyo ishi naye. Kwakuwa ndoa ile haikuwa wazi
kimalengo na muda, haijulikani kama inaendelea au imekufa. Kama inaendelea (na ndio hali halisi, kwani Sharifu na CUF bado wamo serikalini pamoja) tuamini CDM nao wameingia katika ndoa,
au ni ndoa ya Mitala kwa CUF kuoa CDM na CCM. Sivyo kwakuwa ni CCM na CDM wenye nguvu kwa sasa na ndio wa kuhiari ndoa.
7. SLAA vs LIPUMBA NANI ATAKUWA TAYARI
KUMUACHIA MWENZAKE KUGOMBEA URAIS?
Kiasili wanamalengo tofauti; Slaa kama Padri,
Kaacha upadri katika madhabahu lakini sio katika imani na yanayo fanana, bilashaka waliomshawishi kujiunga upinzani na kugombea bado uwekezaji wao hauja lipa na matarajio hayaja fifia. Kadhalika Lipumba kwa mtazamo wa ‘waislam’ na pia walio
mshawishi na kuwekeza katika ugombeaji wake
bado wapo na wanamatarajio makubwa bado na mtu wao.
8. JE CDM ITAKUWA IMEHAMIA MAREKANI
ILIKUIFUATA CUF?
Kimsingi vyama vya ‘siasa’ katika nchi zisizo za kimfumo huwa na ushirika na vyama au nchi katika mataifa yaliyo na mifumo. CDM ni ujerumani na Uingereza kidogo. Wakati CUF ni Uingereza na sasa Marekani baada ya ndoa yao na CCM. CCM kwa sasa ni marekani (washirika wazuri katika siasa zao). Yupi tuamini kamuacha
na kumfuata yupi. Bado suala la maslahi linahitaji jicho la kindani.
9. HALI YA UMMAH WA TANZANIA KWANI BADO
KUFUNGUKA MACHO NA AKILI?
Kila mara wanasiasa wakidemokrasia wamekuwa wakiudanganya ummah kwa hoja nyepesi na ‘hovyo’. Bilashaka nao wanaona na wana maamuzi yao. Mfano, Tukisema wananci, au watanzania ni pamoja na wana CCM, CDM, CUF na wasio na vyama kwani chama sio kigezo cha uwana nchi katika TZ. Lakini kama tume ya warioba (wananchi) walitoa maoni ya katiba kwa mtazamo wao, na tume ya katiba (wananchi) wakatoa katiba kwa maoni yao vipi iitwe moja sio ya
wananchi? Leo katika mazungumzo ya Jusa
ameonesha upande wa ZNZ walitaka serikali ya
shirikisho la mkataba wakati TANGNYK walitaka muungano wa serikali 3, sasa kama Tume ya warioba imepitisha serikali 3, si kuendelea kuinyonga ZNZ?
10. UHALISIA NI UPI/
Vyovyote itakavyokuwa,
wana nchi wasitarajie neema yoyote kwa upinzani kama ilivyo kwa ccm. Na hii ni kutokana na vyama vyote kuwa vinafanana kimsingi na mitazamo.
Wote ni mabepari, wana demokrasia. Wakongwe na waanzilishi wa demokrasia na ubepari sasa unawatokea puani ila tu bado hawaja jua njia ya kutokea (Mfumo badili) lakini wamekinai, sembuse hawa wafuasi tu. Katiba hata ingepata maoni ya asilimia 100 ya si watanzania tu bali wanaadamu wote duniani kamwe haiwezi kumsaidia binadamu.
Hii ni kwa sabubu za kimaumbile, udhaifu wa
binadamu hajui ya baadae, na anaongozwa na hisia za umimi. Hawezi kuweka sheria ya kumpinga hisia zake.
Najua wengi bado hawaja ona njia
ya kutokea japo haswa wanataka kutoka.
JADILI KWA WELEDI SIO MATUSI AU UKISHINDWA PITA TU.
0 maoni:
Chapisha Maoni