Jumamosi, 6 Julai 2024

- SOKO LA BWILINGU NI FURSA KWA KILA MTU  AELEZA MHE. MBUNGE RIDHIWANI KIKWETE


Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambaye pia ni Mbunge wa Chalinze  Mhe.Ridhiwani Kikwete amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chalinze kuwapeleka Maafisa Maendeleo kukutana na kina Mama, Vijana na Kina Baba ili kuwaelekeza namna yakuunda makundi yatakayowawezesha kukopa fedha kwaajili ya kunufaika na fursa mbalimbali za mikopo ya Halmashauri ya asilimia 10  isiyo na riba ambayo imeanza kutolewa tena kuanzia tarehe 01.07.2024 baada ya Rais kuelekeza yafanyike maboresho ya utoaji mikopo hiyo ambayo inaokoa makundi maalum katika kujiinua kiuchumi.


Amesema "anataka vikundi vyenye utaratibu mzuri ambavyo vinatoa haki sawa kwa wanachama wote kunufaika na fedha hizo za mikopo na kwakuzingatia hakuna mtu mbabe, hakuna mtu mwizi, hakuna mtu anayetumia nafasi hiyo kujinufaisha mwenyewe kwakua moja ya jambo kubwa ambalo lilifanya utaratibu huo ukasimamishwa ni baadhi ya watu wanakuja katika jina la kikundi alafu fedha zinazoingizwa zinakwenda kwa mtu mmoja na yeye ananufaika pekeyake", alisema Mhe. Ridhiwani.


Ameyasema hayo kwenye mkutano na wananchi wa Chalinze mkoani Pwani ambapo ameongeza kuwa "maelekezo yameshatolewa na mimi kwangu ni maelekezo kwa Ofisi ya Mkurugenzi kuhakikisha kwamba wananchi wa Chalinze hususani wafanyabiashara wanakua ni sehemu ya kundi la kwanza lakufaidika na fursa hiyo, aliendelea kusema Mhe. Ridhiwani


Katika hatua nyingine Mhe. Ridhiwani amewaambia wananchi wa Chalinze kwa utaratibu waliojiwekea Baraza la Madiwani waliamua kutumia makusanyo ya ndani kwa kutenga fedha kwaajili ya ujenzi wa soko la Bwilingu na kununua baadhi ya majengo yaliyokuwepo katika eneo hilo ili kupata soko lenye ukubwa ambalo limewaweka wafanyabiashara wengi  kwenye eneo hilo, na litatumika na watu mbalimbali kutoka maeneo yanayozunguka eneo hilo na mikoa ya jirani kwaajili ya biashara zakujiingizia vipato.


Amesema "wananchi hawakukosea kuwachagua na kuwatuma viongozi wanaowatumikia kwakua wanatengeneza fursa ambalimbali zakibiashara bila ubaguzi kwa kuzingatia afya za wafanyabiashara na wateja wanaofika kupatiwa huduma katika eneo hilo, alisema Mhe.Ridhiwani.


Aidha amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amewezesha kila halmashauri kupata fedha hizo ambazo zinakwenda kuongeza vipato vya makundi maalum nakujikwamua kiuchumi.



Na.Elisa Shunda, Dar Es Salaam.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi  (CCM) anatarajiwa kuwa mgeni rasmi Katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Wazazi Kitaifa Julai 13 mwaka huu Mkoani Katavi.


Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam, leo tarehe 29/06/2024. Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi Tanzania Jumuiya ya CCM, Ndg. Ally Salum Hapi *(MNEC)* amesema  maadhimisho hayo yataanza  Julai 8 na kufikia kilele chake Julai 13 mwaka huu.


Hapi amesema  Katika maadhimisho  ya wiki ya Wazazi yataambatana na shughuli mbalimbali za kijamii na kichama,


Amesema shughuli zitakazofanyika katika maadhimisho hayo ni pamoja na ufunguzi wa Wiki ya Wazazi Kitaifa ambayo  itafanyika Julai 8  Wilayani Mlele Mkoani Katavi.


Aidha amesema katika ufunguzi huo wanatarajia kupanda miti zaidi ya laki  moja *(100,000)*


Hata hivyo amesema Rais Dkt. Samia Atawakagulia shughuli mbalimbali za ustawi wa Jamii ambazo zinafanywa na Dawati la jinsia la Jeshi la Polisi na  Shughuli zingine za Chama Cha Mapinduzi za usajili wa kielekroniki.


Wanatarajia pia kuwa na Kongamano la Maadili na Malezi, huku akisema Kama wanavyofahamu wanalo tatizo la mmomonyoko wa Maadili Katika Jamii na tatizo hilo linafungamana na malezi.


Amebainisha kuwa Katika maadhimisho ya Wiki ya Wazazi Kitaifa kutakuwa pia na usiku wa utamaduni ambao utashindanisha vyakula vya asili vya kitanzania.


Akizungumzia kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025, amesema Jumuiya hiyo imejipanga kuhakikisha inashiriki  kuhamasisha watanzania kujitokeza kuboresha taarifa zao kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga Kura na wapiga kura wapya wajitokeze  kujiandikisha.


Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unatarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu, ambapo kauli mbiu ya Maadhimisho ya wiki ya Wazazi Kitaifa kuhamasisha Jumuiya ya Wazazi  inaendelea kutoa mchango na kuhamasisha kufanyika kwa uchaguzi na watanzania kuhamasika kushiriki katika uchaguzi huo.


Mwishoo.

Inaendeshwa na Blogger.

Machapisho Maarufu

Machapisho ya Karibuni

Recent Posts Widget